Zanzibar 2020 Utabiri: Samia Suluhu kuwa Rais wa Zanzibar, Dkt. Mwinyi kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania

Hapo zama za kale Raisi wa Zanzibar ndie aliekuwa VP,lakini kutoka na ufefhuli aliofanya Kamando Salimini Amour,kufikia hadi kusema " hakuna Raisi mkubwa na mdogo Raisi ni Raisi tu"

Kinyemela bila kushirikisha Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla cheo cha makamo wa Raisi wa kuchaguliwa kikaundwa.

Hii yote ilifanywa kwa Madhumuni ya kupunguza nguvu za Zanzibar katika Muungano..

God bless Zanzibar, Tanzania and Africa as whole
 
Naunga mkono hoja nguvu ya VP inakuja tu ikitokea Lakutokea Kwamba yupo kwenye Top katika succession plan ila in common ni VP ni ceremonial figure
 
Dr.mwinyi Nampa asilimia Mia kwa Zanzibar,..
Yet ndie atakaeipeperusha bendera ya ccm Zanzibar...
 
+ 19. BALOZI ALI KARUME
 
Nawaona ccm wakipigana vikumbo kugombea uraisi wa Zanzibar lakini kama kawaida nimeona katika ndoto yangu Mh. Mazurui wa ACT akishinda kwa kishindo Uraisi wa Zanzibar dhidi ya Mpinzania wake ccm mwanamume maji ya kunde, Nikiwa naisubiri Tume ya uchaguzi itowe matokeo ya Mwisho,Ukazuka upepo mkali sana, na hapo hapo nikashtuka.
 
Ahaaaaaa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] lala Tena umalizie ndoto bwana . Rythm yako imeanza vizuri halafu umekimbia
 
Asee hawampi kule labda kwa goli la mkono na iwe kwa mbinde sana maana masheikh hawawezi wakaruhusu mwanamke atawale kule. Imbombo ngafu.
CCM haijawahi kushindwa kufanya tofauti na unachowaza leo.
Nani angelijua Gharibu Bilal angepotea kwenye ulimwengu wa siasa.
Nani alijua Mkapa angesimama 1995.
Nani alijua Magufuli angeshinda.

Mama Samia anaweza kuongoza Zanzibar bila shida yeyote.
Rekodi zipo ili zivunjwe.
Safari hii Zenji wake mkao wa Sapraizi
 
Ramli chonganishi hizi
Umenichekesha Sana [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]. Ahsante kwa kuniongezea siku za kuishi duniani
 
Tizama tamthilia ya DESIGNATED SURVIVOR na Scandal, utajua wanasiasa na watawala wanaandaliwaje.
Hautaamini macho yako na kuanzia siku hiyo utagundua Kila maamuzi Yana matarajio tofauti.
 
Uweli huyu mama katulia sana,ni moja kati ya viongozi wasiokuwa na papara katika uongozi wake,nawaza anauwezo wa kufika mbali zaidi kiuongozi.
 
Uweli huyu mama katulia sana,ni moja kati ya viongozi wasiokuwa na papara katika uongozi wake,nawaza anauwezo wa kufika mbali zaidi kiuongozi.
 
Samia kuwa rais nzanzibar inawezekana ila kutokana na mambo ya kiimani sidhani kama wale watu watakubali waongozwe na mwanamke
 
Tuachane na zanzibar yetu nyie komaeni na litanganyika lenu. Sisi raisi wetu kipenzi ni Maalim Seif Sharif Hamad
 
Tuachane na zanzibar yetu nyie komaeni na litanganyika lenu. Sisi raisi wetu kipenzi ni Maalim Seif Sharif Hamad
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] much respect [emoji106]
 
Mkuu Chabuso, kusema ukweli, elimu ya uraia inahitajika sana, hizo sio sababu, huna haja ya kutumia maneno makali kama ufedhuli, wala sababu ya rais wa Zanzibar kuondolewa umakamo wa rais sio ilifanywa kwa madhumuni ya kupunguza nguvu za Zanzibar katika Muungano bali kuulinda muungano.

Sababu halisi ni kuwa, rais wa Zanzibar alikuwa Makamo wa rais na mjumbe wa cabinet, and just incase anything happens kwa rais, Makamo wa rais anaapishwa kuwa rais.

Sasa kufuatia Tanzania kuingia mfumo wa vyama vingi ile 1992, kukawa na uwezekano wa Zanzibar kuwa na chama tofauti na Bara, hivyo rais wa Zanzibar ambae ni from opposition ataingia kwenye cabinet na just incase if anything happens kwa rais wa JMT, makamo wa rais ambaye ni opposition anaapishwa kuwa rais wa JMT. Hivyo wakabadili katiba na rais wa Zanzibar is nobody kwenye set up ya muungano, hivyo hata CUF ingechukua Zanzibar, JMT ni salama.

Ili kumpa heshima rais wa Zanzibar, Rais wa JMT atamteua kuwa Waziri asiye na Wizara maalum, ili aingie kwenye cabinet, Komando aligoma hata kuapishwa, Karume na Dr. Shein wamekubali uteuzi na wakaapishwa kama mawaziri wasio na wizara maalum, ila wamesusia kuhudhuria vikao vya cabinet.

Usikute ndio maana kuna fulani huwa anashinda lakini hapewi!.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…