Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani

Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani

Huu uzi unaelekea kufa kama wa huyu jamaa
Screenshot_20230109-171332.jpg
 
Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani - 14.




Mimi "Nishafika"

Warda "Umesimama wapi?"

Aliendelea "Ooh ok nishakuona"


Baaada ya nusu dakika alikuja mwanamke mmoja mwenye asili ya uarabuni akiwa amevaa hijab nyeusi ikiwa imempendeza sana kutokana na rangi ya ngozi yake.

Warda "Bila shaka wewe ndiye uliyetumwa na Ally"

Mimi "Yes ndiye mimi "

Warda "Unaitwa nani?"

Mimi "Naitwa Umughaka"

Warda "Mhh mbona Ally hakunitajia jina hilo!"

Mimi "Kaka Ally amezoea kuniita Master,Umughaka ndiyo jina langu halisi"

Warda "Ooh sawa nimekuelewa"

Aliendelea "Ngoja kwanza nimpigie simu halafu nikupe uongee nae"

Alichukua simu yake akaanza kumpigia simu Ally Mpemba na wakaanza kuongea,baada ya kuongea akanipatia na mimi simu ili niongee na Ally,baada ya kujiridhisha aliniambia nifuatane nae.Tulitembea kama hatua kumi kisha tukaingia kwenye nyumba moja ambayo ilikuwa ni ghorofa,ile ghorofa ilikuwa ni Apartment ya watu kuishi na haikuwa kwa ajili ya ofisi.

Baada ya kufika ndani tuliingia kwenye lift nikaona yule dada anabonyeza batani ambayo ilionyesha namba 4,ile lift iling'oa nanga na baada ya sekunde kadhaa tukawa tumefika kwenye floor namba 4,tulipofika tulitembea hatua 3 tukawa tumefika kwenye chumba ambacho baada ya kukifungua tuliingia ndani.

Warda "Nisubiri hapo "


Aliingia chumbani ambako hakutumia muda mwingi akawa ametoka na pochi kubwa ambayo ilikuwa imetuna.

Warda "Hizi ni pesa ambazo Ally amesema nikukabidhi sasa kabla ya kuondoka inapaswa uzihesabu ndipo uondoke"

Alizitoa zile hela kwenye ile pochi kubwa ya kike,kiukweli zilikuwa ni pesa nyingi sana.Nilianza kuzihesabu na kuzipanga ndipo nilipata jumla yake milioni 40.Wakati nazihesabu alikuwa amekaa akiniangalia huku akiendelea kuchezea simu yake.

Mimi "Tayari"

Warda "Umepata bei gani?"

Mimi "Milioni 40"

Warda "Ok uko makini"

Alichukua karatasi pamoja na wino akawa ameweka pale juu ya meza na kuniambia.

Warda "Shika hii"

Aliendelea "Utasaini hapa na hapo chini utaweka dole gumba "

Basi nikafanya kama alivyoniambia na nilipomaliza alichukua simu yake kisha akampigia simu Ally Mpemba.


Warda "Haya nishamkabidhi pesa yako,huyu hapa ongea nae"

Ally Mpemba "Master,huo mzigo nenda kaniwekee benki,nakutumia sasa hivi vielelezo"

Mimi "Sawa kaka"


Warda "Ngoja nikupatie kibegi kidogo,huo mkoba nina kazi nao"

Sasa baada ya kupewa kibegi kidogo,niliziweka zile hela kwenye kile kibegi huku akili yangu ikiwa imechanganyikiwa kabisa,nilipanga nitoroke na zile hela,baada ya kushuka ghorofani nilianza kutembea mdogo mdogo kuelekea mnazi mmoja.

