Utachukua uamuzi gani ukigundua watoto uliowalea na kuamini ni wako kumbe sio wako?

Utachukua uamuzi gani ukigundua watoto uliowalea na kuamini ni wako kumbe sio wako?

Busara ni kumtimua bila kumdhuru
busara ni kufuata kile Roho Mtakatifu atakachokuongoza nacho, hata akisema umsamehe ubaki naye ila watoto wajue baba yao ili wasije kuoana na ndugu zao hapo baadaye, unatakiwa kukubaliana nalo. maamuzi mengi watu wanayachukua nje ya Mungu huwa hayana mwisho mwema. kuna kitu tu kizuri alichonacho huyo mwanamke ambacho hata kama alikuwa na makosa, ila kinamfaa huyo jamaa.

watoto wanaonekana walizaliwa miaka mingi, pengine kabla ya ndoa au baada ya ndoa, wakati ule ambao watu ambao hawajaokoka huwa wanakuwa hawana uhakika na mchumba waliye naye na wanakuwa na wachumba wengi, na si ukute huyo mwanamke hakujua kama mimba sio ya huyo jamaa, pengine alitembea nao wote siku za hatari, na ameishi akijua watoto ni wa jamaa. na baada ya kuoana amekuwa mke mwema, kwanini umtimue kwa makosa ya miaka 15 iliyopita?
 
Hii ndio ile hatua wenzetu wa geita, rukwa na iringa huchukua na mara ingine tunaona kama hawapo sawa,

Ukitaka kuona ni zito fanya kama limekutokea afu jipige kifua uamue uone kama utaamua unavyowaamuliaga watu wakitolewa na hilo tukio
 
nawaeleza watoto mimi sio baba yenu. mwambieni mama yenu awapeleke kwa baba yenu akaendeleze kuwalea. nilipowahudumia ndio pamekoma kuanzia leo. na mwanamke namtwanga talaka. mchezo unaisha namna hiyo
Yaani umehudumiq watoto wamekuwa wakubwa hivyo na unawaacha bure?
Hapana mimi lazima nipewe fidia au nibaki nao ila mama yao tubaki kuwasiliana tu mapenzi ndio yataishia hapo
 
mchezaji wa zamani wa Chelsea, Real Madrid na timu ya taifa ya Cameroon 🇨🇲 Geremi Njitap, ametangaza kuvunja ndoa yake na mkewe Laure Fotso, ndoa iliyodumu kwa muda wa miaka 12, baada ya kugundua ya kwamba, watoto wawili mapacha (pichani, wa kike katikati na wa kiume kulia), sio watoto wake.

Utachukua maamuzi gani ukigundua watoto uliowalea na kuamini ni wako, kumbe sio wako?
View attachment 2942848
View attachment 2942852
 

Attachments

  • FB_IMG_1711214617650.jpg
    FB_IMG_1711214617650.jpg
    52.1 KB · Views: 3
Daah yaani watoto walishakuwa hivyo
Na mna muda mrefu kwenye ndoa+uchumba sugu+ uchumba hapo tuseme wana zaidi ya miaka 20 sasa kwa nini muachane? Hapo ni kumsamehe tu na hao watoto kaa kimya usiwaambie watakusaidia baadae ukiwa hauna nguvu.
Hayao ni maamuzi mazito kuliko unavyofikiria na mbaya zaidi Kwa ex husband, na hao watoto kusema kwamba wakusaidie ukiwa huna nguvu omba hekima ya Mungu iwe juu yao na watambue uthamani wako, pia Mama yao awe positive kwao juu ya husband ilihali akijua sio baba yao na afahamu kuwa Mume ameamua kuwa nao sababu anawapenda Sana kama watoto wake wa damu. Inahitaji Moyo mkubwa Sana Sana kuhimili.
 
mchezaji wa zamani wa Chelsea, Real Madrid na timu ya taifa ya Cameroon [emoji1062] Geremi Njitap, ametangaza kuvunja ndoa yake na mkewe Laure Fotso, ndoa iliyodumu kwa muda wa miaka 12, baada ya kugundua ya kwamba, watoto wawili mapacha (pichani, wa kike katikati na wa kiume kulia), sio watoto wake.

