Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani

Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani

Habari za leo wakuu, bila shaka mko poa.

Nitaendelea kusimulia afya yangu ikitengemaa maana siko vizuri, Siku mbili zimepita nimetoka huko Kigamboni sasa nadhani nilipata mdudu (Korona), aisee kanitandika kinoma, sema nimejitahidi sana kutumia virutubisho na hivi sasa naendelea vema japo viungo vya mwili vinauma vibaya sana!.

Msijali nitaendelea nilipoishia,hali itakuwa vema ndugu zangu.

Nawapenda sana.
 
Habari za leo wakuu,bila shaka mko poa.

Nitaendelea kusimulia afya yangu ikitengemaa maana siko vizuri,Siku mbili zimepita nimetoka huko Kigamboni sasa nadhani nilipata mdudu (Korona),aisee kanitandika kinoma,sema nimejitahidi sana kutumia virutubisho na hivi sasa naendelea vema japo viungo vya mwili vinauma vibaya sana!.

Msijali nitaendelea nilipoishia,hali itakuwa vema ndugu zangu.

Nawapenda sana.
Ila ile million 9 ulipigwa muraa, uongo ?
 
We jamaa hauko makini na pesa, mtu anakufungia vioo eti anasingizia betrii, ivi kwel unajua ndugu yako yupo njian anakuja eti betrii ikusumbue bas unaacha unalala zako kwa amani ameshindwa kuweka line kwa mtu au simu ingine ili ukimpigia umpate, au aweke battery lingine,

Bado amewash asimu na unampa 9 million na ata anapoishi haupajui. ulipuliziwa dawa ya umbu muraa
 
Habari za leo wakuu,bila shaka mko poa.

Nitaendelea kusimulia afya yangu ikitengemaa maana siko vizuri,Siku mbili zimepita nimetoka huko Kigamboni sasa nadhani nilipata mdudu (Korona),aisee kanitandika kinoma,sema nimejitahidi sana kutumia virutubisho na hivi sasa naendelea vema japo viungo vya mwili vinauma vibaya sana!.

Msijali nitaendelea nilipoishia,hali itakuwa vema ndugu zangu.

Nawapenda sana.
Pole na kumbe covid bado ipo
 
we jamaa hauko makini na pesa, mtu anakufungia vioo eti anasingizia betrii, ivi kwel unajua ndugu yako yupo njian anakuja eti betrii ikusumbue bas unaacha unalala zako kwa amani ameshindwa kuweka line kwa mtu au simu ingine ili ukimpigia umpate, au aweke battery lingine,

bado amewash asimu na unampa 9 million na ata anapoishi haupajui. ulipuliziwa dawa ya umbu muraa
Uaminifu wa mtu toka kijijini ni mkubwa sana.
Hajui mjini watu karibu wote wameharibika
 
Habari za leo wakuu,bila shaka mko poa.

Nitaendelea kusimulia afya yangu ikitengemaa maana siko vizuri,Siku mbili zimepita nimetoka huko Kigamboni sasa nadhani nilipata mdudu (Korona),aisee kanitandika kinoma,sema nimejitahidi sana kutumia virutubisho na hivi sasa naendelea vema japo viungo vya mwili vinauma vibaya sana!.

Msijali nitaendelea nilipoishia,hali itakuwa vema ndugu zangu.

Nawapenda sana.
Pole sana Omughaka get well soon mkuu[emoji120]

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Habari za leo wakuu,bila shaka mko poa.

Nitaendelea kusimulia afya yangu ikitengemaa maana siko vizuri,Siku mbili zimepita nimetoka huko Kigamboni sasa nadhani nilipata mdudu (Korona),aisee kanitandika kinoma,sema nimejitahidi sana kutumia virutubisho na hivi sasa naendelea vema japo viungo vya mwili vinauma vibaya sana!.

Msijali nitaendelea nilipoishia,hali itakuwa vema ndugu zangu.

Nawapenda sana.
Pole kijana ila siyo korona hyo

Wee sema una mambo mengine inakufanha ushindwe kuleta visa Happ
Kigamboni ulienda kufanya nn wakt wee unapaki boda boda bunju b je umeenda kupiga dili zako zile chafu[emoji23]

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
we jamaa hauko makini na pesa, mtu anakufungia vioo eti anasingizia betrii, ivi kwel unajua ndugu yako yupo njian anakuja eti betrii ikusumbue bas unaacha unalala zako kwa amani ameshindwa kuweka line kwa mtu au simu ingine ili ukimpigia umpate, au aweke battery lingine,

bado amewash asimu na unampa 9 million na ata anapoishi haupajui. ulipuliziwa dawa ya umbu muraa
Ni umpumbavu San amefanya huyu kiajna

I'll ukimbuambia unaambiwa uanaaribu story watu hwataki kuoji vitu vya msingi
 
Mjomba usijifanye msongo sana.
Hapa kila mtu ana maisha yake.
Hawatakuja kukulilia shida.

