badison
JF-Expert Member
- May 29, 2015
- 1,450
- 2,761
- Thread starter
- #41
Nianze kwa kukubalina na wewe kuwa ni kweli binadamu ana sehemu tatu,Body,Mind na Spirit. Lakini hakuna uwezekano wa mwanadamu kuzaliwa bila nafsi. Kimsingi binadamu ni spirit yenye soul na inaishi ndani ya body.Chenye uwezo wa kusimama peke yake ni Spirit na sio soul wala Body. Kwa hiyo ni impossible kwa mwanadamu kuzaliwa bila soul otherwise huyo ni creature wa aina nyingine na sio binadamu.
Soul inadeal na mambo makuu matatu,Emotions,Will and Mind.Binadamu wote wana hisia ambazo zinaweza kuwa Hasira,furaha,amani,wasiwasi,woga nk.Bila nafsi ni impossible kufeel hizi emotions.Lakini pia kila binadamu anamaamuzi au machaguzi yake whether anayaonyesha kwa watu au lah.Hii ndo tunaita will hata kichaa anachagua kuacha jambo moja na kuamua kufanya lingine.Binadamu wote wanahuu uwezo na hawawezi kuupoteza.Lakini pia kila mwanadamu anauwezo wa kuthink logically,kutunza kumbukumbuku za matukio ya awali nk.Hii ni uthibitisho wa uwepo wa Mind.
Kwa hiyo its impossible kwa binadamu kuexist without soul.Soul and spirit always exist together. Kuna material mengi sana outthere lakini material mengi hayanaga ukweli especially material yanayodeal na Mambo ambayo ni Immaterial.Choose your materials wisely.
Tuanze na material ambayo yapo relevant kwako mfano kitabu cha biblia Marko 8:36 kinasema For what shall it profit a man, if he shall gain the whole world, and lose his own soul? Hii kwanza inakufundisha mtu anaweza kuishi bila nafsi na akafanikiwa kwemye mambo ya kidunia kwa kupitia kutesa mwengine. Nafsi ni ile sauti inayoishi ndani kwako haisuhiani kabisa na uhai wako. Kuna watu hawana internal dialog sema ni ngumu sana kukubali juu ya hili na wengine kwa kiupitia hii mada wamejua wapo katka kundi gani.
Uhai wa mwanadamu upo kwenye damu tuu ndio mana unapaswa kujua kuwa roho inaishi kwenye damu. Katika maisha ya kibinadamu mambo mengi yamefichwa kwa kigezo cha kutokuamini ukweli kwani truth is stranger than finction.
Sociopaths na psychopaths are soulless being au ni aina fulani ya watu ambao hawana nafsi yani jamii yote ya Narcisist hawana sifa za kuwa na emotion zozote wala hisia au feelings za namna yoyote je hao unawazungumziaje? Ndio mqqna kuongezeka kwa watu hawa ambao hawana nafsi imekuwa chqngqmoto kwenye jamii kuongezeka kwa matukionya kikatili kuvunjika mahusiano kama ndoa kuongezeka ka laana ya zinaa na vitu kama hivyo.
Anyway inabidi utofautishe kati ya roho (spirit) na nafsi (soul) ndio utaelewa material nilizoandika hapa. Hawa watu ambao hawana nafsi wapo sana tuu na wanaitwa empty souls au soulless beings au NPC hili linaweza kuwa jambo jipya kwako chukua muda kujiridhisha. Roho ni uhai nafsi ni utashi wa kumuongoza mtu. Ambaye hana nafsi ndio anayeweza kutumika na mapepo au demons kwa urahisi.
Sio kila binadamu ana maamuzi juu ya nafsi yake. Kuna watu hawana uwezo wa kupenda wala hawana hisia zozote na bado wanaishi kwenye jamii watu hao ndio hawana nafsi.