Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha ubia nchini Tanzania PPPC Bwana David Kafulila akihojiwa katika kituo cha ITV kwenye kipindi cha DK 45 amesema yafuatayo namkuu,
" Kwanza ni kweli kwamba umasikini Tanzania haujaisha ila ni kweli kwamba Tanzania Umasikini Umepungua sana hapa hoja ni umasikini huu Umepungua kwa njia gani au kwa kiasi gani.
Anarejea ripoti ya Utafiti ya REPOA ya mwaka 2006 inayosema kama nchi ya Tanzania itawekeza kwenye sekta ya kilimo na Sekta hiyo ikakua walau kwa 10% tu kwa miaka mitatu mfululizo basi itapunguza umasikini kwa Watanzania wote Kwa 50%
Anaendeleaje kwa kusema Kukuza uchumi vijijini ni kuwekeza kwenye kilimo katika dhana pana, miundombinu ya maji, umeme, barabara na huduma za msingi kama elimu na afya takwimu zinaonesha mapinduzi makubwa maeneo yote hayo tumefanya vizuri sana, hakika kazi kubwa imefanywa na awamu ya sita alisema,
Kafulila anasema uwekezaji wa mbole kutoka tani laki tano hadi tani Milioni moja na laki mbili Wakati huo huo bajeti ya kilimo imeongezeka karibu mara tano zaidi, Bajeti ya Barabara TARURA vijijini nayo imeongezeka mara tano zaidi, Umeme vijiji umeongezeka kutoka vijiji elfu 10 mpaka vijijini elfu 12 haiwezakani mambo haya yote yafanyike na pasiwepo mabadiliko yoyote ya kiuchumi Kwa Watanzania hilo haiwezekani.
Kafulila anaendelea Kwa kusema inawezekana tatizo la Umasikini Tanzania ni kweli halijaisha ila ni kweli pia kwamba tatizo la Umasikini Tanzania limepungua kwa kiasi kikubwa sana hasa kwenye miaka minne ya awamu hii ya sita (6) ya Mama Samia Suluhu Hassan" alisema.
View attachment 3356631
===