Utajuaje kama huna nafsi au umeuza nafsi

Utajuaje kama huna nafsi au umeuza nafsi

Utulivu wa nafsi ni mafanikio. Nitoe angalizo tuu kuwa Hii mada sio kwa ajili ya kila mtu ni kwaajili ya watu wachache sana ndio wataelewa.

Kwa mujibu wa tafiti za kiroho inathibitishwa kuwa asilimia 75 ya wakazi wa hapa duniani hawana nafsi. Ikumbukwe binadamu anakamilishwa na vitu vitatu ambavyo ni mwili, nafsi na roho. Nikisema tafiti za kiroho namanisha wenye uwezo wa kuona vitu wanaona jinsi demons au mapepo wanavyoruka kutoka ndani ya mtu mmoja na kwenda kwa mtu mwingine.

Kwa mfano mimi kuna kipindi nilikuwa nashambuliwa sana na demons au mapepo kupitia empty souls au watu wasiokuwa na nafsi ambao wanaingiliwa na mapepo bila wao kujua na kujikuta wakifanya vitu vya ajabu mbele yangu ili kunipa hofu kuwa kuna kituhakipo sawa.

Mapepo walinishambulia sana kwa kupitia watu hawa ambao hawana nafsi mfano nilikuwa nafatiliwa na watu kila niendapo, kila kazi nikifanya naharibiwa au nasambaziwa taarifa za uongo za kunichafua bila mimi kujua. Miongoni mwa vitimbi ni kukohoa ovyo kucheka ovyo na chuki za waziwazi kwa watu ninao wajua na hata nisio wajua au kufatiliwa na watu wanaovaa aina fulani za nguo lakini mwisho wa siku nilishinda mbinu za adui.

Badae nilikuja kupata Maarifa ambayo yalinifungua nikajua baadhi ya siri za ulimwengu ikiwamo baadhi ya siri za mfalme suleiman ndipo nilipojua ukweli kuhusu “Tzvarnoharno” nguvu ya Tzvarnoharno ni kubwa sana. Pale mtu anavyo pata kujifahamu yeye ni nani na asili yake ni nani huanza kushambuliwa katika ulimwengu wa roho kama wewe una roho ndogo unaweza kudhani unalogwa lakini kama ni mtu wa imani utajua ni devil yule mwovu anakujaribu.

Fanya utafiti au reseach juu ya neno “Tzvarnoharno” utajua baadhi siri za mfalme suleimani kwanini aliweza kuwamiliki majini 72 na kuyatumikisha atakavyo.

Chanzo cha binadamu/ watu kukosa nafsi ni moja ni kuzaliwa ukiwa hivyo ukiwa huna nafsi hii inaitwa glitch in the matrix na mbili ni kuuza nafsi ili uweze kutumika kama chombo (vessel/portal) na viumbe wa daraja la chini kama vijini. Mtu mwenye vijini au anayepandisha kijini huyo hana nafsi wala nguvu yoyote ya kiroho na muda wote huwa na hisia kama upepo unaingia mwilini mwake.

Kukosa nafsi kwa lugha rahisi naweza kutoa mfano wa kifaa kama Computer. Bila kuwekwa Operating system computer haiwezi kufanya kazi kwamfano huo ni kwamba ili uweze kutumia vizuri computer ni lazima uwe na Windows bila hiyo windows inakuwa computer ambaye haija kamilika.

Watoto wengi waliozaliwa kuanzia miaka ya 2000 (millennials) wengi wao hawana nafsi ni kama Bots tuu. Maisha yao ni vanity and greedy hawana uwezo wa kuchambua hoja au uwelewa wa kuwa na malengo katika maisha yao. Hawana malengo isipokuwa wachache sana ambao wamebahatikq kuzaliwa wakiwa kamili.

Katika mada zangu nimekuwa nikizungunzia kuhusu negative and positive energies. Negative energy mfano wake ni fears, worrying, hate, green, overindulge in sex, addictions drugs and cigarettes to mention the few.

Kwa upande wa positive energy mfano wake ni definite purpose in life, thinks of love, success, abundance,prosperity,courage and faithfulness to mention the few.

