Utabiri: Mwaka huu hautaisha kabla ya Dola ya Marekani kufika 3000Tsh

Utabiri: Mwaka huu hautaisha kabla ya Dola ya Marekani kufika 3000Tsh

Upepo wa Pesa

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2015
Posts
21,600
Reaction score
35,158
Sio kwamba tunaongea au kuombea mabaya la hasha. Tunajaribu kuangalia hali halisi!

Mpaka kufikia leo katika bureu de change dola moja inanunuliwa kwa 2660Tsh. Hii rate inapanda kila siku kwa kasi ya ajabu!

Nikijaribu kuangalia uwezo wa viongozi tulionao (Samia, Mwigulu, Majalia nk nk) na nikiangalia hali ya uchumi na jinsi dola inavyo paa INATOSHA SEMA Mwaka huu 2024 hautaisha kabla USD 1 kuuzwa kwa 3000Tsh!

UPDATE:

Leo 4/7/2024 dola inauzwa 2710 kwenye maduka ya kubadili fedha.
 
Sio kwamba tunaongea au kuombea mabaya la hasha. Tunajaribu kuangalia hali halisi!

Mpaka kufikia leo katika bureu de change dola moja inanunuliwa kwa 2660Tsh. Hii rate inapanda kila siku kwa kasi ya ajabu!

Nikijaribu kuangalia uwezo wa viongozi tulionao na (Samia, Mwigulu, Majalia nk nk) na nikiangalia hali ya uchumi na jinsi dola inavyo paa INATOSHA SEMA Mwaka huu 2024 hautaisha kabla USD 1 kuuzwa kwa 3000Tsh!

Hii nchi watangayika wamepumbazwa na wakapumbazika .

Yaani nchi ina soko la ndani la watu mil. 65. Ina amani, ina raslimali za kutosha, imepakana na nchi Nane na Bahari inayopokea soko lote la Nchi za mashariki halafu Imegeuka kuwa nchi ya wachuuzi wasioweza hata kukusanya pesa za ushuru wa bandari na wa viwanja vya ndege.

Baada ya adui kuteka viwanja vya ndege vya Tanganyika na bandari sasa ipo siku atatuambia kuwa hatuna uwezo wa kujilinda tunahitaji ulinzi wa nchi nyingine kutoka Uarabuni kama ilivyo Ufaransa na baadhi ya nchi za Afrika ya Magharibi.

Haiwezakani mpaka hela ya kenya inapanda thanani wakati wahitaji malighafi na chakula kutoka Tanzania .

Wakenya wanaingia mpaka Vijijini kununua vyakula badala ya waTannganyika wenyewe kununua na kuweka kwenye maghala na kuwaizia wageni ili pesa za kigeni zibadolishwe kwenye mifumo rasmi.

Kelele za waziri wa kilimo ni nyingi lakini hatuoni wakijenga masoko mipakani.

One stop center zinatakiwa kwenye mipaka yote ili wanaoingia mipakani kununua mazao waapate masoko mipakani . Na pesa zipitie mifumo rasimi .

Mikopo Inachukuliwa kila siku halafu inaishia kwenye sadari za nje na ndani za kila siku na misafara mirefu inayotumia mafuta kutoka nje kwa kununua magari ya kifahari kila kukikcha .

Majengo ya serikali yanawekwa Furniture kutoka chini kwa mikopo kutoka ulaya .
 
Back
Top Bottom