Utabiri wa Sheikh Yahya Hussein mwaka 2006 na Tanzania kuwa na Rais Mwanamke

Utabiri wa Sheikh Yahya Hussein mwaka 2006 na Tanzania kuwa na Rais Mwanamke

huyo mzee aliingia kwenye 18 za GWAJIMA.GWAJIMA akapiga maombi jamaa akakata moto
 
Sasa mbona alishindwa kujitabiria kifo chake?
Ethics haziruhusu. Hata madaktari hawaruhusiwi hata kutibu relatives wao. Na ndio maana na waganga wa kienyeji kuwatafutia watu dawa za utajiri lakini wao hubakia maskini.
 
kifo chake alitabiri, na ukitaka kujua hili alianza na kumuandaa mwanae kwa kumpeleka kwenye vipindi vyake radioni na pia alitabiri kifo chake kwa namna ya ajabu (isiyokubalika kidini) alisema: Tarehe fulani(alitaja jina) itakuwa kiama, kama si kiama basi mimi ntakufa, HILI HALIKUWA ZURI KIDINI

Nakweli ndio siku alokufa mwenyewe, jamaa alikiwa vizuri kwenye utabiri japo mimi sio muumini wa mambo hayo
Kweli nakumbuka kabisaa
 
Humu nishakuta uzi wa 2020 mtu akisema rais atakufa na vp atakua rais ila kwa muda mfupi kisha atakua mwingine.

Nishakuta uzi wa 2018 ukisema mtarudi hapa kukoment kwa furaha.

Leo bwana Yahya kuna uzi wake wa kutabiri uongozi wa kipindi kifupi.

Mbona kama vile watu walilijua hili kuanzia mwanzo? Was it so obvious?
View attachment 1730612
Interesting! Una maana ya kuwa hata mama Samia naye atatutoka baada ya kuteua makamu wa rais mwingine? Don't tell me that!! Tunahitaji uongozi wake sasa more than ever!
 
Kwahiyo sisi tutaamini vipi Kama hii ni habari ya kweli??
 
Kuamini katika mambo ya utabiri ni moja ya makosa makubwa ya kishirikina kwa mujibu wa Imani ya kiislam
Wewe dini huijui watabiri wengi ni wasomi wakubwa wa dini ya kiislam
 
Basi sawa...kuna kingine tena alichotabiri tukitarajie?
(A)--Alitabiri Simba atafungwa na yanga matokeo yake ikawa tofauti.

Akaokolewa na police baada ya genge la mashabiki wa Simba kuvamia kwake Magomeni..


(B)--Ila ninachokumbuka ni shehe yahya kusema Tanzania itatawaliwa na mwanamke wakati wa mchakato wa uchaguzi na kikwete kupita kupitia ccm.

Akipoulizwa kwann ulisema atashinda mwanamke?

Akasema ktk utabiri wa nyota hazitambuwi majina ya mtu,

Bali nyota zinatambuwa namba.
Kama ilivyo computer.

Kwahyo kikwete ana nyota ya kike kupendwa na watu..

Watu tulimuelewa hivyo...hayo mengine sidhani kama yana ukwl.

Na haukuwa utabiri wa siri bali ulitolewa kwenye magazeti kipindi hicho 2005..
 
Lete picha (ushahidi wa video) sio brah brah na kutishana...
 
Kutabiri ni kama kubet tu ukichana mkeka unakaa kimya mkeka ukitiki lazima uanikwe.
 
Ni kweli kabisa hii niliwah isoma kweny gazet la KIU..mwaka 2012..... Kipindi Niko School!!

Nalkumbuka hili gazetii japo muda ulikua umpitaaa....

Lakin kuna rafik angu alkuja nalo shule!!!
Watu walibishan mnooo....nalkumbuka ile siku.,......

RIP Mnajimu!!!!
 
20210319_133454.jpg
 
Nimesoma hii article pale kwenya magazeti ya Shigongo, ikanishtua kwa vile inaoneka utabiri wake ulikuwa kweli kabisa. je ni coincidence tu au ni kweli alikuwa anajua kupiga mahesabu ya kuona mbele? Najua kuwa aliwahi kutabiri kuwa mtu yeyote atakayechukua formu kumpiga Kikwete mwaka 2010 angekufa ghafla, watu ndani ya CCM ambao walikuwa wameshapanga mkakati wa kumng'oa Kiwkete mwaka 2010 wakaa kimya kabisa.

ALIYEKUWA Mtabiri maarufu Afrika Mashariki, Shehe Yahya Hussein aliitisha mkutano wa wahariri na waandishi wa habari mwaka 2006 na kuzungumzia utawala wa Rais Jakaya Kikwete ukiwa na umri wa mwaka mmoja tu.

Baada ya kuzungumza hayo nilipata nafasi ya kumuuliza. Je Tanzania baada ya Kikwete inaweza kupata rais mwanamke?

Shehe Yahya alinijibu:

“Baada ya vipindi viwili vya Rais Kikwete atakuja rais ambaye ni mweusi mchapa kazi lakini mchekeshaji sana, hata hivyo atatawaka kwa kipindi kifupi tu hapo ndipo Tanzania itapata rais mwanamke.”

Wahariri na waandishi waliguna kuonesha kutokubaliana naye wakiwemo wahariri wakongwe Hemedi Kimwaga, Yasini Sadiki, Magnus Mahenge na wengine ambao siwezi kuwakumbuka.

Shehe Yahya baada ya kuona tunambishia alichukua ubao kama ule wa darasani na mkononi alishika kutabu kilichoandikwa Astrology: Monthly numerology, akaanza kufanya hesabu kwa fomula anazojua yeye na akatuambia kwamba kwa Jakaya inaonesha atamaliza muda wake wa miaka kumi na lakini ajaye ataongoza kwa kipindi kifupi.

Tulimuuliza ataongoza kwa muda mfupi kwa sababu gani, alisema hayo mengine yeye hawezi kujua lakini akasisitiza kwamba hivyo ndivyo itakavyokuwa. Tulitawanyika pale kila mmoja akiwa anaona kama amepigwa ‘changa la macho’.

Lakini sasa nimeng’amua kwamba kumbe alikuwa akimtabiria mama Samia bila yeye mama kujua tulichokuwa tunafanya.

HAKIKA SHEHE YAHYA ALIKUWA MNAJIMU WA KWELI.

Kumbuka haya yanatokea baada ya miaka 15 ya utabiri wake na mtabiri akiwa katangulia mbele za haki. Sheh Yahya alifariki mwaka 2011. Mungu ampe raha ya milele na amnusuru na adhabu ya kaburini.
Uongo mtupu. Leteni huo ukurasa wa Hilo gazeti tuusome. Sio kutuketea ngonjera hapa baada ya kuwa tukio limeshatokea halaf ndo museme utabiri. Hakuna utabiri Kama huo
 
Back
Top Bottom