Umaarufu ndani ya mipaka ya TZ au hadi nje ya mipaka?
Maana ukitazama waliotajwa hapa wote mbinu zao za kuteka soko la muziki zilikuwa/zipo tofauti...
Nature aliimba muziki unaojali watu wa mtaani zaidi na kidogo maisha halisi ya watanzania, muziki wake ulichagizwa na vijimaneno maneno vinavyoweza kujulikana na watu wa mtaani, na ndio ilikuwa wakati sahihi maana bongo flavor ilipendwa zaidi na watu wa rika la katikati.
Ukiacha hilo, Nature alipata kushiriki nyimbo nyingi sana na zote zilikuwa moto kiasi kwamba huwezi choka kumsikiza...
Mr Nice yeye sio tu kuwa aliimba muziki bali alikuja na style yake pekee ya muziki ambayo aliipa jina la Takeu, muziki wake ulitoka nje ya Tanzania lakini ukaishia nchi zinazoizunguka Tanzania...
Alikiba huyu utamu wa sauti yake, simulizi katika nyimbo zake ulifanya apendwe Tanzania na nchi zinazoizunguka Tanzania, wakati akiwa kileleni muziki wa bongo flavor haukuwa ukijulikana sana duniani, na hata wakati ulipoanza kujulikana huyu bwana ni kama alikuwa kwenye likizo ya utunzi na uimbaji...
Diamond huyu bwana mdogo uwezo wake wa kuimba simulizi za mapenzi kwa namna ya kulalamika ulimfanya awe na namna ya pekee kugusa mashabiki zake na ndio umaarufu wake ndani ya mipaka ya mashariki ya Afrika ulipoanza.
Kitu kingine alichoweza kukifanya Diamond ni kuamua mapema sana kuufanya muziki wake uwe biashara na si burudani pekee, aliamua awekeze katika muziki na kuthubutu kujaribu kwenda nje ya mipaka kuzidi walipofika waliomtangulia.
Kwa kifupi Diamond umaarufu wake ni mchanganyiko wa vitu vingi sana na binafsi naona ndiye kijana aliyefanikiwa sana kujulikana nje ya mipaka ya Afrika na hata duniani kwa ujumla