1. Wengine wanazo za urithi.
2. Wengine wanatoa stress zao huku
3. Wengine walinzi wanasubiria usiku wakalinde

4. Wengine madada poa wanazmsubiri shift
5. Kubwa zaidi wengine wako safarini wanasigeza muda wafike
Wengine now ndio muda wa lunch, tunasubiria msosi kwa mama ntilie huku tunaperuzi jf
 
stori kama hizi kabla ya kusoma hua nascroll mpaka mwisho ili kujihakikishia kua sitapoteza muda wangu.
 
Habari za leo wakuu,bila shaka mko poa.

Nitaendelea kusimulia afya yangu ikitengemaa maana siko vizuri,Siku mbili zimepita nimetoka huko Kigamboni sasa nadhani nilipata mdudu (Korona),aisee kanitandika kinoma,sema nimejitahidi sana kutumia virutubisho na hivi sasa naendelea vema japo viungo vya mwili vinauma vibaya sana!.

Msijali nitaendelea nilipoishia,hali itakuwa vema ndugu zangu.

Nawapenda sana.
Pole sana
 
Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani - 04.

Sasa muda ambao mke wa anko anafika pale nyumbani mimi nilikuwa nyuma ya nyumba ambapo kulikuwa kuna kama kibustani kidogo ndani yake kulikuwa kumepandwa miwa ambayo ilikuwa imekuwa mikubwa na hakukuwa na walaji,niliona nikate zangu muwa nikaa chini nikaanza kutafuna,kumbe aliingia chumbani anakolala yule mzee ambaye ni baba yake na akakuta amejisaidia kitandani na hakukuwa na mtu aliyemwangalia na kumjali,kwa mawazo yake yeye alidhani mimi nimemuona yule mzee na nikamuacha kama alivyo ili aendelee kuteseka!.
Akili na mawazo yake yalimtuma vibaya kwasababu sikuwa nimeingia mle chumbani tangia mchana,pia yule mzee alikuwaga kama na kakiburi fulani hivi ambako kalikuwa ka kijinga,anaweza kuwa amebanwa na haja kubwa wala asiite mtu yeyote,utakuta ameinyanyuka ameingia chooni na amechafua vibaya bila hata kuflashi.Inawezekana alifanya makusudi siku ile ili kunikomoa.

Kumbe muda huo Anko anapewa makavu laivu ilikuwa ni hiyo ishu na bahati mbaya sana Anko wangu alikuwaga akoromi kwa yule mwanamke bali hasira za kugombezwa na mkewe zilikuwaga zinaishia kwa wanae au mimi kwa wakati ule nipo kwake.

Muda huo ambao nipo zangu natafuna miwa sina habari,kumbe alimwambia yule mfanyakazi akaingia mle ndani akatoa yale mashuka akawa amemnyanyua mzee akampeleka bafuni mzee akajisafisha kisha akatandika shuka safi na kuweka mazingira ya chumba poa.

Mimi sikufahamu chochote kwasababu nilipomaliza kula miwa nikazunguka kule mbele ya nyumba ndipo nikakuta gari ya mke wa anko ikiwa imepaki nikajua atakuwa amerudi,sikutaka kuingia ndani kwasababu ilikuwa bado mapema,niliingia stoo nikachukua fagio la nje nikaanza kufagia pale nje.

Nilipomaliza niliingia ndani kuoga na kubadili nguo ili nije nikae sebuleni nitazame luninga,wakati naingia mle ndani nilikuta mzee amelala na kitandani kukiwa na shuka nyingine,sikufahamu kumbe dakika chache zilizopita hali ya mle ndani haikuwa nzuri,sasa huo usiku anko alivyorudi ndipo mkewe akamuamshia mtiti!.

Baada ya hayo malumbano Anko alivyorudi sebuleni alikuwa amebadirika na sikutaka kusema chochote mimi niliendelea kutazama luninga,chakula kilipotengwa alielekea kula na alipomaliza aliingia chumbani kwake!.Mkewe yeye sikuonana nae kwa siku hiyo.

Asubuhi kama kawaida wao waliondoka wakawa wamelekee kazini,pale nyumbani nikawa nimebaki mimi,yule binti wa kazi pamoja na mtoto mkubwa wa anko ambaye naye aliondoka ilipofika mida ya saa 3 asubuhi.Sasa baada ya yule mtoto wa Anko kuondoka,yule binti wa kazi alikuja kuniita nikanywe chai,muda huo nilikuwa nje napambana kungolea nyasi kwenye maua yaliyokuwa kando ya fensi.

