TUNAENDELEA NDUGU ZANGU
shahzad Alidai kwanza kwa hali jinsi ilivyo wanahitajika wataalamu wa Marine remote sensing kwa kutumia geophysical techniques.
( Hapa sasa nilibidi nitulie sana kwani mzee alianza kutema nondo ambazo ndio niliamini zina msaada kwangu. Na yeye apa alikua anaongea kama mtu ambaye amefika tayari kwenye site hivyo anayajua mazingira yote)
Lakini pia ukiacha wazee wale wa scuba diving kitu ambacho hapo awali yeye aliamini cha msingi alisema pia kuna haja ya kuwa na technology ya mawasiliano mnapokua site.
Aliongezea pia kwa kutaja vyombo ambavyo vitarahisisha zoezi la excavation, kwani maeneo mengi ya mji huo yalifunikwa au kudondokewa na kuta pana zilizo zunguka mji.
Kwakua mji huu ulikua na bandari lakini pia ulikua na hazina kubwa ya dhahabu basi ni dhahiri dhahabu hiyo haikua sehemu ya wazi. Je kama kulikua na chemba za kuhifadhi mali hiyo utazipataje hizo chemba bila ya kuwa na heavy duty machine za excavation.
Swala sio hizo chemba, kikubwa ni kuijua location ambayo ilikua na karakana au workshop zilizotumika kutengeneza masanamu yale ya dhahabu yaliyotumika kuabudia kwa nchi za huko ulaya.
SHAHZAD: je unafikiri zoezi hili halitahusisha serikali? Ni wazi kabisa kwamba watangulizi wetu walichemka kutokana na hizi changamoto japo hawakuziweka wazi.
Kama nilianza kuchoka hivi kwa taarifa ile kwani kuna namna ilinivunja moyo wa kuendelea na huu mchongo.
Tulifika home na moja kwa moja tulielekea kwenye chimbo letu ambalo lilikua na zana za kutosha zilizotokea kwenye mji huo.
SHAHZAD: mjukuu wangu usikate tamaa kikubwa hakikisha unapata hivyo nilivyokwambia kama unaitaka ela kweli.
MIMI: ila mzee wangu bado hujaniambia chochote kuhusu changamoto za walozi/ wachawi kwani ulisema kuna kila dalili ya kuwepo kwa shughuli hizo kwenye eneo hilo.
SHAHZAD: hahaha hahaha hahahahah unaogopa wachawi?
Usijali hakuna kiumbe muoga kama mchawi huoni wanafanya shughuli zao gizani wakati sisi tumelala, unamchokoza mchana yeye anakuja kulipa kisasi usiku ukiwa umelala.
Shahzad aligusia kitu na yeye, alisema wachawi ni washenzi sana specifically wa afrika kwani wanajua mambo mengi sana. Na lau kama wangeutaka utajiri basi kwa duniani hawa jamaa wasingefikiwa na yeyote kati ya binadamu wa kawaida isipokua wao wenyewe kwa wenyewe.
SHAHZAD: yaani ukitaka kujua wachawi wote hawana akili, kipindi kile ambacho sisi tunasumbuka kujua ni namna gani tutaitoa mali ya rapta. Wao wanafika mpaka eneo lile ila kwa ajili ya matambiko yao ya uchawi huku wakitumia zile artifacts za kale zilizopo maeneo yale.
Kuna jambo aliliongea shahzad japo ilikua ngumu kumuelewa mzee huyu, alisema katika sehemu ambazo hutakiwi kumuhofia mchawi basi baharini ni sehemu salama sana especially chini ya bahari.
Kulingana na shahzad ni kwamba ata wachawi wenyewe hufika huko kwa vibali maalum kwani sio milki yao kabisa. Aligusia kuhusu Schulz kwamba alikuja kichwakichwa bila kuaga kwao ndio maana aliangukia pua.
Kuhusu habari ya wachawi na bahari mzee shahzad alisema wachawi wana ground kubwa mbili tu ambazo wanazitumia kwa uhuru kwenye shughuli zao.
Na sehemu hizo ni angani na nchi kavu yaani ardhini, lakini speaking of bahari hawa jamaa hawana ujanja kabisa. Ukiona mchawi yupo baharini tena deep down ujue ni sawa na kumuona kobe juu ya mti nadhani umeelewa.
Tukianza na Angani huku kila siku tunasikia habari zao mara utasikia kuna mchawi kadondoka alikua anatokea mwanalumango mara utasikia kuna mchawi kudoka akielekea sehem Fulani.
Kiuhalisia walozi wanalitumia sana anga letu kwa mujibu wa mzee huyu shahzad lakini ujanja wao kwenye anga una kikomo pia. Ujanja wa walozi au wachawi kwenye anga huishia kwenye tabaka moja linaloitwa stratosphere.
Kwa mujibu wa shahzad ni kwamba wachawi wetu hawa hawana uwezo wa kufika mesosphere, thermosphere wala exosphere ambako ndipo mara nyingi inakua ni destination ya spaceship.
Hizo nilizozitaja hapo juu yaani kuanzia stratosphere, mesosphere, thermosphere na exosphere haya yote ni matabaka yanayopatikana kwenye anga hewa bila kusahau tabaka la chini au la mwanzo kabisa ambalo ni troposphere.
Sasa basi wachawi na ndege zao za mchongo huishia apo kwenye tabaka linaloitwa stratosphere juu ya hapo hawana ujanja. Kwa bahati mbaya sana shahzad hakuniambia kwanini hawana ujanja.
Lakini kwa namna moja niliamini ni kweli sababu kama jamaa wangeweza kutoboa mpaka exosphere maana wangeweza kufanya mpaka moon landing yaani wangefika mpaka kwenye mwezi kama kilichofanywa na apollo 11 mnamo mwaka 1969.
