KikulachoChako
JF-Expert Member
- Jul 21, 2013
- 19,185
- 37,239
Habari za muda huu wapendwa...bila shaka sote tuwazima wa AFYA.
Maisha ya kimapenzi yamejawa changamoto na vitimbi vya kila aina. Mara nyingi wale tuliowapenda na kuwathamini ndio wanaotuletea vunjiko la moyo na maumivu yasiyoisha. Wahenga wanasema kuwa lisemwalo lipo kama halipo laja.
Uaminifu umekuwa jambo adimu kwenye ulimwengu huu uliojawa jeuri, vitimbi na tamaa kwenye mioyo ya binadamu. Je ukipata kujua kuwa watoto unaowalea sio wa kwako utachukua hatua gani?
Inawezekana majibu yetu yakatoa muongozo kwa Wenzetu wanaopitia haya na wahenga walisema mwenzako akinyolewa na wewe tia maji.
Karibuni tujadili......!!