Nilikuwa najisemea uenda ndiyo wakati ambao Mungu aliamua kunitoa kwenye umasikini kupitia zile hela za Ally Mpemba kwa maana hata kama ningeondoka zangu kurudi Mwanza asingepata kwasababu ni mtu tu ambaye nilikutana nae kkoo na halikuwa hanijui kiundani wala haifahamu familia yangu,kiukweli nilikuwa kwenye vita nzito kuhusu zile fedha lakini niliamua nizipelekea Benki ili kuendelea kuonyesha uaminifu wangu kwa Ally,nilisema kama ni umasikini niliandikiwa basi ningekufa masikini tu hata kama ningekimbia na zile hela,pengine ni heri kufa masikini kuliko kuiba cha mtu ambaye ufahamu kakipata vipi,Uaminifu kwangu hata kama usingenilipa lakini ungenijengea heshima kubwa miongoni mwa marafiki na watu wa karibu,hivyo niliamua kuwa muaminifu ingawa nilikuwa nahitaji sana fedha.

Nilitembea kwa haraka sana hadi katikati ya jiji mtaa wa Azikiwe ambapo kwa mujibu wa maelekezo ya Ally Mpemba ilipaswa niende hapo ilipo benki ya Crdb kuziweka hizo fedha.

Baada ya kumaliza kila kitu pale benki,niliondoka zangu kurudi kkoo,nilipofika kwakuwa muda nao ulikuwa umeenda sana,nilimwambia Aunt Farah anipatie kile kiasi ambacho aliambiwa na Ally anipatie ili niondoke zangu kununua mahitaji ya siku hiyo kisha niondoke nikaandae mapema.

Aunt Farah alinikabidhi laki tatu ambazo kwa mujibu wa maelekezo ya Ally Mpemba ni kwamba,laki mbili ningeitumia kwa mahitaji ya vitu kwa siku zilizokuwa zimebaki hadi yeye kurudi na ile laki moja ingekuwa kwa ajili ya matumizi yangu ya kawaida.

Kweli,ile kazi niliifanya kwa uaminifu mkubwa mno hadi siku ambayo alirudi Ally mpemba alikuwa akinishangaa namna nilivyokuwa muaminifu kiasi kile na sikuwahi kumwambia mtu yeyote siri ile.


Ally Mpemba "Kaka kati ya watu na wewe ni mtu!"

Mimi "Kwanini kaka?"

Ally Mpemba "Ndugu zangu si waaminifu kama wewe ulivyo muaminifu"

Aliendelea " Sielewi hata nitakulipa nini!"

Mimi "Usijali kaka haya ni maisha tu!"


Kiukweli nilikuwa najiuliza mle ndani kwa Ally kulikuwa na kitu gani lakini nilikuwa nakosa jibu kwasababu ndani ya siku zote hizo nimekuwa nikiwinda nipate kukiona lakini nilikuwa naishia kusikia sauti tu,mimi sikutaka kuonyesha kama nina wasiwasi,nilichofanya ni kwamba nikiwa nazungumza nae yeye aelewe mimi sifahamu chochote na nilikuwa napotezea mambo mengine ili asije kunoti kitu kutoka kwangu.

Niendelea kupiga kazi yangu ya usajili wa line za simu huku na ile kazi ya usimamizi wa Catering ikiendelea,kiukweli kama kuna muda ambao nilitengeneza pesa ilikuwa ni kipindi hicho,baada ya kupata pesa ya kutosha,nilimtafuta dalali akanitafutia uwanja maeneo ya Chanika Zingiziwa chenye ukubwa wa 25 x 20 nikawa nimenunua Milioni 3.

Nikawa nimepanga nipambane sana ili nikusanye fedha nyinngine nianze ujenzi mdogo mdogo ili nitoke kwenye nyumba za kupanga na mimi niamie kwangu.

Kuna siku tulipata tenda ya kuhudumia chakula maeneo ya Mikocheni,sasa Ally akawa ameniambia siku iliyokuwa inafuata nisiingie kazini ili niende kuwasimamia wale kina mama na vijana kama kawaida yangu maana ndiyo ilikuwa kazi yangu,kiukweli Ally alikuwa akiniamini sana na ilifika kipindi fedha zake zote mimi ndiye nilikuwa nikizipeleka benki,mkurya mimi nikajiona ni mtu mwenye bahati ya kuaminika na na mtu mwenye asili ya uarabu kuliko wakurya wote kutoka Tarime;kweli,siku iliyofuata sikwenda kazini kama kawaida na nilimpigia simu Team leader wangu nikampanga kabisa ili asije akaona baada ya kushika shika vihela nimeanza kuwa na kiburi.

