Utafiti: Profesa Janabi yupo sahihi 100%; watu wanajiua wenyewe kwa upumbavu wao

Utafiti: Profesa Janabi yupo sahihi 100%; watu wanajiua wenyewe kwa upumbavu wao

Kwa staili ya ulaji kama huu kwanini mtu asife mapema? Unategemea nini kutoka kwa mtu mpumbavu kama huyu? Si ameamua kujiua mwenyewe kwa makusudi?
Itungwe sheria inayofanana na wale wanaokunywa sumu au kujipiga risasi ili wafe
 
Kuna wale wa dini ile wanategemea mwezi wao wa kuacha kula mchana lakini jioni wanafakamia misosi ya ajabuajabu ambayo bado tu inawanenepesha. Huku kwenye mawaidha yao hujisifu kuwa wakifunga kula wataepukana na hayo maradhi. Kama mtu unaona ukila vyakula fulani unafura mwili ni bora kuviacha, kula michemsho isiyo na chumvi/sukari ku maintain body
 
1704284242876.png

Mswahili anasema akila pilau akanywa pepsi anaongeza speed ya digestion ili usiku ale vizuri zaidi
 

Attachments

  • 1704284243089.png
    1704284243089.png
    45.4 KB · Views: 3
Chini ya ccm hakika watanzania tunapigika
mbona Sugu, Msigwa, Lema, Mdee, Zitto, Bulaya, Mnyika wote walizaliwa mafukara lakini wakatajirika ndani ya utawala wa CCM?

Hata Mayor Jacob biashara yake ya Mayai imeshamiri kutokana na mazingira wezeshi ya Chama cha Mapinduzi

cha msingi kama unataka unyevu nyevu simama kwny mfereji unaotiririsha maji mwaka mzima

pambana ingia kwny Central commitee ya Chama chako, mkiishiwa mnapiga press conference mbili tatu Msajili wa Vyama Jaji Mutungi anaitwa anaelekezwa aachie mafungu ya ruzuku Makamanda mnaanzisha heka heka za Helcopter mnatingisha kwa madai ya Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi na mkishapata justifications mnatafuna chenji na mnaendelea na uwekezaji kama kawaida

Mzee Slaa alikimbia mafuriko ya mferejini sasa hivi anakufa kwa kiu ya maji huko mlimani

Sent from my SM-G9500 using JamiiForums mobile app
 
Unajuaje yuko sahihi kwa 100% na si 99% wala 98%?

Godel's Incompleteness Theorems zinakataa sayansi yenye uhakika wa 100%.

Mambo mengi anayoyasema Janabi bado yanafanyiwa uchunguzi. There are known unknowns. Utasemaje Janabi yuko sahihi kwa 100%?

Umefanya assumption gani? Una margin of error gani?

Janabi ana makosa kwenye presentation, si kwenye substance.

Kama wewe unavyokuwa na makosa hayo hayo ya presentation.

Kuna suala la usomi na utamaduni.

Watanzania wengi hata tukipata usomi, kubadili utamaduni ni kazi.

Kwa mfano, utamaduni wa kuwa unnecessarily dramatic umekufanya utoe asilimia katika jambo ambalo tukijikita kuihakiki hiyo asilimia, huwezi kuitetea.

Ingekuwa uko katika comedy show, ningejua unatumia comedic license for effect. But, this is science. There is no such license in science.

Unatoa asilimia 100% kiasi kwamba, mtu akitaka kuifanya hiyo asilimia iwe distraction, anafanya hivyo kirahisi tu.

Message yako ya muhimu kabisa inapotea. Watu wanakuona alarmist.

Mistake hiyo hiyo unayofanya wewe, ndiyo hiyo hiyo anayofanya Janabi.
Mkuu hiyo asilimia imejikita kwenye population sample niliyofanyia utafiti. Sample yote niliyoitafiti iliangukia kwenye obesity. Kwanini upinge wakati mimi ndiye niliyefanya utafiti?

Kumbuka utafiti haupingwi kwa maneno matupu bali hupingwa kwa utafiti kinzani. Kama unataka kuni prove wrong, nenda kafanye utafiti kinzani sio porojo.
 
Mkuu hiyo asilimia imejikita kwenye population sample niliyofanyia utafiti. Sample yote niliyoitafiti iliangukia kwenye obesity. Kwanini upinge wakati mimi ndiye niliyefanya utafiti?

Kumbuka utafiti haupingwi kwa maneno matupu bali hupingwa kwa utafiti kinzani. Kama unataka kuni prove wrong, nenda kafanye utafiti kinzani sio porojo.
Population sample ndiyo inathibitisha Janabi yupo sawa 100%?

100% umeipata kwa population sample kivipi? Watanzania 100% wanakufa kwa kula ovyo?

Population sample inathibitisha Janabi hakosei hata neno moja?

Unaelewa 100% ni nini wewe?

Nimekuuliza assumptions zako na margin of error, kwa nini hujajibu?
 
Babu yangu alikua hapendi kabisa kusikia haya mambo.

Hakuna siku aliacha kugida soda au bia, kama yupo kwenye dozi au mfungo atagida soda.
Siku nyingine ni bia.

Aliishi miaka 70+.
 
Urithi wa uzima wa milele. Maana yake unakufa kwanza ndio baada ya kufufuka unaurithi huo uzima ukiwa umekidhi viwango.
Biblia haiongei uwongo, uzima wa milele ni kuishi milele bila kuonja mauti.

