Azarel
JF-Expert Member
- Aug 25, 2016
- 28,916
- 40,479
Tatizo lako wewe unajikuta Mjuaji sana na kuona kama wengine hawajui chochote,Naamini 95% hawatakuelewa kwa ujinga wao na watajifanya wanaelewa sana na wataleta hoja za kijinga mradi wakupinge na kujifanya wao wanajuwa kumbe hawajuwi.
Niliwahi kuandika hivi kuhusu Watanzania:
Tanzania tuna Adui mmoja tu, Ujinga, nyingine zote ni porojo za ujinga wetu tu
Hili la adui ujinga nimeliandika mara nyingi hapa JF kwenye posts tofauti. Kwa miaka mingi sasa huwa nauliza na kujiuliza "hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?" Kuuliza kwangu siyo kwa kukisia au kwa kebehi au kejeli, ni swali la ukweli kabisa. Kilichonisukuma kuandika haya, ni yote...www.jamiiforums.com
U have Prejudice & Pride
Ulisema Tanzania tuna Adui mmoja tu yaani Ujinga na hatuna Adui Umasikini wala Maradhi kitu ambacho ni UONGO
Maradhi na Umasikini na Adui wakubwa katika nchi za dunia ya tatu
Halafu ukasema Maradhi na Umasikini ni matokeo ya Ujinga kitu ambacho sio kweli kwa 100%
Umasikini unaweza kuwa ni matokeo ya Ujinga endapo tuna rasilimali na hatuzitumii ipasavyo au tunaendekeza rushwa
Lakini MARADHI sio tokeo la Ujinga, kwasababu hata nchi zilizoendelea zisizo na Wajinga wengi zina Maradhi
Kwa Mfano, unaweza kusema COVID 19 ilisababishwa na UJINGA? haikuathiri zaidi nchi zisizo na Wajinga wengi na zenye werevu?