Bila ya Legacy ya akina Sugu,Prof Jay na baadae kizazi cha kati kikiwa na akina Nature,Jay Mo, King Crazy GK, Mwana FA na wengine wengi,hao akina Mond,Harmonize si lolote si chochote. Washukuriwe waliopambana hadi Bongo Flavor kukubalika. Miaka ile,huu muziki ulionekana na uhuni mtupu,lakini waanzilishi hao walipambana hadi ukaanza kujulikana kwa jamii. Lakini pia miaka hiyo yaani 1999 kurudi nyuma hakukua na media wala Whatsapp,Instagram wala chochote,hivyo ilikua ni vigumu sana kupata milage kimataifa,hongera kwa Technology,nje ya hapo hakuna mtu angemjua Mondi wala Haramonize wala nani kwa level rahisi kama ilivyo sasa. Na ndiyo maana wazee wetu wa Muziki wa Dansi,wamekufa wakiwa na maisha ya kawaida kwa wengi wao,ila vipaji vyao huwezi kufananisha hizi porojo na kelele za sasa ambazo muziki wake wimbo ukitolewa leo,baada ya mwezi mmoja unakosa mvuto. Bila kuathiri na kutaja jina,mfano huu wimbo mpya uliotoka,hivi una chochote cha maana?
Uno,Babalao na hata Mshumaa,ni nyimbo za miez 3 au 4 baada ya hapo hamna kitu,zote zinasahaulika,ni kwa sababu hazina maudhui yoyote,tena afadhali Mshumaa,angalau una maudhui yanayoishi,hizo zingine ni burudani fupi,ambazo expiry date yake haiwezi kuzidi miezi 6