Baada ya maandalizi mimi na timu yangu ya Catering,tukawa tumefika maeneo ya mikocheni kama kawaida,tuliendelea na maandalizi hadi kuhakikisha vitu vyote viko sawa,sasa tukiwa kwenye hiyo shughuli mida ya 2 usiku,Ally akanipigia simu akiwa na kiwewe kisichokuwa cha kawaida.


Ally Mpemba "Master hebu fanya haraka njoo hapa Sinza Mori"

Mimi "Kaka Sinza Mori sipafahamu"

Ally Mpemba "Hebu mpelekee Jabir simu niongee nae"

Baada ya kumpa Jabir simu na kuzungumza nae inaonekana alimwambia Jabir anitafutie muda ule Taxi na akamuelekeza eneo ambalo ningemkuta,sasa baada ya kupata Taxi,Jabir alimpatia maelekezo yule dereva kisha akaniambia niingie kwenye gari tuondoke.

Tulipofika hilo eneo ambalo ambalo Ally alikuwa amesema nimkute pale,nilimpigia simu akaniambia niingie ndani,ilikuwa ni hotel kubwa tu ambayo pia ilikuwa ni bar,nilipoingia ndani nilimkuta jamaa yupo na watu kadhaa wakiwemo mademu wenye asili kama yake wakila na kunywa.


Ally Mpemba "Kaka kanisaidie kufungua chumba,siunajua nimejisahau "

Aliendelea "Aiseee yaani hata sielewi nimejisahau vipi!"


Mimi "Sawa kaka ngoja sasa niwahi!"

Ally Mpemba "Ukishafungua utanirudishia hapa funguo utanikuta hapa hapa "


Mimi "Sawa kaka"

Niliondoka kuelekea kwenye Taxi tukaondoka zetu kuelekea Magomeni,nilipofika nilimwambia dereva Taxi anisubili nje ya geti.Nilifungua mlango kisha nikaingia ndani nikawasha taa,sasa nilipowasha taa sikuona kitambaa cheupe pale kwenye ile meza ya kioo ndipo nilielekea jikoni kwenye kabati nikakikuta ikabidi niende nikitandike kisha nikachukua kabeji na mboga mboga nikaziweka juu ya ile meza,baada ya kumaliza niliondoka zangu nikaenda kufungua ule mlango wa kile chumba.

Sasa nilipomaliza kuufungua ule mlango nikiwa nimegeuza mgongo naondoka ili nitoke ndani nifunge mlango niondoke,aisee nilisikia nimesukumwa na nguvu isiyokuwa ya kawaida,ile nataka kuanguka chini nilimuona kiumbe wa ajabu ananipita kwa kasi ya ajabu akiwa uchi kama alivyozaliwa akikimbilia sebuleni na kuanza kuyafakamia yale makabeji kwa spidi kali mno,nilipokuwa bado naendelea kushangaa na kuhamaki yeye hakuwa kabisa na muda na mimi.

Ndipo nilimshuhudia mwanamke aliyekuwa na asili ya kiarabu lakini akiwa na manywele mengi si kichwani tu hadi kwenye makwapa na sehemu za siri,alikuwa anatoa harufu kali sana ambayo haikuwa ya kawaida.Niliogopa sana na ikabidi nikimbilie nje na kufunga mlango kisha nikaelekea kwenye lile bomba la nje kunawa,baada ya kumaliza kunawa nikatoka nje nikafunga geti nikapanda Taxi kurudi Sinza kumrudishia jamaa funguo,kiukweli roho ilichafukwa sana na niliogopa sana na hata ujasiri niliokuwa nao wote uliyeyuka.