Katika mada zangu nimeweza kuelezea wasomaji wangu wachache kuhusiana na watu ambao ni narcissist au sociopaths ambao ni watu wenye negative energy na vilevile katika mada zangu nimweza kuzungumzia watu wema au wenye positive energy ambao ni empathetic au empaths.

Watoto wengi wanaozaliwa kipindi hichi hawana nafsi kama ukifanya uchunguzi kwa watoto tena ni rahisi sana kwa mtu anayekaa nyumba ya kupanga au uswahilini unaweza ukaona kuna watoto wa aina mbili wachoyo wenye wivu na watundu na vile vile ukaona watoto watoaji na watulivu. “ ondoa mtazamo kuwa hao ni watoto tuu” hakuna kitu kama hicho. Tabia ya mtu ni ile ya utotoni usidanganye hata kama mtoto wako anatabia hizo jua ndio hivo tena. Ndio mana wazee wwa zamani walikuwa wanauwa watoto wachanga kwani waliweza kujua kuwa huyu mtoto hana nafsi nilioewa maarifa kuhusu utamaduni wa kabila la wapare wa milimani kuna utamaduni wao unaitwa Nkumba Vana. Kwa mpare anajua hii ni nini.

Binadamu wanaozaliwa kipindi hiki hawana nafsi kwa sababu dunia kuanzia mwaka 2000 kulianza reincarnation of Souls za wafu wa miaka ya 1800-1900- mpaka mwanzoni mwa 1950 kumbuka kuwa nafsi ambazo zipo katika reincarnation cycle ni zile ambazo zilifeli mtihani wa maisha wakashindwa kufaulu mitihani yao ya maisha hivo inawabidi warudie mitihani yao ili waweze kuendelea mbele 5d au mbinguni.

Ninapo sema kila nafsi ina mtihani wa maisha mfano wake ni kama hivi unaweza kuta matatizo yako ni familia, kusalitiwa, roho mbaya, chuki, kukosa mke mume, kukosa true love au mahusiano, addiction ya madawa ya kulevya au ngono au urahibu wowote ule kwa kifupi mtihani wako wa maisha ili uwende mbinguni ni kile kitu kinachokutesa na kile kitu unachotamani kukiacha kakini huwezi. Kama Ukifabila kukamilisha hicho jua umefeli lazima urudi tena hapa duniani tena mpaka ufaulu.

Take notice kwamba hakuna dini wala maombi yatakayo kufanya uende mbinguni huo ni upigaji wa wanao mwabudu sun god au Black cube ( Saturn worship) huyu Saturn ndio Zohal mungu wa dunia hii au God of time yeye ndio mungu wa dini zote kubwa hapa duniani yeye ndio mkuu wa Matrix. God of many names. Yeye ndiye A kwa waislam na J kwa wakristo.

Kutokana na madhara makubwa ya biashara ya utumwa pamoja na vita vikuu vta dunia na machafuko roho nyingi za wanadamu ziliweza kuona ukatili mkubwa sana katika kipindi hicho na roho nyingi ilizo fia vitani au utumwani hazitaki kurudi tena duniani, ikapelekea hao watu waliofeli mitihani yao kuogopa kurudi duniani ili kurekebisha makosa yao hivyo wameamua kubaki 4d kama mizuka au nafsi za wafu na kutelekeza miili yao ambayo inazaliwa hapa duniani bila nafsi.

Baada ya kutelekeza miili yao watu wanazaliwa bila kujua wema au roho nzuri au kujali wengine.

Mtu ambaye hana nafsi atajijuaje mwenyewe au atajigundiaje? Hii ndio msingi wa mada yangu maelezo ya hapo juu ni kwa ajili ya kujenga hoja ili watu wangu waelewe nini chanzo.

Binadamu yoyote anakuwa na mwili na roho kwa kuwa na vitu hivo viwili anaweza kuonekana mkamilifu kwa kuwa anakula anakunywa na kuzungumza na anaweza hata kuzaa watoto lakini bado ndani ndani yake hajakamilika. Kwani kuna kitu kakosa ambacho ndio nakiweka bayana hapa.