Binti wa kazi " Hivi jana ulikuwa wapi?"

Mimi "Jana?,Jana saa ngapi?"

Binti wa kazi " Aliporudi Mama"

Mimi "Nilikuwa kule Bustanini"

Binti wa Kazi "Jana mama kagomba"

Mimi "Alikuwa anagomba kuhusu nini?"

Binti wa kazi "Aliporudi aliingia chumbani kwa babu akakuta babu kajinyea,alikuwa anakuulizia mi nikajua labda umetoka!"

Mimi "Alijenyea saa ngapi?,mbona mchana nilipotoka ndani alikuwa tu vizuri"

Binti wa kazi "Alikusema maneno mabaya sana,we acha tu"

Mimi "Mimi siyo mjinga nimuone huyo mzee akiwa anashida niache kumsaidia,mbona siku zote namuosha na kumpeleka chooni na mpira nambadilishia!"

Mimi "Jana nilikuwa bustanini na sikutoka nje kabisa"

Mimi "Kwani kabla sijaja hapa nani alikuwa akimuangalia mzee?"

Binti wa kazi "Nani zaidi yangu?wanae tu wala hawana time na babu yao"

Baada ya mazungumzo ya muda kadhaa nilinoti kitu kwa yule dada wa kazi ambacho hakutaka kabisa kuniambia,kwa kifupi yule mke wa anko inaonekana alitoa shiti nyingi dhidi yangu,niliamua kutulia na kutafakari.
Sikwenda kwa Anko uenda kwakusema nimepigwa na maisha ili anifadhili la hasha,nilienda pale kwasababu wakati nafika mjini mwenyeji wangu alikuwa hapatikani,sasa kuna muda nilikuwa nashangaa wanavyonichukulia ni kana kwamba nimepigwa na maisha!.

Baada ya kupata kifungua kinywa niliamua nimsubiri Anko akitoka kazini ile jioni nimuage na kesho yake nisepe niwaache wapambane na matatizo yao na roho zao mbaya.Kweli,usiku ule kabla ya kula tukiwa pale sebuleni tukiangalia taarifa ya habari,nilimwambia kesho mimi nitaondoka.

Anko Nico " Utaondoka kwenda wapi?"

Mimi "Nitaenda kwa yule mtoto wa baba mkubwa"

Anko Nico " sawa siye tupo"

Baada ya hayo mazungumzo niliona kabisa nilikuwa sitakiwi.Ukiachilia Anko,lakini mkewe na watoto wa Anko walikuwa ni watu ambao hawana time na mtu,tangia nimefika hapo hawakuwahi hata kusema na mimi wala kujua hali ya maisha ya shangazi yao,walikuwa ni watu ambao hawakuwa na muda kabisa,pengine uzungu uliwaharibu au walilithi tabia za kwao mama yao.

Kesho yake nilimuaga yule mzee pamoja na yule binti wa kazi nikaondoka zangu,nilipotoka nje nilitembea hadi kituo cha daladala nikapanda kuelekea tegeta.

Kwakuwa nilikuwa nimeshawasiliana na Kileri akawa ameniambia anakaa Kivule na hivyo ilipaswa nipande magari yatakayonifikisha ubungo stendi ya daladala na nikifika hapo nipande za gongo la mboto nikashukie banana kisha nichukue za kivule.

Namshukuru Mungu nikawa nimefika na jamaa akaja kunichukua tukaelekea kwake.Nilipofika kwa jamaa nilikuta anakaa kwenye nyumba ambayo bado haijaisha na nilikuta mafundi wakiwa wanaweka vigae kwenye vyumba baadhi.

Kileri "Karibu wa kwetu,hapa mimi ndipo naishi na familia yangu"

Mimi "Hongera kaka umejitahidi"

Kileri "Kawaida tu,naipeleka mdogo mdogo mpaka itaisha,mjini hapa ukiwa na kwako unaepuka usumbufu wa kodi"

Baada ya mazungumzo ya hapa na pale,jamaa akawa ameniambia kesho yake tungeenda Tandika ambako alidai ndiko anakofanyia biashara ili nikajionee namna biashara ilivyo shamiri.

Ilipofika asubuhi tuliondoka kuelekea huko Tandika kama alivyokuwa ameniambia.Tulipofika hapo Tandika kuna duka moja la vyombo tuliingia lakini kuna kitu kikanishangaza.

Itaendelea......
Endelea mkuu
 
Back
Top Bottom