Utachukua maamuzi gani ukigundua watoto uliowalea na kuamini ni wako, kumbe sio wako?
View attachment 2942848
View attachment 2942852
kwa upande wangu ntaongea na huyo mke wangu ili hiyo siri isitoke,tulee watoto basi
 
mchezaji wa zamani wa Chelsea, Real Madrid na timu ya taifa ya Cameroon 🇨🇲 Geremi Njitap, ametangaza kuvunja ndoa yake na mkewe Laure Fotso, ndoa iliyodumu kwa muda wa miaka 12, baada ya kugundua ya kwamba, watoto wawili mapacha (pichani, wa kike katikati na wa kiume kulia), sio watoto wake.

Utachukua maamuzi gani ukigundua watoto uliowalea na kuamini ni wako, kumbe sio wako?
View attachment 2942848
View attachment 2942852
Angemsamehe tuuu.

Natania😎
 
Twins’ True Origins: The truth emerged after a paternity test, which shattered Geremi Njitap’s long-held belief that the twins were his offspring. Instead, they are the biological children of his wife’s previous husband. The weight of this revelation has left the former football icon grappling with a mix of emotions – betrayal, shock, and disbelief.
Faida ya kuoa single mother,anaeendelea kuonana na mzazi mwenzake.
 
l
Yaani umehudumiq watoto wamekuwa wakubwa hivyo na unawaacha bure?
Hapana mimi lazima nipewe fidia au nibaki nao ila mama yao tubaki kuwasiliana tu mapenzi ndio yataishia hapo
hata ukiwatosa, jua mtoto wako ambaye amezaliwa mama mmoja nao, hatawaacha, na atakuheshimu sana kama utawathamini watoto alionyonya nao ziwa moja. ugomvi ubaki wa wewe na mama, ila watoto wabaki na furaha na amani. pia, hata mama yao, kwa story hii, inaonyesha watoto hao walizaliwa kabla hawajaoana, ndoa ina miaka 12 wao wana miaka 15, hivyo walizaliwa kwenye kipindi ambacho walikuwa wachumba tu, hawakuwa kwenye ndoa. sihalalishi uzinzi ila nadhani ni busara kwake hao watoto aendelee kuwapenda kama alivyojenga upendo kwa miaka yote hiyo, ila baba yao apatikane ili wajue biological father, wanakujaga kuoana ndugu ukifanya mchezo.

pia, kwa mama, hilo ni kosa kabla ya commitment ya ndoa, asimhukumu kwa makosa ya kabla ya ndoa ambayo hata yeye si ukute ni kwasababu tu ni mwanaume angekuwa anashika mimba angeshakuwa na watoto wa nje kwasababu kama hakuwa anacheat huko aliko awe wa kwanza kurusha jiwe. ugumu unakuja tu pale mkeo uliyeishi naye miaka yote hiyo anapotakiwa akabiliane na aibu, ila linatakiw akuwa hivyo kwa muda mfupi na wakubaliane kuendelea na ndoa regardless of that. ni sawa na mtu umetenda dhambi, unatubu, na katika kutubu kuna aibu utaenda kukumbana nayo, hivyo unasema as long as nitasamehewa dhambi yangu, niko tayari kukabiliana na aibu hii. then maisha yataendelea.

mimi nilishakuwa mzinzi sana hata kwenye ndoa, kabla ya kukabidhi maisha yangu rasmi kwa Yesu. nilipokuja kuamua kusalenda, nilikubaliana na aibu zote, matusi yote hata kwa watu walioniheshimu as long as nimesamehewa dhambi zangu, na huwa naweka wazi tu ili iwe fundisho kwa wengine, nawaeleza madhara ya uzinzi kwenye ndoa na mengi mazito niliyopitia kutokana na dhambi.
 
Back
Top Bottom