Utajiri wa nchi ni akili za Watu sio rasilimali kama madini na nyinginezo

Hii Nchi Ina watu wapumbavu Sana na mdomo Sana.Yote yanayojadiliwa Ni Pesa Sasa lijitu hakitaki kutoa risiti Wala kudai risiti ila linataka Hali nzuri,haiwezekani.

Wanatoa visingizio vya kijinga Mara ooh Pesa inaliwa na blaa blaa kibao ila kiuhakisia Pesa inayoliwa haisidi hata 30% na kwenye 30% na zilizosakia pengine nyingi zinaingia kwenye mipango na matumizi yasiyo na tija Sana..

Kwenye kupanga kipinkianze na wapi tupeleke Pesa kunahitaji mjadala ili tuwe na mipango yenye matokeo makubwa zaidi ila kesi ya wizi sio kubwa Sana hapa Tanzania ukilinganisha na Nchi Nyingi..

Nilisoma mahala fulani kwamba hizi NGOs huwa zinatumiq zaidi ya Til.3 kwenye Uchumi wa Nchi,Sasa ukiangalia hizo pesa pamoja na kwamba ni za Private sector ilitakiwa ziwekewe utaratibu yaani wao wa compliment pale Serikali inapoishia lakini huwa zinaiehia kwenye mikono ya wachache hukunzikiharibu Uchumi kwa kuingia kwenye mzunguko bila utaratibu maalumu na hazina tija..
 

Hata wangeiba 1% ni Haki ya wananchi kulalamika.
Ila walalamika lazima wawe wanaolipa Kodi(walioibiwa) sio jitu halilipi Kodi, halizalishi chochote ndani ya taifa alafu linakuwa la Kwanza kulalamika.
Kwa kweli mtu wa namna hiyo hana uhalali WA kulalamikia wezi au mafisadi.

Kila kitu kinaenda na wajibu, majukumu, na Haki
 
Wapo na wanaakili sana.Sema ubinafsi umewazidi baadhi ya viongozi wetu.Mungu tu ndie atawanyoosha mana wananchi wenyewe tumelewa Moshi wa Mwenge.
 
Nimesoma kwa kuruka ruka.
 
Yaani Ng'wigulu waziri wa fedha? Hakika hatujawahi kuwa siriazi.
 
Tatizo hadi leo tuna akina ''Sultani Mang'ung'o" wengi!
Ona awamu ya 4 tulivyoingia mikataba ya kipuuzi kabisa ya gas yetu!
Tena ya kupewa 'shanga' kama alivyofanya mang'ung'o mwenyewe!
 
Kutokujua unachokifanya ndio kukosa akili Kwenyewe huko
Nimesema hao wenye kusaini mikataba mibovu isiyo na faida kwa taifa wanajua vizuri tu wanachokifanya kuwa si sahihi.
Ndio maana watu hutaki katiba mpya yote ni katika kutaka kuweka mifumo mizuri.
 
Kuna nyumba nilikua naishi ya kupanga miaka kadhaa uwezi Amin hadi zamu ya chooni watu wanataka kuwekewa ratiba kama watoto wa secondary

Uwezo wa watanzania ni mdogo sana kwenye mambo mengi kiufupi watanzania hawajitambui
 
Hii point kubwa sana sababu viongozi ni matunda ya jamii ni kweli wanareflect jinsi tulivyo
 
Enzi zile Amin akawatimua Wahindi 70,000 kwa mkupuo na kuwanyang'anya kila kitu na kuwapa wananchi hawa unaowasema

Hivyo hivyo Mugabe nae kama huyo tu nae akatimua wazungu leo unanunua mkate mmoja million
Walijimikikisha mashamba ya muzungu matokeo yake waliiba matrekta yote na swimming pools wakanyea na kuyafanya dampo

Mwingine akaibuka kwetu akawa anaimba nchi yetu ni tajiri sana, tumeibiwa sana kumbe nyuma ya pazia wanaiba x2
Acha waishi hivyo hivyo ndio wamechagua maisha hayo na wamekataa kutoka
 
Kwangu Mimi hii ni thread ya kufunga mwaka 2022.ni madini tupu ahsante taikon.Unaweza kukuta mtu ni daktari au MWALIMU Lakini anakula ndizi kwenye daladala anarusha maganda dirishani.Hapa taikon unahisi TATIZO ni nini??
Hiki kitu kinanikera sana na unakuta ndani ya gari Kuna kopo/dustibin la kuwekea takataka lakin unakuta mtu anatupa takataka nje
 
Kwangu Mimi hii ni thread ya kufunga mwaka 2022.ni madini tupu ahsante taikon.Unaweza kukuta mtu ni daktari au MWALIMU Lakini anakula ndizi kwenye daladala anarusha maganda dirishani.Hapa taikon unahisi TATIZO ni nini??

Ukosefu wa Akili ni tatizo KUBWA.

Na Hilo tatizo miaka ya hivi karibuni litaingia Uzunguni. Tuombe uzima
 
Hii serikali huwa naifananishaga na bongo movie. Wasanii wa bongo movie hawana ubunifu hufanya mambo kimazoea, hawajui kwamba wako nyuma ya muda wakifanya jambo jipya kwao hutaka wajisifu na kusifiwa hata kama hilo jambo lilitakiwa kufanyika miaka kumi nyuma huko matokeo yake hujiona wamepiga hatua kubwa kana kwamba wameanza juzi hiyo bongo movie. Wasanii wa bongo movie pamoja na kwamba wanaangalia kazi za wenzao waliyoendelea huko ila bado hawajifunzi hata kwa yale yenye kuwezekana wanafikiri ndani ya duara lile lile la siku zote.
 

Nisiposifia nitafukuzwa kazi nifanyaje Mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…