Huruma,majuto na masikitiko vyote kwa pamoja vilinisumbua sana kwa usiku ule;Sasa wakati nikiwa kwenye gari narudi Sinza,Ally Mpemba alinipigia simu akiwa kama mtu aliyepagawa.



Itaendelea................
Halafu mwanamke unaenda kuolewa na huyo Baba na utajiri wake ukijinasibu umeokota dodo kwenye mwarobaini [emoji30][emoji30][emoji30]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani - 15.




Ally Mpemba "Kaka ...kaka....umefanya nini! Kaka!?"

Mimi "Kuna nini kaka Ally?"

Ally Mpemba "Kaka unataka kuniua?"

Mimi "Kaka Ally uko poa kweli?"

Basi jamaa alianza kulia kwa kwikwi kitu ambacho kilikuwa kikinichanganya zaidi,sikuelewa kama yale maneno aliyokuwa akiniambia yalikuwa ya kwangu au labda kuna mtu alikuwa akimpigia simu bahati mbaya ikaja kwangu!.
Nilipofika lile eneo ambalo nilimuacha Ally Mpemba akiwa na rafiki zake sikumkuta hivyo ikabidi nimpigie simu.

Mimi "Kaka nimerudi na sikuoni hapa!"

Ally Mpemba "Nisubiri hapo hapo narudi muda huu"

Haikupita hata dakika 20 jamaa akawa amefika pale akamlipa yule dereva taxi kisha akaniambia niingie kwenye gari yake tuondoke.Wakati tukiwa kwenye gari jamaa alionekana kana kwamba amechukia sana na sikuelewa kilichokuwa kimemchukiza ni kitu gani.

Ally Mpemba "Daah ndugu yangu nilikwambia ufike ufungue tu chumba uondoke sasa wewe umefanya nini?"

Mimi "Kaka nilipofungua chumba ile natoka nielekee nje ndipo yule kiumbe akanipita akikimbilia sebuleni"

Ally Mpemba "Kaka ushaharibu"

Kwa namna ambavyo jamaa alikuwa amechukia niliamua kukaa kimya ili nione atafanya kitu gani,sikutaka kabisa kumuongelesha kwa wakati ule maana niliona ningeendelea kumuudhi,sasa kumbe kile kitendo cha mimi kumuona yule kiumbe wa ajabu kilimshitua Ally Mpemba kule alikokuwa na sikuelewa alijuaje,kiukweli nilibaki na maswali mengi sana ambayo hayakuwa na majibu;kwakuwa nishakuwa mtu mzima tayari,niliamini hata fedha alizokuwa nazo Ally Mpemba zilikuwa na msukumo wa ushirikina ndani yake,kiukweli niliamua kukaa kimya ili nione ataniambia nini!.

Tulivyofika nyumbani mida ya 4 usiku,nilishuka kwenye gari nikafungua geti kisha jamaa akaingiza gari ndani na kuipaki,alishuka haraka haraka akaniambia hebu njoo ndani,alivyofungua mlango na kuzama ndani tukakuta yule kiumbe amekula kila kitu kilichokuwa pale kwenye meza kama kawaida,sasa Ally Mpemba akaniambia nitoe kile kitambaa nikipeleke jikoni kisha nimsaidie kusafisha pale sebuleni,yeye aliingia chumbani ambako alikaa kwa muda kama wa dakika 5 kisha akawa amerudi pale sebuleni akiwa amevaa kanzu nyeupe akiwa amejifunga na kitambaa,mkononi akiwa ameshika kanzu nyingine nyeupe akanitaka niivae.

Ally Mpemba "Vaa hii tafadhali!"

Mimi "Nivae juu ya nguo zangu hizi?"

Ally Mpemba "wewe vaa hivyo hivyo tu!"

Baada ya kuvaa ike kanzu ambayo ilikuwa ikinukia manukato mazuri,alichukua kitambaa cheupe kama alichokuwa amejifunga kichwani akanifunga na mimi!.Kimuonekano tulifanana kama wale jamaa wa dubai au saudia wanao vaa kanzu na vilemba.
Aliisogeza ile meza ya kioo pembeni kisha akatandika nguo ngumu kama kikoi kisha akanitaka nimsogelee.

