Utabiri: Siku chache zijazo itatokea ajali ya Ndege ya abiria

Utabiri: Siku chache zijazo itatokea ajali ya Ndege ya abiria

Mkuu upo?

Kwani alisema ndege itaanguka bongo, je ingeanguka ulaya, Marekani au Asia???
Bado mngeendeleza huu unabii?

Natabiri timu moja ya mpira itaifungua timu nyingine....(Sijasema Simba wala Yanga au Manchester wala Barcelona)
Sijasema timu itashinda magoli mangapi, ila nimesema ina jezi nyekund(sio kijani/njano) 😂 😂 😂
Haya tafuta huu utabiri na utaupata sasa hivi...

Ndege itaanguka(wapi? timu gani... sijui) - 0% ushindi wa beti
ndege ina rangi ya nyekundu (jezi ya timu kijani/njano)- 0% ushindi wa beti
Timu itashinda magoli 3 (ndege kukatika vipande viwili) - 0 % ya beti
Goli la kwanza litafungwa na sijui(ooohh.....watu wengi watakufa - wangapi?.. oohh watoto wengi watakufa)-0% ya ushindi wa beti

Anza kuweka utabiri wako kwenye hela sio kutabiri, ili uitwe nabii....
 
Salaam Aleykum

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, nasikitika kusema kwamba siku chache zijazo kutatokea ajali ya ndege kubwa ya abiria ambayo itasababisha vifo vya watu ikiwemo watoto wadogo. Tuombe Mungu aepushe lakini kama ni maandiko basi yatimie.

1. Ndege itakuwa na Logo yenye rangi nyekundu.
2. Ndege itakatika vipande viwili katikati.
3. Maiti au majeruhi wa mwanzo kuokolewa watakuwa watoto.

Tusaidiane kuomba Mungu kwa pamoja ili ikiwezekana ajali hiyo isitokee
Kenya Airways au Zipo zenye wekundu na rangi nyingine
 
Salaam Aleykum

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, nasikitika kusema kwamba siku chache zijazo kutatokea ajali ya ndege kubwa ya abiria ambayo itasababisha vifo vya watu ikiwemo watoto wadogo. Tuombe Mungu aepushe lakini kama ni maandiko basi yatimie.

1. Ndege itakuwa na Logo yenye rangi nyekundu.
2. Ndege itakatika vipande viwili katikati.
3. Maiti au majeruhi wa mwanzo kuokolewa watakuwa watoto.

Tusaidiane kuomba Mungu kwa pamoja ili ikiwezekana ajali hiyo isitokee
Rangi ni tofauti
 
Ndio mkuu ni katika ndoto wala sipigi ramli wala sina uwezo wa kuchagua jambo la kuonyeshwa,huwa ni only serious issues
Kwenye ndoto sawa inawezekana, mi Mwanangu wa darasa la tano Kama mwezi hivi umepita,aliota Baba yake ninefariki na wako msibani kwenye mazishi yangu,akaamka asubuhi akamwambia Mama yake,na Mama yake akaniambia,nikasema msijali ni ndoto tu hakuna kitu Kama hicho! Baada siku mbili kupita tu,tukapokea taarifa za msiba wa Mama Mkwe Bibi yake na Mwanangu! Basi tukasema kwa pamoja kua ndiyo ile ndoto ya Mtoto imetimia Sasa!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Siyo wabongo tu mkuu. Mara nyingi si rahisi kuamini hivi vitu. Ni nature ya binadamu. Likishatokea ndo kumbu kumbu zinakuja kwamba hili jambo lilizungumzwa.

Mfano kuna yule jamaa aliyesemaga ameona bendera ikipepea nusu mlingotihalafu akasema tuombee sana ikulu. Some days after, mzee Magu akafariki
Sheikh Yahaya na utawala wa juu hadi wahariri wakimbeza wakamuona hamnazo.
 
Utabiri ulitimia kwa 80% kwa sababu
1. Siku chache zijazo
2. Kuna ajali
3. Ajali ya ndege
4. Ndege ya abiria
5. Watu watakufa
6. Miongoni mwa watakaookolewa ni watoto
7. Itakatika vipande viwili X
8. Ina logo nyekundu X
Hakuna pua ya ndege umeona imebebwa toka ziwani mkuu? Au vipande viwili vilitakiwa viweje/ukubwa gani?

Huo unjano pia ni matokeo ya uwepo wa nyekundu. Utundu wa mafundi rangi wanalijua hili. Mama wa rangi zote ni rangi 4 tu; orange si sehemu yazo. Zikichanganywa ndio tunapata zaidi ya rangi hata mia.

Zaidi ya yote: utabiri/ndoto ni kambo ya kiroho (fumbo) kupata usahihi wa tafsiri ni shule nyingine na angalau fasiri itolewe na mtu tofauti na muona maono. Ni nadra kuzikuta hizi karama kwa mtu mmoja. Huyu mwamba katoa alivyoona inafaa na upande wangu kapatia 100%

Ingekuwa wenye ndoto ni mimi na wengine katika hili tungeona njiwa mwenye madoa doa anaanguka ghafla. Badala minofu na manyoya kusambaa wangetoka nzi wakiwa hai na wengine wamekufa. Basi ingeishia hapo. Kuja kupata tafsiri ya ndege ulaya, sijui abiria hadi nembo ni kiwango kingine cha level ya aliens[emoji122]
 
Duuuh mkuu we hatar na vp uliota kama ndoto au uliona maonao na je ni vingi huwa vinatokea au ndio hii ya kwanza kuota na kutokea na je huwa unachukua maamuzi gani au huwa unafanya nini baada ya tukio unapoona kitu kimetokea kama ulivyoota na upo kwenye Imani gani ya dini christian or Muslim
 
