Utabiri: Mungu tunaileta mbele yako kamati itakayopitisha jina la Rais wa Tanzania 2025

Nanga mkono hoja. Huyu anayejiita TumainiEl ni mjinga mmoja asititoe kwenye reli. Anawskilisha kundi lililokuwa limeshika hatamu wakati wa mwendazake. Siasa za mivutano, kuuana, kufunguliana makesi ya kubambikiza hazina nafasi tena. Tanzania yetu imetulia na iko salama kwenye mikono ya Rais Samia.
 
Mkuu Stuxnet , huyu TumainiEl sio mtu wa mchezo mchezo!, ni kati ya manabii wetu humu, hivyo sio mtu wa kupuuzwa!. Labda itakuwa ameambiwa ila kusema ameambiwa anaogopa!, sasa ndio anazunguka zunguka kutafuta namna ya kusema!.
P
 
Unaonekana uko desperate sana na Rais aliyepo sasa, ni hivi kila mamlaka inatoka kwa Mungu na kuna kila sababu njema nyuma ya jambo flani taifa linahitaji kiongozi aina ya Rais Samia angalau kwa vipindi 2 vya miaka 5 hivyo huyu tunae mpaka 2030.

Taifa linahitaji maridhiano na kwa sasa hakuna anayeweza kuleta hayo maridhiano ya kweli isipokuwa Rais Samia, taifa linahitaji katiba mpya na anayeweza kutupa ni Samia tu kwa sasa, taifa linahitaji mageuzi ya kweli ya kilimo, nishati na uchukuzi kisha tuhamie viwanda na biashara na kwenye hii transformation Rais Samia ameonyesha uwezo mkubwa wa kudili ni project kubwa na serious bila kupunguza nguvu upande wowote hivyo huyu anatufaa mpaka 2030 kaa mapenzi ya Mungu
 
Naunga mkono hoja
P
 
Mama Samia yupo vizuri kama Rais mstaarabu.
Lakini Kwa nchi yetu na nchi nyingi za Kiafrika na katiba zake alipaswa kumpa nguvu kubwa sana Waziri Mkuu Kasim majaliwa ili aendelee kuwakimbiza mchakamchaka mafisadi na wabadhirifu wa Mali za umma .

Hii nchi inatafunwa Kwa Kasi kubwa sana Kwa Sasa . Kila mtumishi wa umaa anawaza safari na posho za vikao TU . Angalia mpaka watu wa Hali ya Hewa wanatutabiria utumbo mtupu. Kwa maana kwamba hawana muda wa kufanya kazi yao kwa umakini na Kwa ufanisi. Watu ni makongamano kila siku. Hakuna Tena usimamizi mzuri wa matumizi ya fedha za umma. Makongamano na kukodisha maukumbi na kila siku Kwa mambo ambayo yalishapangwa miaka mingi badala ya kupeleka pesa kwenye miradi zinakwenda kwenye posho mifukoni mwa wachache waliobuni miradi ya safari na makongamano.

Miaka Mitano sio mingi lakini sio michache Kwa Kiongozi aliyechaguliwa na Mungu Kwa kazi aliyotumwa kuifanya .

Yesu Kristo Masihi na Mwana wa Mungu alifanya kazi yake kwa muda wa miaka Mitatu TU lakini kazi ya miaka Mitatu imeendea karibu Dunia nzima.

Mama Samia sio lazima akae miaka 10 ndipo afanye mabadiliko ya kifikra na kimtizamo. Anaweza akasimama uchaguzi mkuu ujao Kwa haki na Kwa usawa Kwa kiwango kitakachotupa Rais na viongozi waadilifu na Wazalendo hata kama yeye atakosa .Ataacha alama kubwa sana . Kundi linalomzunguka ndilo linalokua na hofu ya kukosa lakini yeye hata akikosa Bado ataheshimika na kuthaminiwa maisha yake yote.

Nchi hii Bado Ina safari ndegu ya kujenga misingi ya kiuchumi na kijamii zaidi kuliko siasa. Bado tatizo ni ufisadi sio mikutano ya kisiasa Wala kuandamana.
 
Asante kwa kutupa Jemedari Hayati John Pombe Magufuli. Asante kwakuwa hakumaliza kazi lakini yote nikwa utukufu wa Mungu.
NDO ULIPOHARIBU APO TUU
 
ana hofu ya Mungu.
Natamani YEYE ageuze uamuzi wake ili tusiendelee kuongozwa na yeye, maana naona yeye hana mpango wa kuachia 2025 licha ya mambo kutotuendea vizuri tuliowengi. Lakini yote kwa yote tunamwachia YEYE ili ajaribu kuongea kwa upole na yeye ili walau waya-solve haya mambo kwa amani kwa maslahi ya nchi yetu na kwa walio wengi pia. Maana sasa hivi naona wachache wana nguvu kuliko wengi. Na kutokana na nguvu zao, hata wakipiga kelele iwe mitandaoni au kwenye vyombo vya habari, basi sauti ya kwao ndo inasikika tu. Sauti za wengi zimemezwa na sauti za wachache!
 
Afadhali 004 aliitwa dhaifu, lakini alikuwa msikivu,

Huyu wa sasa mawaziri wanatajwa Kwa UFISADI Ripoti hii, inajirudia tena mwakani wanatajwa wale wale, Yeye Anavunga haoni😳😳

Tumepatwa na nn Nchi hii?
 
Huyo Mungu unayemsema huwezi kuthibitisha kwamba yupo.

Kama unabisha, thibitisha yupo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…