Wapo ambao ahadi yao ni ufufuo, na wapo ambao wataishi milele.
Je unajua Yesu anakuja lini?

Je akija sasa hivi, na matendo yako yakiwa mema, utaishi milele au itabidi ufe kwanza?

Ndio maana alisema kama anavyopaa ndivyo atakavyorudi, na kila jicho litamwona.

Hapo wapo wale wa moto wa milele (bila kuonja mauti) na sisi wa uzima wa milele (bila kuonja mauti)
 
Babu yangu alikua hapendi kabisa kusikia haya mambo.

Hakuna siku aliacha kugida soda au bia, kama yupo kwenye dozi au mfungo atagida soda.
Siku nyingine ni bia.

Aliishi miaka 70+.
Mkuu,

Hata kama angeishi miaka 20 tu, kama alielewa kuwa akilewa kila siku atakufa na miaka 20, ni haki yake tu.

Kwanza, si kila mtu anataka kuishi maisha marefu.

Wengine wanamazingira, wanaona kuishi maisha marefu ni ubinafsi na kuharibu mazingira.

Wanataka waishi maisha mafupi, matamu.

Sasa hao nao utawalazimisha waishi maisha marefu bila wao kutaka?
 
Mkuu,

Hata kama angeishi miaka 20 tu, kama alielewa kuwa akilewa kila siku atakufa na miaka 20, ni haki yake tu.

Kwanza, si kila mtu anataka kuishi maisha marefu.

Wengine wanamazingira, wanaona kuishi maisha marefu ni ubinafsi na kuharibu mazingira.

Wanataka waishi maisha mafupi, matamu.

Sasa hao nao utawalazimisha waishi maisha marefu bila wao kutaka?
Binadamu wote wakiwa katika utimamu wa akili na afya njema wanataka kuishi maisha marefu, vinginevyo labda walio katika mateso makali, ufukara uliokithiri au magaidi wa kujitoa mhanga.
 
Binadamu wote wakiwa katika utimamu wa akili na afya njema wanataka kuishi maisha marefu, vinginevyo labda walio katika mateso makali, ufukara uliokithiri au magaidi wa kujitoa mhanga.
Hapana,

Kuna watu wamesoma sana, washaona maisha hayana maana.

Ukijinyima kula, ukila sana, utakufa tu.

Na unaweza kujinyima kula unavyotaka, ukataka kuishi maisha marefu, ukapata ajali na kufa kesho yake.

Na hata ukifanya nini, hata ukiishi maisha marefu, most likely wewe na kazi zako zote zitasaulika baada ya vizazi vichache tu.

Mimi nina rafikibyangu alikuwa profesa, kaandika a very rare atlas yake, from scratch. Kafanya kazi miaka 20 kuitengeneza hiyo atlas. Sasa hivi hajafikisha hata miaka 10 tangu afe, hakuna mtu anayeifungua hiyo atlas.

Na ulimwengu wote unakongoroka.

Sasa hivi watu wanapigana kutafuta dawa za antibiotics, ambazo eventually, in less than 50 years, zote zita fail kutokana na antibiotic resistance. It's a rat race.

Mwishowe jua litapasuka kwa supernovae na kuiunguza dunia yote.

Na hata ikiwezekana kufanya interstellar travel, you cannot escape the heat death of the universe.

Sasa, ndiyo maana watu wengine wanafikiria sana maisha na kuona kila kitu ni ubatili mtupu.

Sasa, mtu akishajionea hivyo, akaamua kufurahia maisha yake anavyotaka yeye, kula anavyotaka, kunywa anavyotaka, maisha yake yawe mafupi na matamu, afanye anachotaka yeye, afe siku yoyote, tatizo liko wapi?

Mtu anakuuliza, kwa nini aishi maisha marefu ikiwa vile vitu anavyopenda kufanya, vile ambavyo anaona vinayapa maisha utamu, anakatazwa kufanya?

Urefu wa hayo maisha utakuwa na maana gani? Urefu wa hayo maisha utakuwa na tofauti gani na kifungo kirefu katika gereza asilolipenda?
 
Kweli watu wanahitaji elimu sana kwenye lishe bora, siku hizi vyakula vingi tunavyotumia sio balanced diet.

Mijini imekuwa fashion siku hizi kuku wa kukaanga na mishikazi ya kukaanga na chips mafuta yanayotumika pamoja na kuwa low quality yanakuwa overused mpaka yanakuwa meusi sana.

Haina ya chakula hii na zege kwa afya ya moyo na mishipa ya damu ni vibaya sana na wengi wanatumia kila siku.

Tunatengeneza taifa la vijana ambao wanapata magonjwa yasiyoambukiza na ghali sana kuyatibu.

Bado tuna vyakula vya asili vingi tu lakini elimu ya chakula bora wengi hawana kabisa.

Wadau husika inabidi wastage intervention mapema kabla hali haijawa mbaya sana.
1704293602991.png
 
Ila Wakuu magonjwa ya kushindwa kufanya kazi kwa viungo vya mwili yameongezeka sana. Na sisi tumebweteka kwelii. Hakuna mazoezi hakuna kutembea. Ni mashindano ya vitambi tu wake kwa waume.
 
Back
Top Bottom