Utachukua hatua gani ukigundua watoto unaolea siyo wa kwako?

Utachukua hatua gani ukigundua watoto unaolea siyo wa kwako?

KikulachoChako

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2013
Posts
19,185
Reaction score
37,239
Habari za muda huu wapendwa...bila shaka sote tuwazima wa AFYA.

Maisha ya kimapenzi yamejawa changamoto na vitimbi vya kila aina. Mara nyingi wale tuliowapenda na kuwathamini ndio wanaotuletea vunjiko la moyo na maumivu yasiyoisha. Wahenga wanasema kuwa lisemwalo lipo kama halipo laja.

Uaminifu umekuwa jambo adimu kwenye ulimwengu huu uliojawa jeuri, vitimbi na tamaa kwenye mioyo ya binadamu. Je ukipata kujua kuwa watoto unaowalea sio wa kwako utachukua hatua gani?

Inawezekana majibu yetu yakatoa muongozo kwa Wenzetu wanaopitia haya na wahenga walisema mwenzako akinyolewa na wewe tia maji.

Karibuni tujadili......!!
 
Unawalea tena watakuja kukusaidia kwa kutambua wema ulio wafanyia
 
Haya mambo ni mengi mno kwenye ndoa zetu. Lakini omba Mungu yasikukute, kwani huleta hasira na kuvunja mahusiano.

Kikubwa yakikutokea usichukue uamuzi kwa hasira. Angalia kama mapungufu yapo upande wako eg Kukaa mbali na mwenza, kukosa nguvu za kiume nk. Inabidi uvumilie.

Lakini kama tatizo ni uaminifu mdogo wa mwenza (piga chini). Unaweza ukaishi na mwenziyo lakini hakupendi na wala hataki kuzaa nawe (piga chini).
 
Habari za muda huu wapendwa...bila shaka sote tuwazima wa AFYA......

Maisha ya kimapenzi yamejawa changamoto na vitimbi vya kila aina......mara nyingi wale tuliowapenda na kuwathamini ndio wanaotuletea vunjiko la moyo na maumivu yasiyoisha.....

Wahenga wanasema kuwa lisemwalo lipo kama halipo laja......

Uaminifu umekuwa jambo adimu kwenye ulimwengu huu uliojawa jeuri, vitimbi na tamaa kwenye mioyo ya binadamu......

Je ukipata kujua kuwa watoto unaowalea sio wa kwako utachukua hatua gani.......??

Inawezekana majibu yetu yakatoa muongozo kwa Wenzetu wanaopitia haya na wahenga walisema mwenzako akinyolewa na wewe tia maji.......

Karibuni tujadili......!!
Hakuna kitu inauma kama kudate na girlriend mmoja tu huyohuyo alafu baadae unakuja kugudua kumbe ni girlfriend of the people for the people to the people by the people[emoji29]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani kwamba mke wako amekusaliti kadunyana na mtu mwingine na watoto kakuletea ndani ya ndoa na wewe unalea na unakuja kugundua sio wa kwako.. HAINA HAJA YA KUGOMBANA.. hapa ndio ongezeko kubwa la vifo linapozaliwa tumia HEKMA.. na uanze maisha yako ya mahusiano tena
 
Hakuna kitu inauma kama kudate na girlriend mmoja tu huyohuyo alafu baadae unakuja kugudua kumbe ni girlfriend of the people for the people to the people by the people[emoji29]

Sent using Jamii Forums mobile app
Lakini pia kuacha mke sio jambo jepesi......nadhani waliooa wanajua....
 
Inategemea nahaya.

[emoji117]Umri wako Mwanaume.

[emoji117]Uwezo wako wa kuzalisha.

Ikiwa Umri umeenda sana yaan mtoto wa mwisho yupo lasaba huko...Kausha ..... Hapa kuanza Upya ni sawa na UJINGA ,ukizingatia hao watoto wangekua wakijua wewe ni Baba.

Ikiwa ndo kwanza una 25--35 ,ACHANA NAYE.

Ikiwa umri umeenda au hujaenda lakini Unajijua huzalishi, hujawah kua hata na wkausingiziwa,zaidi ya yote umezunguka sana nakila mahal unaambiwa huwez kuzalisha ......Kausha tu, Mkeo kaamua kukufichia aibu , nakama mkeo alikua unaenda kujitegesha, na hawaambii wanaomtunga mimba kua nizao.

Wee Kausha tu , Lea ,watoto wakutambue kama baba...

HATA IVO, KATIKA UAMUZI WOWOTE ULE, WEE CHAGUA AMBAO UNAKUPENDELEA WEWE, UNAOKUPA FAIDA KWANZA WEWE, ALAFU WATOTO. WAMWISHO AWE MWANAMKE.
 
Habari za muda huu wapendwa...bila shaka sote tuwazima wa AFYA......

Maisha ya kimapenzi yamejawa changamoto na vitimbi vya kila aina......mara nyingi wale tuliowapenda na kuwathamini ndio wanaotuletea vunjiko la moyo na maumivu yasiyoisha.....

Wahenga wanasema kuwa lisemwalo lipo kama halipo laja......

Uaminifu umekuwa jambo adimu kwenye ulimwengu huu uliojawa jeuri, vitimbi na tamaa kwenye mioyo ya binadamu......

Je ukipata kujua kuwa watoto unaowalea sio wa kwako utachukua hatua gani.......??

Inawezekana majibu yetu yakatoa muongozo kwa Wenzetu wanaopitia haya na wahenga walisema mwenzako akinyolewa na wewe tia maji.......

Karibuni tujadili......!!
Kabla ya kujifundisha kupenda tunatakiwa tujifundishe kumiliki hisia zetu endapo tutasalitiwa kwa sababu usaliti ni jambo linaweza kumkuta mtu yeyote.

Ukishtuka mtoto sio wako mkuu kaa na mkeo kwa peace tu na mpyo safi umuulize mwenye mtoto ni nani,

akishakuambia muonane na mwenye mtoto mzungumze umuulize kwamba ana mipango gani juu ya hao watoto,mwambie wewe hutaki hawa watoto wapate tabuu kwa sababu kila mtoto huja duniani kwa namna yake.

Mtakachokubaliana wewe utaangalia kama kina maslahi na wewe au laa ila hakikisha hauchukui maamuzi yoyote yale ya kumuumiza mama au mtoto.

Hakuna kisasi utakacholiipa kikaendana na thamani uliyoonesha ya kuwajali na kuwalea watoto hao,hivyo hata ukimfanyia ubaya mkeo au mtoto bado hadhi ya wema wako kwa watoto utabaki pale pale na itabaki vile vile kwamba uliwapa thamani watoto ambao sio wako,

sasa kuendeleza thamani hiyo hakikisha hii hali unaihandle vizuri kuonesha kwamba sio tu kwamba unawathamini wanao tu bali hata wasiokuwa wanao kama hao watoto na wengineo uwezo wa kuwathamini unao sana tu.

Thamani ya maisha sio kulipa kisasi kwa waliokukosea,bali ni kusamehe waliokukosea
 
Mimi kama ni watoto 3 au wa 4.. ikatokea mmoja si wangu ntampokea na kumtambua kama mwanangu.

Napenda watoto so sitokua na namna ya kumtelekeza
 
Back
Top Bottom