Mtabiri kataja ndege kuanguka na kukatika vipande viwili, lakini pia kaona rangi nyekundu, simple tuutafsiri utabiri wake, ndege kuanguka ni 100% , ile rangi nyekundu alifichwa yawezekana ni damu iliyomwagika baada ya vifo, ndege kukatika vipande viwili hii haijatokea lakini how if ingeanguka kutoka anga ya juu sana pale kahama na sio sehemu ya maji kama ziwani hali ingekuaje? Kiasi kikubwa utabiri wake umetimia
Ukituluzia Akili Utabiri Umetimia Kwa Asilimia Kubwa. Kwanza Dhumuni kuu Ajari Ndo Iyo. Rangi Nyekundu Kama Ulivyo Sema Ni Dam Ni Kweli, Swala La Mtoto Mdogo Apa Unaona Ni mtoto Mdogo Alie enda Kuoka Watu Kwenye Ile Ajari Na Kama Taifa Tumetambua Mchango wake Kila Sehem Kaimbwa bwana Mdogo Majaliwa UkilinganishaUshujaa Alioufanya Na Umri wake Hakika Ni Mdogo Mno. Sasa Hapa Ndo unaangalia Kwa undani Zaid kwa sababu Utabiri Uwekwa Code Ndo Kama Hizi Mtoto mdog Kaokoa Nafsi Za watu Wengi Na Kwake Pia Nadhani Anaokolewa Na Umaskini yeye Na Familia Yake. Swala La Vipande Viwili Nadhan Mnajua Ndege Ndani Ina Sehem Mbili Sehem Ya Rubani Na Abiria. Baada Ya Ajari Unaona Upande mmoja (Abiria) Wanapata Msaada Na Wengi Kuokoa Nafsi zao Lakini Upande wa Pili Wa Rubani Wanashindwa Kupata Msaada kwa Uzembe Wa mtu mmoja Na kusababisha uu Upande wa Pili Watu Wote kupoteza Maisha Na Ukimsikiliza Shuhuda Vifo Vya Upande uu Vinatia Sana Huzuni.
 
Hakuna pua ya ndege umeona imebebwa toka ziwani mkuu? Au vipande viwili vilitakiwa viweje/ukubwa gani?

Huo unjano pia ni matokeo ya uwepo wa nyekundu. Utundu wa mafundi rangi wanalijua hili. Mama wa rangi zote ni rangi 4 tu; orange si sehemu yazo. Zikichanganywa ndio tunapata zaidi ya rangi hata mia.

Zaidi ya yote: utabiri/ndoto ni kambo ya kiroho (fumbo) kupata usahihi wa tafsiri ni shule nyingine na angalau fasiri itolewe na mtu tofauti na muona maono. Ni nadra kuzikuta hizi karama kwa mtu mmoja. Huyu mwamba katoa alivyoona inafaa na upande wangu kapatia 100%

Ingekuwa wenye ndoto ni mimi na wengine katika hili tungeona njiwa mwenye madoa doa anaanguka ghafla. Badala minofu na manyoya kusambaa wangetoka nzi wakiwa hai na wengine wamekufa. Basi ingeishia hapo. Kuja kupata tafsiri ya ndege ulaya, sijui abiria hadi nembo ni kiwango kingine cha level ya aliens[emoji122]
Mku tuko pamoja kabisa, nilikuwa najibu wanaobeza utabiri
 
Sijamaliza niliweka maandazi sasa hivi naongezea na chai .View attachment 2409466

Credit mnazompa za bure kabisa .Hajataja muda ,pamoja na makosa mengine.

Na mimi natabiri ,lazima mimi siku moja nice.
Dada wala sihitaji credit kutoka kwa mtu yeyote lakini jua kwamba nina kipawa na nina uwezo wa kupata maono katika jambo lolote,hivi hujiulizi kwanini sijasema ajali ya gari?au unadhani ajari za gari huwa sizionagi?
 
Kwenye ndoto sawa inawezekana, mi Mwanangu wa darasa la tano Kama mwezi hivi umepita,aliota Baba yake ninefariki na wako msibani kwenye mazishi yangu,akaamka asubuhi akamwambia Mama yake,na Mama yake akaniambia,nikasema msijali ni ndoto tu hakuna kitu Kama hicho! Baada siku mbili kupita tu,tukapokea taarifa za msiba wa Mama Mkwe Bibi yake na Mwanangu! Basi tukasema kwa pamoja kua ndiyo ile ndoto ya Mtoto imetimia Sasa!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Yap ni kweli Mungu huzungumza na watu katika ndoto...jitahidi uwe na diary na peni karibu unapolala na uandike ndoto zinazokushtua sana au ambazo huzielewi.Tafuta maana na uziombee kama kuna baya Mungu akuepushe na kama kuna zuri Mungu alitimize.Mimi binafsi hufanya hivyo na ninaona mafanikio makubwa.Tatizo wengi hupuuza na kushangaa mambo yanawatokea ghafla..
ANGALIZO:usitafute ushauri wa ndoto yako kwa wapiga ramli na waganga au washirikina....Tafuta kwa watumishi wa Mungu na wale waliopewa vipawa vya utafsiri toka kwa Mungu
 
Mkuu kuna baadhi ya siku huwa natembezwa kuonyeshwa baadhi ya mambo na nnachoneshwa lazima itimie coz huwa ni mpango wa Mungu ambao ameshakadiria itokee.Kwakuwa ni mpango wa mungu na sio Shetani basi huwa haiwezekani kubadiri hata kwa dua au maombi kwani huwa ni mambo ambayo muda wake wa kutimia huwa umefika.
Uokoke uwe mlokole ndugu MUNGU atakutumia kwa viwango vya juu sana maana kuna kipaji cha maono makubwa atakuongezea
 
Back
Top Bottom