Ally Mpemba "Wewe ni rafiki yangu na ninakuamini sana,tafadhali nisaidie!"

Mimi "Nikusaidie nini kaka?"

Ally Mpemba "Nifuate nitakavyokuelekeza"

Mimi "Sawa kaka"

Ally Mpemba alikuwa akitamka maneno ya kiarabu ambayo alinitaka na mimi nimfuatishe,alikuwa akitamka huku tukiwa tumekaa chini ya kile kikoi,baada ya kufanya lile zoezi kwa kurudia rudia kwa muda wa nusu saa tukawa tumemaliza na kisha akatoa kile kikoi akawa amekirudisha chumbani kwake.Aliporudi tena pale sebuleni aliniambia nikae kwenye sofa nami nikaa!.

Ally Mpemba "Kaka naomba ulichokiona ibaki siri yako!"

Aliendelea "Hakuna mtu yeyote anayejua ili jambo isipokuwa wewe"

Mimi "Usijali kaka haya ni maisha tu!"

Ally Mpemba "Mimi nilikuchukua wewe unisaidie mambo yangu kwakuwa wewe unamkondo wa hela"

Aliendelea "Na umekuwa muaminifu nahitaji kukufikisha mbali zaidi!"

Aliendelea "Huyo uliyemuona siyo kiumbe wa ajabu bali huyo ndiye anayenipatia hela na mali hizi unazoziona"

Aliendelea "Siyo mkorofi na akikupenda utamfurahia,huwezi kujiuliza kwanini wewe ndiye nilitaka uwe karibu na mimi?"

Wakati ananiambia mambo yote hayo mimi nilikuwa nimetulia tu nikimuangalia huku nikitikisa kichwa cha kuonyesha ukubali kwenye maswali aliyotaka ukubali wangu.

Ally Mpemba "wewe unanyota ya utajiri master labda uichezee mwenyewe!"

Mimi "Kweli kaka!?"

Ally Mpemba "Una nyota ya pesa ambayo pesa ikija kwako haitoki labda uitoe mwenyewe au mtu akuchukue uwe unamzalishia pesa!"

Aliendelea "Kaka mjini hapa,ukifa masikini shauri yako,mimi nakushauri kama rafiki yako"

Mimi "Kaka kuna mtu anapenda umasikini?,nahangaika juani ili nipate pesa kaka"

Ally Mpemba "Pesa unatembea nayo nyuma yako harafu unasema unahangaika juani!,watu wa bara hamjuagi kuchangamka!"

Mimi "Kaka nielekeze namna ya kufanya"

Ally Mpemba "Wewe unakifua?,siyo unapenda kupanda tu kwenye Range ukadhani mambo ni mepesi"

Mimi "Kaka kama nimewahi kushika bunduki hakuna jambo litakalo nishinda"

Ally Mpemba "Bunduki mwatumia huko bara,hapa mjini twatumia kisomo tu mambo yajipa!"

Aliendelea "Hebu simama unifuate"

Nilisimama nikamfuata Ally Mpemba kisha tukaingia kwenye kile chumba kilichokuwa na yule kiumbe wa ajabu,baada ya kuingia ndani aliwasha taa akasogea mpaka kwenye kabati la ukutani kisha akalifungua,alipolifungua akaanza kuita kwa sauti.

Ally Mpemba "Mayaaa"

Aliendelea "wewe Maya toka nje nakuita"

Alipokuwa akiita yule kiumbe akawa anaunguruma kwa mtetemo,kiukweli nilisogea nyuma kwa hofu maana haikuwa hali ya kawaida na sikuelewa siku zote jamaa alikuwa akiishi vipi mle ndani peke yake na yule kiumbe bila ndugu zake kujua jambo lolote!.

