Extrovert
JF-Expert Member
- Feb 29, 2016
- 70,785
- 186,690
Criteria ya kwanza mke lazma awe caring partner na sio kama mpangaji mwenzio kwenye nyumba. Maana tabia za wapangaji tunazijua wazi.Hii mindset ya wanawake nayo kwa kiasi kikubwa inachangia tatizo, wengi wao hupigania kuolewa wakiamini kwenda kwa mume ni sawa na kwenda kwa "baba zao wadogo", wanakwenda kutafuta malezi mengine nje ya nyumbani kwao walipozaliwa.
Hapa ndio chanzo cha wale jamaa wa kataa ndoa wanapopata nafasi ya kujidai, wanawake wanakuwa wagumu sana (baadhi) kutoa sehemu ya kipato chao kurekebisha mambo nyumbani pale hali inapoyumba, na hata wakitoa, basi ujue utasemwa mpaka ujute.
Mwanaume akiamua kuishi na mwanamke kwenye hizi ndoa zetu, simply hatakiwi kuwa na kisirani, hatakiwi kujiuliza maswali, akae akijua anatakiwa kutoa pesa non stop kila zitakapohitajika, na kama ikitokea akakosa bahati mbaya, ajiandae kwa lawama, sasa ni wangapi wenye uwezo wa kuvumilia hizo lawama?!
Kabla ya kuoa lazma uwe umeng'amua hio element kwa mkeo mtarajiwa. Je, ni mtoaji au ndio ana mkono wa birika?
Mwanamke mbinafsi hawez kuwa mke mzuri hata siku moja go east go west na ndoa za vijana wa kileo zitavunjika sana tu kwa sababu hio ya mmoja kumfanya mwenzie kama punda.