Utajiri wa MO vs BAKHRESA: Vigezo gani hutumika kuwabaini matajiri?

Utajiri wa MO vs BAKHRESA: Vigezo gani hutumika kuwabaini matajiri?

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Jarida la Forbes limetoa orodha ya matajiri barani Afrika ambapo Mohammed Dewji ameendelea kushikilia usukani kutokea Tanzania na kushika nafasi 15 barani Afrika.

Mimi nina maswali kuhusu orodha hii, hivi hapa nchini hamna watu wana unreported wealth? Kuna watu wanaonekana kwa macho wana uwekezaji mkubwa Tanzania lakini kwenye hizi list hatujawahi kuwaona!

Mara kadhaa nimekuwa nikiona list ya matajiri wa Dunia na Afrika. Huko duniani sina tatizo maana niko mbali nao ila suala la Mo na Bakhresa huwa silielewi.

Kwa kutazama tu kawaida tena sio mimi peke yangu huwa tunaamini Bakhresa ana mali na utajiri mkubwa kuliko Mo. Lakini wenzetu "wataalamu" wa hayo mambo wanamuorodhesha Mo mbele ya Bakhresa.

Sasa nyie wajuvi wa JF naomba mtujuze ni vigezo gani hutumika ambavyo humbeba Mo mbele ya Bakhresa.

Njoo na hoja siyo ushabiki wa mipira

Screenshots_2022-01-25-14-17-32.png
 
Jarida la Forbes limetoa orodha ya matajiri barani Afrika ambapo Mohammed Dewji ameendelea kushikilia usukani kutokea Tanzania na kushika nafasi 15 barani Afrika. Mimi nina maswali kuhusu orodha hii, hivi hapa nchini hamna watu wana unreported wealth? Kuna watu wanaonekana kwa macho wana uwekezaji mkubwa Tanzania lakini kwenye hizi list hatujawahi kuwaona!
Matajiri wanajulikana hasa kupitia Benki na TRA sasa wewe una biashara inaonekana kwa macho kubwa ya mabilioni Benki akaunti INA laki mbili TRA kodi uliyolipa mwaka mzima laki moja utamwambiaje Forbes kuwa wewe tajiri ?

Wanaangalia rekodi za wazi sio za kichawi unalalia pesa ndani kwenye mto
 
Kweli tupu baelezee huyooo 😂😂😂😂
 
Tanzanian billionaire and former Member of Parliament Mohammed Dewji popularly known as Mo Dewji continues to hold the title as the richest man in the country as well as featuring among the wealthiest people in Africa.

In the latest Forbes list of the continent’s dollar billionaires in 2022, Dewji - the CEO of MeTL Group, is ranked 15th with a net worth of $1.5 billion.

The list features 18 billionaires worth an estimated $84.9 billion–15 percent more than twelve months ago and the largest combined tally since 2014 when there were 28 African billionaires; the average net worth is higher this year due to the current smaller number of list members, Forbes says.

Top of the list of African billionaires is Nigerian business magnet Aliko Dangote sittting on $13.9 billion, he is closely followed by South Africa's Johann Rupert and Family with a net worth of $11 billion and Nicky Oppenheimer & family occupying third slot valued at $8.7 billion, Egypt's Nassef Sawiris with a net worth of $8.6 billion is fourth, while Abdulsalmad Rabiu rounds up the top 5 five with $7 billion.

Stock prices and currency exchange rates from January 19, 2022 were used to measure the net worths.

Billionaires from seven African countries made the list. South Africa and Egypt have the most, with five each, followed by Nigeria with three billionaires.

My Take
We endelea kumuita Mwamedi labda itasaidia kumshusha
 
Nasikia kwenye hilo jarida ni ruhusa ukubali kuwekwa au ukatae.
Ndiyo maana Bakhresa hayupo.
kwa ufupi hapendi show off

Huku ni kuishi kwa ramli na nadharia. Hao unaowafikiria wana hela nyingi, hazionekani kwa macho. By the way, Forbes hawajalazimisha wewe ukubali, lakini hiyo ndo fact, wametoa namba 1 na kuendelea! Kama umtakae hayumo, basi hajakidhi vigezo vinavyopimika.
 
Leo imetolewa list ya matajiri, tungojee siku forbes wakatoa list ya wapambanaji GSM hawezi kukosa

Kwanini muwaseme GSM/HOME SHOPPING CENTRE badala ya majority shareholder mwenyewe Vasco Dagama? Mnawafanya WATANZANIA Kuwa ni mazuzu hatajui wizi wenu!
 
Back
Top Bottom