Utabiri wa Sheikh Yahya Hussein mwaka 2006 na Tanzania kuwa na Rais Mwanamke

Wakuu nimepita sehemu nikaikuta hii meme ambayo ilitengenezwa na Wataalam iki mnukuu aliyekuwa mtabiri na msoma nyota mashuhuri Afrika Mashariki na kati marehemu Sheikh Yahya Hussein, vipi huyu marehemu alikuwa anaona mbele zaidi?

Alichokitabiri kwa asilimia kubwa kimetimia, vipi mwaka wa uchaguzi 2025,Vyama vikuu vya upinzani ACT WAZALENDO na CHADEMA, Vitaigeuza CCM kuwa chama cha upinzani?

 
 
Rejea tabiri zake 2010,

Aliwahi kutabiri kuwa rais Mstaafu Benjamini Mkapa atapewa kazi kubwa duniani baada ya mwaka mmoj alipewa kazi n UN kusimamia mchakato wa kura ya kujitenga ya Sudan Kusini
 
Huu mwaka 2011 ni mwaka wa ajabu sana

osama alikufa 2011
Gadaffi alikufa 2011
mabomu mbagala 2011
ckujua km nae huyu shekhe alikufa 2011
Km aliyasema haya napata ?
 
Ebu tuwe wakweli, ni upinzani gani wa kuchukua nchi?
 
Ulongo mtupu,leteni video Tuamini.
Kipindi hicho video zilikuwa adimu sana, media zilizokuwa kwenye chati wakati huo ilikuwa magazeti na redio. Huo utabiri ni kweli aliufanya kabla ya kifo chake na sikuuamini sana mpaka nikausahau..... Lakini amepatia kwa kiasi kikubwa, tungoje kuona kama 2025 upinzani utachukua nchi.
 
Nikweli nimeukumbuka utabiri huo aliitisha press conference akasema hayo , nakumbuka kidogo wachungaji walimtangazia Vita ya Imani , ndoto y Raisi mweusi aliisema (magufuli)
 
Mhu! Nilikuwa nafuatilia uchaguzi wa India na Africa Kusini nikajifunza kwamba vyama vikongwe duniani vinaendelea kupoteza 'mass support' nadhani kwa sababu ya kwamba 'mwenye shibe hamjui mwenye njaa'.
 
Natamani mabadiliko yapatikane lakini pia sioni wa kubadili huko upinzani au kama vipi tubeti tu, tuwajaribu na wao.

Kuhusu hiyo meme, hakuna ushahidi kuwa alisema sheikh yahaya, hilo moja pili hata kama kasema siamini mpaka itokee
 
Nyie mwasema. Unajua marekani pamoja na demokrasia yote iliyopo pale, "hakujawahi kuwako raisi mwanamke"
 
Weka video ya huo mkutano..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…