Sehemu nyingine ambayo ni pendwa na walozi ni kwenye hii ardhi yetu tunayoikanyaga kila siku tukitembea. Kwa mujibu wa shahzad Alisema wale wachawi wa daraja la chini kabisa yaani unakuta mtu ana miliki uchawi wa ef hamsini (jokes).
wachawi hawa ndio upendelea usafiri wa nchi kavu ambao karibia 90% hutumia FISI.
(nimeibold na kuipa color kabisa usiseme hujaona) hahaha ahaha
Hii ndio faida ya kukaa na wazee bwana yaani apa alinifurahisha sana hizi story na alinichekesha pia kwa jinsi aivyokua akisimulia.
Yaani wakati nipo haullaga nilikutana na Javier ambae alikua White supremacist ( alikua anaponda sana watu weusi) lakini leo nipo Tehran nakutana na shahzad anawaponda sana wachawi hususani wachawi wa bongo.
Na wakati anawaponda alisisitiza ya kwamba hawaogopi na pia ata mimi sitakiwi wala sina sababu ya kuwaogopa.
Kutokana na ukweli huo wa kwamba hawa walozi hufika huko baada ya kupewa idhini na wenye mamlaka ya kutawala bahari basi hawa jamaa hukosa makali kabisa kwa binadamu wanaokua huko.
Shahzad alinionyesha pete ya kawaida sana ambayo ilikua imefungwa vyema pembeni ya zana zilizokuwepo mezani pale.. alidai pete hiyo ndiyo ilitumika na watangulizi wake wakati wanaenda kuzamia ndani ya rapta kwa mara ya kwanza.
Anaendelea shahzad, kwa kuwa bahari inamuunganiko wa moja kwa moja na viumbe ambao huku duniani tunawatambua kama majini basi pete hiyo pia ina link na jamii za viumbe hao.
Apa shahzad alikua ana maanisha mamlaka inayotawala bahari kwenye ulimwengu wa giza ni majini kumbe basi aliposema wachawi hupewa vibali na mamlaka husika nadhani alimaanisha hao majini.
Hivyo basi nikiwa na trip au siku ambayo nitaenda kufanya preliminary survey huko rapta nihakikishe naenda nikiwa nimeivaa pete hiyo na yeye atanikabidhi bila hiyana kwakua nimeonyesha nia hiyo.
Aliongezea tena ya kwamba kwa kuwa nitaenda nimevaa pete hiyo hakuna kitu nitaacha ona nikiwa huko. Nitaona mali ambazo kuzitoa ndio kipengele lakini nitaona mauzauza na vikolombwezo vya kila aina ila havitokua na madhara.
Bado alikazia kua pete hiyo huvaliwa na mkuu wa msafara hivyo kama kwenye preliminary survey nitaenda na team ya watu zaidi ya wawili natakiwa mimi ndio nivae.
Nilimuuliza tena shahzad vipi kuhusu mshirika wake aliyejulikana kwa jina la john alielekea wapi baada ya kufeli kwa misheni yao kwani hawakutoka na chochote ndani ya mji huo.
Shahzad alisema john alirudi huko meha kwenye visiwa vya ushelisheli kuendelea na shughuli zake za kusaka dhahabu iliyopotelea baharini.
John alikua na Imani ya kupata Chochote ndani ya bahari hiyo ya Indi kwani takwimu zinasema kuna shehena nyingi ya dhahabu iliyotapakaa kwenye bahari hiyo kwa sababu ya ajali za meli.(shipwrecks)
Kwa mujibu wa shahzad bwana john aliiwinda sana meli moja ambayo ndio inaaminika kuzama na mzigo wa kutosha wa gold ambao thamani yake inakadiliwa kufikia pauni million 100.
Nilimuomba shahzad tumalize siku kwani mpaka hapo alishanipa madini ya kutosha ata yeye alisema siku hiyo ameongea sana na ametumia nguvu kubwa kukumbuka matukio ya nyuma hivyo hatoweza kuendelea zaidi ya hapo.
Aliomba tukapumzike ila kesho mapema nirudi kwani bado kuna mengi napaswa kuyajua. Lakini alinipa assignment moja, ninavyoenda nikajaribu kuwaza ni namna gani nitafanikisha zoezi hilo kwa kutumia maelezo machache aliyoanza kunipa.
Ninatakiwa kufikiria manpower lakini pia ninatakiwa kufikiria technology ambayo itanisaidia kufanikisha zoez hilo.
Wakati simulizi inaanza tulimjua kwa jina moja la Manuela, ila kwa sasa ni fatemeh. Je kuna jina jingine analo?
NB;
wakati simulizi inaanza tulimjua kwa jina la Manuela, na baadae tukamjua kwa jina la fatemeh, mbali na majina hayo lakini pia-
Tunamjua kama ethical hacker wa MOIS lakini pia aligundua uwepo wa virusi kadhaa kwenye mifumo yao ya kikompyuta iliyodhamiria kuharibu mifumo ya nyuklia. Mbaya zaidi ni programming code zake ambazo zilitumika kwenye 2010 stuxnet attack.
Fatemeh anaonekana kuwa ni moyo wa idara ambayo kwa miongo kadhaa imekabiliwa na upinzani mkubwa wa Mossad na CIA.
Kwanini alipewa misheni ya haullaga, je ni kwakua alikua tayari nchini peru kwenye misheni yake ya industrial espionage.
Je! Kuna story au majukumu mengine ya fatemeh hatujayajua, stay tuned, mambo mengi mda mchache.
Wanangu mchawi buku 3 [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787], ila mzigo utaisha trust me
(0623329512) ipo hewani sio Whatsapp pekee kama siku za nyuma,