Utafutaji wa kiwanja umenifanya nielewe mwanadamu ni hatari sana

Usinunue eneo bila kuwajua majirani zako wanne wakikupa taarifa zisizofanana acha usinunue hakikisha taarifa zao zinafanana juu ya umiliki wa eneo husika.
Pia mtu akikuuzia eneo akupe dhamana isiyohamishika mfano nyumba ili kesho ikienda tofaut Hela yako iwe salama.
 
Ni kwamba maeneo hayo thamani ya shamba heka moja ni kati ya laki 5 hadi 1.5milion.

Eka moja ina viwanja zaidi ya kumi ila havizidi 12.

Kwa hiyo, muuzaji ananunua/alinunua eka let say laki 5 na akapima viwanja 10+ vya ukubwa wa 20x20 na anauza Tsh 250,000/=.

Kwa harakaharaka 250,000x10=2,500,000. Kwa hiyo ni biashara yenye faida kwao na ni halisi.

Changamoto ni kwamba pako mbali na mji na kama iwapo mtu una pesa na ukapata muuzaji mwaminifu basi unaweza ukanunua shamba tu ambapo laki 7 unapata heka.

Hapa nipo njiani naenda Vigwaza kuchukua hati ya shamba eka 2 nilinunua milion moja (nilikuwa ninalipia kidogo kidogo laki 2.5 kwa mwezi.

Wezi wapo ila pia wa kweli wapo.
Nzuri hii mkuu. Shukrani kwa taarifa.
 
Akili ya kutafuta viwanja siyo lazima wakili ambaye ni zao la bookish Schools.

Wakili naye anatafuta chakula tena kwa gharama zilizo juu na ufanisi zero
This is called fallacy of generalization.

Tupo Mawakili wadogo, brilliant and hard-working. Tumeandika na machapisho kadhaa ya vitabu na vijarida. Shida yenu mnatega masikio na kukodoa macho kwa hao Mawakili wanaopenda kumulikwa na makamera.

You have proved to be one of those 'wajuaji' ambao mkishapigwa mnakuja kulialia humu.

Nyie ndio ambao joto la mwili likipanda kodogo mnaenda kununua dawa za malaria badala ya kuwaona wataalamu wa afya. Jifunze kuheshimu taaluma za watu, hata hivyo sijamlazimisha mtu kwenda kwa Wakili, nimetoa ushauri tu ili kupunguza vilio vya namna hii vinavyotujazia saver.

Rubbish!
 
Kuna Umuhimu sana wa kuwa na Hati miliki kutoka wizarani kwa kiwanja unacho miliki
Watu wengi wamezoea kununua viwanja kizamani ,ile ya kwenda kwa m/kiti au mjumbe kusainishana haitoshi inabidi watu wajiongeze
.kwa Kila kiwanja unachotaka kununua uhakikishe

Kimepimwa

Kuna ramani ya mipango mji eneo husika

Ikitokea unauziwa na mtu binafsi ni muhimu sana hicho kiwanja kiwe na Hati miliki kutoka wizarani ,kama hakina hiyo aliyekuuzia akupe ushirkiano kufanya mchakato wa Hati miliki ya wizarani

Note:
Ni muhimu sana
Asante sana mkuu
 
This is called fallacy of generalization.

Tupo Mawakili wadogo, brilliant and hard-working. Tumeandika na machapisho kadhaa ya vitabu na vijarida. Shida yenu mnatega masikio na kukodoa macho kwa hao Mawakili wanaopenda kumulikwa na makamera.

You have proved to be one of those 'wajuaji' ambao mkishapigwa mnakuja kulialia humu.

Nyie ndio ambao joto la mwili likipanda kodogo mnaenda kununua dawa za malaria badala ya kuwaona wataalamu wa afya. Jifunze kuheshimu taaluma za watu, hata hivyo sijamlazimisha mtu kwenda kwa Wakili, nimetoa ushauri tu ili kupunguza vilio vya namna hii vinavyotujazia saver.

Rubbish!
Mimi mwenyewe Mwanasheriaa. Sasa nije kwako kufata nini? Nini nisichokijua kuhusu Conveyance?
 
Kuna hivi vinavyotangazwa kila kukicha kwenye maredio vinapatikana mlandizi, bagamoyo, sijui kigamboni na inasemwa ni bei ya chini sana, je uhalali wake upo vipi???

Mwenye taarifa au uzoefu na hili atujuze.
At your own risk, msikilize sana mleta mada.
 
Pesa, Ardhi na Mapenzi.

Hivi ni vitu vilivyo mwaga damu sana, vilivyo karibisha ushetani, vilvyo vunja utu na vilivyo tengeneza uhasama mkubwa sana.

Lakini bado ni vitu vyenye thamani kuliko vitu vyote.

Unapotafuta kiwanja, inabidi uwekeze zaidi katika umakini na upelelezi.

Kuna sehemu nilipata kiwanja, jamaa akawa tayari kuniuzia, lakini kumbe nyuma ya pazia kile kiwanja ni urithi wa watoto wa kaka yake yani baada ya kaka yao kufariki na barua zipo. Yeye akawa amepewa cha nyuma yake ila yeye anang'ang'ania pote.

Kuna sehemu nilipata kiwanja, jamaa akawa ananihakikishia kabisa kuwa hakuna tabu na hadi majirani zake (kabila moja) pale wakawa wanachochea. Lakini kwa bahati nzuri kuna afisa ardhi anaishi pembeni na anamjua mshikaji wangu niliekuwa nae, akatuita pembeni na kuniambia kuwa hapo pana mgogoro jamaa anaekuuzia alinunua kiwanja cha mtu mwingine kwa hio ni kama anataka arushie mtu janga asepe.

Kuna sehemu tena, jamaa ana burgain bei na mimi bei kumbe kiwanja sio chake, ni cha mdogo wake, baadae baada ya kumchimba eti ndio ananiambia sio chake. Kwa hio ina maana bei aliotaka kupatana na mimi ilikuwa kaeka commission yake juu.

KUWENI MAKINI.
yote hayo hayafui dafu kwa TUMBO..
 
Tumia wanasheri , uongozi wa eneo na mtu kutoka ofisi ya Ardhi
 
Back
Top Bottom