Baada ya kuita hilo jina la Maya kwa muda kadhaa,yule kiumbe wa ajabu alitoka na alipotoka alipomuona jamaa alimuinamia kama kumsujudu,kiukweli kilikuwa ni kitendo kilichonishangaza sana kwasababu Ally Mpemba kila alichokuwa akimwambia yule kiumbe alionekana kuelewa na kuogopa.Ally Mpemba kuna lugha aliongea nae kisha yule kiumbe aliyekuwa akitoa harufu ya ajabu aliondoka akarudi kwenye lile kabati kisha Ally Mpemba akarudishia lile kabati.

Kumbe kwenye lile kabati kulikuwa kumechimbwa shimo kama la futi sita na ndipo yule kiume alikuwa akikaa,sasa kama ulikuwa ukifungua ile kabati ilikuwa ngumu kumuona kwasababu alikuwa akiingia kwenye lile shimo kulikuwa na ubao ambao ulikuwa ukifunika na hivyo siyo rahisi mtu wa kawaida hata kama ingetokea kuingia mle chumbani kujua kama kulikuwa na mtu mle ndani labda kama ikitokea umeingia yule kiumbe aanze kuunguruma!.

Mimi "Kaka huyu ni nani kwani?"

Ally Mpemba "Nishakwambia huyo ndiye kila kitu kwangu sheikh"

Aliendelea "Watu wa Bara hapa mjini mmekuja kuwashangaa watu"

Aliendelea "Au nawe unataka kuwa msindikizaji?"

Mimi "Hapana kaka"

Ally Mpemba "Kwanza kabla ya kukusaidia inapaswa uslim"

Mimi "Kuslim tu kaka,mbona haina shida hiyo"

Ally Mpemba "Usiseme haina tatizo,usijedhani ni kuslim kama unavyodhani weye!"

Ally Mpemba " mtu wa kukusilimisha apatikana hapo chumbe"

Aliendelea "Uko tayari mi nimuandae?"

Mimi "Mimi nipo tayari kaka"

Aliendelea "Sawa lakini haya yote uliyoyaona humu ndani yabaki humu humu ndani,utanichukiza sana nikiyasikia sehemu na walahi sitokuacha salama"

Baada ya maneno hayo nilianza kuingiwa uoga na hofu ya ajabu,kiukweli sikujua ni kitu gani kilichokuwa kinanitia hofu muda huo lakini nachokumbuka ni kwamba niliingiwa na hofu.Sasa baada ya majadiliano yale,Ally Mpemba alinipatia funguo za gari ile Aud akanitaka nikalale,sikufahamu ni kwanini vile vyumba vingine ambavyo vilikuwa vimefungwa hakutaka nilale huko hadi aniambie nikalale kwenye gari nje,kiukweli kwa maisha jamaa aliyokuwa akiyaishi ilifika sehemu na mimi nikazamani kuwa kama yeye.

Marafiki muda mwingine utushawishi hadi kujikuta tunaangukia kwenye maisha mabaya kuliko hapo mwanzo,mimi baada ya kufahamiana na Ally Mpemba nilidhani uenda maisha yangu yangekuwa mazuri kumbe haikuwa kama nilivyodhani,ilifika sehemu nikaacha kazi yangu ya usajili wa line iliyokuwa ikinipatia fedha halali na kudandia maisha ambayo baadae niliyaona ni kero na yenye majuto.Kiukweli ilifikia hata kazi niliyokuwa nikiifanya niliiona ya kipumbavu baada ya Ally Mpemba kuwa ananipatia fedha nyingi za bure bure ambazo nilizifurahia bila kujua kuna siku zingenigharimu.Tangu nimemfahamu Ally Mpemba na pamoja na yeye kuwa rafiki yangu,sikuwahi hata siku moja kulala kwenye ile nyumba yake na yeye mwenyewe hakuruhusu mimi kulala mle ndani.

Baada ya wiki kama mbili tulijiandaa na jamaa akawa mwenyeji wangu kuelekea kisiwa cha Chumbe Unguja.


Itaendelea...........
Uhuuu imbombo !

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom