Utabiri: Tundu Lissu kuwa 'mediator' wa 'Truth and Reconciliation Commitee'. Uwezo wake hauna shaka

Mwamba anarudi. Ni Yeyeeeee
 
Naelewa sana. Na nilitarajia swali kama hili.
Wengine mtasema anakuwaje mediator wakati yeye ni kati ya pande mbili zinazohasimiana? Kwa lugha nyingine anahitajika Third paty. Au sio

..labda Lissu anafaa awepo kwenye Tume itakayoshauri kuhusu muundo, mamlaka, na namna tume ya ukweli na maridhiano itakavyofanya kazi.

..kuhusu yeye kuongoza, au kuwa mjumbe wa tume hiyo, nadhani haitakuwa muafaka kwasababu yeye ni mmoja wa Watz ambao wanatarajiwa watakwenda kutoa ushuhuda na ushahidi wao mbele ya tume ya maridhiano na ukweli.

..kwa upande mwingine, ni lazima tukiri kwamba Lissu ni miongoni mwa Watz wachache wenye uelewa mkubwa wa historia, sheria, na katiba, hapa Tz.

..Ni Watz wachache sana wenye uwezo wa kuzichambua sheria zetu ktk muktadha wa kihistoria, kubainisha mapungufu yake, na kupendekeza namna ya kiziboresha, kama anavyofanya Tundu Lissu.
 
hii kauli ya ''anaupiga mwingi'' hivi inaeleweka kweli au mazoeya tu kusema bila kujua unasema nini?
Kuupiga ni kuupiga tu. Haihitaji tafsiri ya kitaalam sana
 
labda Lissu anafaa awepo kwenye Tume itakayoshauri kuhusu muundo, mamlaka, na namna tume ya ukweli na maridhiano itakavyofanya kazi.
Ni kweli. Niliwahi kusikiliza hotuba yake kuhusu hilo la muunda liko poa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…