Binadamu ambaye hana nafsi inamana kwenye akili au ufahamu wake hana ile internal dialog. Nikisema internal dialogue namaniaha kuwa kuna kile kisauti kipo kichwani kwako mfano ukiwa unatembea unafikiria uende wapi au ufanye nini au ukitaka kufanya kitu kibaya sauti hiyo inakupa onyo kwamba usifanye kitu hicho. Mfano ukiwa umelala au unataka kulala unaweza kuwa unawaza mawazo yako hata kama umewasha feni au redio unawaza japo kuwa kuna kelele mawazo yapo.

Mtu ambaye hana nafsi hawazi chochote isipokiwa kilichopo mbele yake wala hana utashi wa kutofautisha kati zuri na baya kwakuwa akili yake na mawazo yake yametulia muda wote huwa anakuwa na utashi wa kuwaza kitu kimoja tuu. Mfano kama anasoma hii mada atasoma tuu maandishi lakini hata waza kuwa ndani ya maandishi kuna nini au ujumbe gani. Mfano akiangalia sinema huwaza starehe ya kutazama bila kujua funzo la sinema hiyo ni nini.

Nafsi ndio operating system ya mwanadamu mtu ambaye hana nafsi anakuwa kama binadamu wa kawaida tofauti ni moja tuu hana hisia au sauti ya kumwonyesha kitu kizuri na kibaya. Anachoangalia ni jambo la kumfurahisha mwili wake na mahitaji ya kimwili tuu au kumridhisha yeye mwenyewe hawazi kuhusu wengine. Hana mahitaji ya kiroho kabisa.

Binadamu mwenye nafsi ni ngumu sana kufanya vitu kama meditation kwani mawazo yake hayapo tayari kusimamishwa ili kichwani kwake kubaki empty ili ufahamu wake uvamiwe na kiumbe kingine asicho kifahamu. Nilisha zungumzia mambo ya meditation kwenye mada ya New Age Religion.

Kwa wale wanaofanya meditation wanajua kuwa inabidi uweze kusimamisha mawazo yako yote usiweze kuwaza kitu chochote kitu ambacho ni kigumu sana kwa mtu mwenye nafsi hawezi kabisa kufanya meditation hata akijaribu ataishia kuwaza mambo yake au kupitiwa na usingizi. Mtu ambaye hana nafsi ni rahisi kufanya mesitation.

Vitu kama meditation ni hatari sana kwa mtu mwenye nafsi inaweza kusababusha ukawa kichaa kwakuruhusu ufahamu wako kuvamiwa na kiumbe usichokijua baada ya wewe ku shut down mawazo yako kichwani ukawa empty head. Ni sawa na kuingiza Virus katika mfumo wako.

Anyway kwa mtu ambaye amezaliwa hana nafsi ataishia kuwa mfuasi wa dark lord na mtu mwenye nafsi ataishia kuwa mfuasi wa Light. Mtu ambaye alikuwa na nafsi kisha akauza nafsi anaweza kuirudisha nafsi yake ila sio kwa maombi bali kwa nia yake ya dhati. Kiumbe aliyeuza nafsi anatawaliwa na asili ya hofu inabidi apambane nae as he walked in the valley of shadow of death and darkness he shall fear no evil.

Ni vigumu kuandika kila kitu hapa.

Reincrnation and past life read the book [emoji1313]View attachment 2040553
Naomba link mada ya new age religion tafadhali.
 
Mkuu sijapata exactly your point but i think The Bible is the most trustwothy book in the history of books,first there are more than 40 different authors who lived at different ages but their massage is the same.This cannot be possible unless there is divine intervention.This is one of the reasons we say The Bible is inspired by God.

Tafauti na hivi vitabu vingine vya waandishi wawili au mmoja,wanaandika mawazo yao hakuna popote pa kucompare na vitu kama hivyo.
Mkuu nakubaliana na wewe kuhusu bible...nimetoa tahadhali ya kuwa makini na mafundisho mengine,kwa mfano Mungu wa kwenye Bible na quran ni sawa according to mleta mada,.....kuna upotoshaji mwingi sana unafanyika kupitia Bible sababu imeandikwa ktk namna ya kimafumbo....mwisho wa yote giza haliwezi kuzima NURU...kuna mtu anaitwa Alister Cromwell soma historia wakati anakaribia kufa.
 
