Utabiri: Mgombea urais CCM 2025 hatakuwa Mwanamke

Hapa unataka kumvuruga mavi Lord denning

Yeye anaamini mama yupo mpaka 2040.

Kumbe kuna vidume vimeshacheza karata vinasubiri kumbetua mama kibabe kabla ya 2023.
 

Watu watatekwa fomu utairudishaje hapo Lumumba ON na Dom.
 

Sina hakika na unachozungumza kwenye hii post yako, au kwenye uzi huu, lakini mimi ni mmoja ya watu wasioamini tena kwenye uwepo wa CCM madarakani. Na ikibidi tuondoe kabisa huu mfumo wa chama kimoja kukaa madarakani kwa shuruti kwa muda mrefu. Naona akina Mwigulu wameanza kuiba pesa ili wakae madarakani kwa njia chafu.
 
Hakuna chama cha upinzani nchi hii kinaweza kulinda misingi na Tunu za Taifa. Kama hadi leo upinzani unafikiria kubomoa Taifa eti Muungano wa Serikali sijui tatu au nne; bila kutumia akili ndogo kwamba Dola ya Tanzania ilishaundwa, kufikiria kuchukua nchi iliyojengwa na kiumbe anaitwa Mwalimu Nyerere wasahau. Mungu pekee labda aamue.

Kutwa kutukana vyombo vya ulinzi na usalama, kudhalilisha nchi na mengi tu ya ovyo.# Nchi ina misingi.πŸ™πŸ™πŸ™
 
Fanya kazi kwa bidii upate hela za kulea watoto wako,
hizi siasa za nchi zinahitaji utulivu Sana ktk kuzifuatilia, tunahitaji mabadiliko makubwa ya kimfumo na kifkra kuliko kubadilisha badilisha watu,
Maana watu wengi hawasimami na hoja Bali wanaangalia watu
 

Hiyo misingi ni ya kiccm. Na kwa taarifa yako muda wa CCM kukaa madarakani umepita, huo muda wa kulinda misingi ya kukimbiza ushirikina uitwao mwenge umepita boss. Hakuna anayetukana vyombo vya dola, bali vyombo vya dola vinapewa ukweli wake kwa kujiingiza kwenye kuibeba CCM badala ya kulinda taifa.
 
Utabiri mfu huu.
Chief ameishapanga safu yake ni nani wa kumshinda?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…