Utabiri: Tundu Lissu kuwa 'mediator' wa 'Truth and Reconciliation Commitee'. Uwezo wake hauna shaka

Utabiri: Tundu Lissu kuwa 'mediator' wa 'Truth and Reconciliation Commitee'. Uwezo wake hauna shaka

Uwe unampenda au humpendi utakubaliana na mimi kwamba Mh Tundu Lissu ni tunu ta taifa. Sitaki kurudia mambo mengi yaliyopita lakini kwa ufupi ni kuwa yale yoote aliyotuonya wana wa tanzania kuhusu utawala bora na sheria sote tumeshuhudia athari zake. Athari kwa watanzania wote, wenye vyama na wasio na vyama.

Sasa kumekucha, chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, kiongozi shupavu anayejiamini ambaye uwezo wake hautiliwi shaka sasa analenga kuleta utengamani wa kitaifa.

Inapendeza sana watu kukaa kwa upendo.

Leo imetamkwa rasmi kwa kauli ya Waziri wa Mambo ya ndani Mh Masauni kuwa sasa ni wakati mwafaka waliokimbia nchi warudi tujenge nchi pamoja kwa upendo.

Hii ni hatua ya kupongezwa, ni ushujaa kwa Rais.

Jambo lingine linalitarajiwa ni Truth and Reconcilialtions yaani Ukweli na Usuluhishi. Chini ya Tundu Lissu mpenda haki ninaona Bright Future is coming. Ni kiongozi wa kuaminika.

Aliwahi kukiri hadharani Mbunge wa CCM wa jimbo la Mvumi Dodoma Mh Lusinde kuwa pamoja na tofauti zao za kisiasa lakini Tundu Lissu ni Mtu mwadilifu sana, mwelewa, mpenda maendeleo na hanunuliki.

Karibu Home Mh Tundu.
Umekuwa role model kwa vijana wa Tanzania
Mwamba anarudi. Ni Yeyeeeee
 
Naelewa sana. Na nilitarajia swali kama hili.
Wengine mtasema anakuwaje mediator wakati yeye ni kati ya pande mbili zinazohasimiana? Kwa lugha nyingine anahitajika Third paty. Au sio

..labda Lissu anafaa awepo kwenye Tume itakayoshauri kuhusu muundo, mamlaka, na namna tume ya ukweli na maridhiano itakavyofanya kazi.

..kuhusu yeye kuongoza, au kuwa mjumbe wa tume hiyo, nadhani haitakuwa muafaka kwasababu yeye ni mmoja wa Watz ambao wanatarajiwa watakwenda kutoa ushuhuda na ushahidi wao mbele ya tume ya maridhiano na ukweli.

..kwa upande mwingine, ni lazima tukiri kwamba Lissu ni miongoni mwa Watz wachache wenye uelewa mkubwa wa historia, sheria, na katiba, hapa Tz.

..Ni Watz wachache sana wenye uwezo wa kuzichambua sheria zetu ktk muktadha wa kihistoria, kubainisha mapungufu yake, na kupendekeza namna ya kiziboresha, kama anavyofanya Tundu Lissu.
 
hii kauli ya ''anaupiga mwingi'' hivi inaeleweka kweli au mazoeya tu kusema bila kujua unasema nini?
Kuupiga ni kuupiga tu. Haihitaji tafsiri ya kitaalam sana
 
labda Lissu anafaa awepo kwenye Tume itakayoshauri kuhusu muundo, mamlaka, na namna tume ya ukweli na maridhiano itakavyofanya kazi.
Ni kweli. Niliwahi kusikiliza hotuba yake kuhusu hilo la muunda liko poa sana
 
Back
Top Bottom