UTAFITI: Tukikikuza kilimo kwa 10% tu tutafuta umasikini wa Watanzania kwa 50%- David Kafulila

UTAFITI: Tukikikuza kilimo kwa 10% tu tutafuta umasikini wa Watanzania kwa 50%- David Kafulila

Hawa watu muda wote ni maneno marefu kama mnyororo. Ndiyo anajua hili leo? Mbona hili limeshasemwa miaka 40 iliyopita lakini kwa sababu watawala wetu ni watu wanafanya kazi kwa maneno kama alivyo huyu jamaa, hakuna utekelezaji.
🤓🤓
 
huyu jamaa manenoo mengi
Huo wimbo ushaimbwa sana
Utekelezaji sasa

Ova
 
Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha ubia nchini Tanzania PPPC Bwana David Kafulila akihojiwa katika kituo cha ITV kwenye kipindi cha DK 45 amesema yafuatayo namkuu,

" Kwanza ni kweli kwamba umasikini Tanzania haujaisha ila ni kweli kwamba Tanzania Umasikini Umepungua sana hasa awamu ya sita hapa hoja ni umasikini huu Umepungua kwa njia gani au kwa kiasi gani.

Anarejea ripoti ya Utafiti ya REPOA ya mwaka 2006 inayosema kama nchi ya Tanzania itawekeza kwenye sekta ya kilimo na Sekta hiyo ikakua walau kwa 10% tu kwa miaka mitatu mfululizo basi itapunguza umasikini kwa Watanzania wote Kwa 50%

Anaendeleaje kwa kusema Kukuza uchumi vijijini ni kuwekeza kwenye kilimo katika dhana pana, miundombinu ya maji, umeme, barabara na huduma za msingi kama elimu na afya takwimu zinaonesha mapinduzi makubwa maeneo yote hayo tumefanya vizuri sana, hakika kazi kubwa imefanywa na awamu ya sita alisema,

Kafulila anasema uwekezaji wa mbole kutoka tani laki tano hadi tani Milioni moja na laki mbili Wakati huo huo bajeti ya kilimo imeongezeka karibu mara tano zaidi, Bajeti ya Barabara TARURA vijijini nayo imeongezeka mara tano zaidi, Umeme vijiji umeongezeka kutoka vijiji elfu 10 mpaka vijijini elfu 12 haiwezakani mambo haya yote yafanyike na pasiwepo mabadiliko yoyote ya kiuchumi Kwa Watanzania hilo haiwezekani anasisitiza Kafulila.

Kafulila anaendelea Kwa kusema inawezekana tatizo la Umasikini Tanzania ni kweli halijaisha ila ni kweli pia kwamba tatizo la Umasikini Tanzania limepungua kwa kiasi kikubwa sana hasa kwenye miaka minne ya awamu hii ya sita (6) ya Mama Samia Suluhu Hassan" alisema.

===

Ameongea mengi zaidi msikilize hapa chini.
View attachment 3356631

===
Huyu sidhani kama anajua lolote, anasifia tu siku zote.
 
Najua vitu vinavyosaidia Nchi kuendelea upo mwaka Tanzania waliweka 18% VAT kwenye transit goods niliwahi kumpigia simu Waziri wa Fedha kipindi hicho alikua Mpango nadhani kumwambia Wazambia wameikimbia bandari yetu kisa hayo mambo ya VAT kwenye mizigo yao na Wakongo wengi walikua wanatoa mizigo yao kupitia Durban na Mozambique yule mzee ni msikivu sana alifanya research akaja na majibu sahihi na baadae wakaondoa hiyo VAT na kuwafata Wazambia tena na kuendelea na mshkamano wao tena sisi tupo huku kwenye kazi za usafirishaji tunaona wanavyolalamika wateja kwa hiyo ni rahisi kuwafikishia viongozi wetu ambao ni wasikivu kwa wananchi..
Yule mzee anajielewa sana, ndio maana ameamua kustaafu kuliko kufanya kazi na hawa wahuni wanaogawa baskeli na kuteka watu
 
David Kafulila tangu ameingia PPP iliyoanza tangu wakati wa JK mwaka 2009, lakn mabadiliko na mjadala wa PPP nikama vile imeanza na Kafulila. Mwamko wa Umma, Serikali na Sekta Binafsi sasa ni PPP ndio habari nzima.
 
Mimi Kafulila nakumbuka akiwa Mkuu wa Mkoa Simiyu mkoa ambao zaidi ya asilimia 60% ya pamba inazalishwa huko, mbali na kusimamia uwajibikaji watendaji wa serikali alianzisha mfumo wa ununuzi wa pamba maarufu kama Simiyu cotton model ambao ulidhibiti wizi wa ushirika kwa kuwaondolea monopoly ktk ununuzi wa pamba na kufanya ununuzi kuwa huria kwa mkulima kuuzia ama ushirika au wanunuzi binafsi, uamuzi uliosababisha bei ya pamba kufikia 2000/= kwa kilo, bei ambayo haikuwahi kufikiwa ktk historia ya pamba ...
 
Yule mzee anajielewa sana, ndio maana ameamua kustaafu kuliko kufanya kazi na hawa wahuni wanaogawa baskeli na kuteka watu
Sasa huyu jamaa etu amekuja na kodi ya hela ikikaa bank aisee si hatari hii anajua madhara yake si anawafukuza wateja wa bank kuweka hela bank na watu waanze kukabana tena kama zamani sijui wenzetu shule zao walisomea wapi aisee badala ya kuhamasisha watu watunze fedha bank na wasibebe hela yeye anawatoa bank kiarhisi kwa kupandikiza kodi ya kijinga kabisa ili wapate fedha nyingi za kuiba ambazo CAG akisema pana wizi hakuna kinachotokea..
 
Kwani kilichomfanya mzee astaafu ni hicho?
 
Back
Top Bottom