UTAFITI: 55% ya wananchi wanaukubali utendaji wa Rais Magufuli 2018 toka 96% ya 2016

UTAFITI: 55% ya wananchi wanaukubali utendaji wa Rais Magufuli 2018 toka 96% ya 2016

Tunaelekea kuzuri. Lazima watu waliopofushwa akili ziwarudi. Tuendelee kuliombea taifa, tuko kwenye raiti trak.
 
SIKILIZENI NIWAMBIE, WALA MSIPIGE VIGELEGELE KUHUSI HAWA TWAWEZA ..AMIN NAWAMBIA TWAWEZA NISEHEM YA UTAWALA HUU ..HAWA WATU WANATUMIKA SANA.

KWA TAARIFA YENU, MUWE MNATUNZA KUMBUKUMBU VZURI, , TWAWEZA HUWA WANATOA UTAFITI WAO EITHER KUFUNIKA JAMBO FULAN LILOTOKEA MUDA MFUPI AU KUNA JAMBO LINALOENDELEA ...SASA LENGO LA TWAWEZA HUA NI KUBADILI MAZUNGUMZO YANAYOTREND NDANI YAJAMII.

SIKILIZENI MSISAHAU PETROL IMEPENDA BEI , MSISAHAU YANAYOENDELEA YA MWIGULU BASIII ..

MKIKALIA YA TWAWEZA, AMINN UTAFIT UJAO UTAONYESHA WANAOMKUBALI MKUU NI 82% .

Hawana maana hao.
 
Tena nafikiri huu utafiti ukifanyika hivi sasa..jpm yupo chini ya 40% kwenye kukubalika utendaji wake..
Uzuri hili hata yeye analifahamu..
Nchi inaongozwa na mwehu.
Ndio maana jana kawaita wazee? mnajua utafiti huo ni watanzania hao! kwa hiyo inahusisha hata mabaka mabaka
 
Tunataka kuiambia Serikali wasiwatishe wananchi, kawaambia wananchi kua watawapiga kipigo cha Mbwa Koko, wananchi hawaogopi ni 18% tu ndiyo wanaogopa kipigo cha Mbwa Koko, wananchi wanataka haki na nimwambie tu ndugu yangu Polepole endeleeni tu- Fatma Karume Rais Wa TLS [HASHTAG]#KwnzaHabari[/HASHTAG]
 
TAMKO LA MALI - ZITTO TWAWEZA.jpg


Swali #8 item namba 3 inaonyesha ZITTO ana mkataba wa ushauri na TWAWEZA, unategemea data zitakuwaje kama sio za kupika! Na hiyo ni fomu ya tamko la raslimali na madeni.
 
Watafiti waliuliza swali gani? Kwa kuzingatia utambuzi na maoni ya wachangiaji wakuu, pengine kama ilivyokuwa kwa waandaaji, the entire thing seems to be a cooked story!
 
Uwe utafiti wa kwel au wa uongo ila jambo la msingi ni kuwa kunakushuka, tazama ratio 96-71=25, mwaka 2016
71-55=16 mwaka 2017
55-( )=? Mwaka 2018

Kwa takwim hizi kunakupolomoka kwa ccm na serikali,

Ukiwa baba bora, hutakasirika ikiwa mtoto wako anaonesha kufel, la maana utakachofanya ni kuyakubali matokeo na kutafuta mbinu ya kumsaidia mtoto asiendelee kufeli...

Wito kwa serikali, wafanyie kazi utafiti huu..wachukulie +v altitude zaidi kuliko -v

Wananchi wanamalalamiko mengi miyoni mwao, na hakuna lugha sahihi ya kuwaambia zaidi ya kuwapa kile ambacho kitawapa mkate wao, sio takwimu
 
Rais wetu alishasema hakwenda Ikulu kutafuta umaarufu

Alikwenda ikulu kutafuta maendeleo, ambayo kimsingi yanakuja, shida kubwa ninamna ambavyo yanakuja,

Hebu tafakali, kwa sasa, secta binafsi ambayo ilikuwa mbiya(partinalship) na serikal wamewaita wezi na kuwaondoa kabisa, isipokuwa kwa wajenzi pekee,

Unatalajia utafika vipi juuu bila kupanda ngazi? makampuni binafsi yaliyotaraji kupata kazi toka 2016 yameacha kazi, yamekuwa jobless, hao watz waliokuwa wanapata mkate kwa kupitia hayo makampun nao ni jobless,

Haya maendeleo yatakuja vp? Na kwa kufanya kazi ipi? Huko mikoani ndo balaa samaki hawauziki, ukikutwa nao ni kama bangi, kusin huko miladi yote imesimama.

Unahitaji utafiti upi kujua maisha nimagum?
 
Haya matokeo yamekuwa more reliable na sina uhakika kama prof kitila bado ni mjumbe wa hii taasisi
 
Maswali ya amani na uhuru wa wananchi hayapaswi kujibiwa kwa hoja za mkate, hii ni busara kubwa, kina Gadafi, sadam nk waliweka mikate mezani watu wakachagua uhuru, wakina Mugabe walifikiri wanapendwa sana watu waliposherehekea kuondoka kwake akapigwa na butwaa! Kamwe uhuru wangu siwezi kubadilishana na sgr au sg, kama alivyosema Nyerere, heri maskini huru kuliko tajiri mtumwa! Hivi kama wanapendwa kweli, si wako wengi bungeni? wabadili basi sheria ya uchaguzi ili refa wakicheza Simba na Yanga refa asitoke Yanga atoke chama cha marefa!
 
Ahsante Jenerali Ulimwengu kwa kusema ukweli japo ni mchungu kwa walio wengi ambao wamezoea kupindisha ukweli waonekane eti wazalendo.Yapo mambo ya msingi ambayo yanapaswa kufanyiwa kazi ili taifa lisonge mbele na wale wanaoyasema mambo hayo kwa uwazi wasichukuliwe kama wasaliti huku wengine wakipotezwa kabisa na wengine wakinusurika vifo tena vya risasi!
 
Back
Top Bottom