Mimi sio muumini wa theory ya creation kutoka kwenye bible au quran soma mada zangu. Wala sina cha kitu cha kunishawishi kuna kitu kinaitwa creator. Ila nachojua nipo, nilikwepo na nitaendelea kuwepo. Ukisoma
Mada zangu nilisha zungumzia chimbuko la binadamu na nikaweka wazi msimamo wangu kuwa adamu na hawa ndio creation na walikuwa wamefungiwa mahali wasichamgqnyikane na binadamu wengine wenye nafsi. Chimbuko la adamu na eva ndio hawa watu ambao hawana nafsi.
Babu kama umeamua 2+2 kuwa ni 9 basi hakuna namna tutaelewana.
 
Mkuu nakubaliana na wewe kuhusu bible...nimetoa tahadhali ya kuwa makini na mafundisho mengine,kwa mfano Mungu wa kwenye Bible na quran ni sawa according to mleta mada,.....kuna upotoshaji mwingi sana unafanyika kupitia Bible sababu imeandikwa ktk namna ya kimafumbo....mwisho wa yote giza haliwezi kuzima NURU...kuna mtu anaitwa Alister Cromwell soma historia wakati anakaribia kufa.
Pamoja kuongozi ngoja nikamsome huyo jamaa.
 
Mimi sio muumini wa theory ya creation kutoka kwenye bible au quran soma mada zangu. Wala sina cha kitu cha kunishawishi kuna kitu kinaitwa creator. Ila nachojua nipo, nilikwepo na nitaendelea kuwepo. Ukisoma
Mada zangu nilisha zungumzia chimbuko la binadamu na nikaweka wazi msimamo wangu kuwa adamu na hawa ndio creation na walikuwa wamefungiwa mahali wasichamgqnyikane na binadamu wengine wenye nafsi. Chimbuko la adamu na eva ndio hawa watu ambao hawana nafsi.

watu wengi sana hawaelewi hii falsa ya 'nipo, nilikuepo na nitaendelea kuepo'

hii ina ukweli ndani yake
 
Roho inaishi!? Tena kwenye damu!? Kwenye red blood cells au white blood cells!?
Unapokuwa unaandika vitu jaribu kidogo kuwa na elimu ya biology.

Life imeanzia kwenye level ya cell. Na cells zipo mwili mzima wa mtu na sio blood peke.

In short you don't know what you wrote.
Mkuu kwemaa!?
 
Mimi sio muumini wa theory ya creation kutoka kwenye bible au quran soma mada zangu. Wala sina cha kitu cha kunishawishi kuna kitu kinaitwa creator. Ila nachojua nipo, nilikwepo na nitaendelea kuwepo. Ukisoma
Mada zangu nilisha zungumzia chimbuko la binadamu na nikaweka wazi msimamo wangu kuwa adamu na hawa ndio creation na walikuwa wamefungiwa mahali wasichamgqnyikane na binadamu wengine wenye nafsi. Chimbuko la adamu na eva ndio hawa watu ambao hawana nafsi.
Wakati unaelezea kuhusu nafsi, sikuelewa kwakweli na nikapanga nikuulize unaongeleaje maandiko ya kiislam ya kusema "Kila nafsi itaonja mauti" je kwahiyo wasiokuwa na nafsi hawataonja umauti?

Msingi wa swali langu ulikufa baada ya wewe kusema kuwa sio muumini wa theory ya creation, kama hutojali naomba unitag Uzi wako ulio elezea mwanzo au chimbuko la mwanadamu ili nipate kujifunza kitu kipya namie
 
Hakuna mstari wa biblia unaothibitisha moja kwa moja yesu alifanya meditation ndio mana wakristu hawana huo utamaduni. Meditation ni zao la eastern religion kutoka india na mchanganyiko wa Yoga. Kama yesu alifanya meditation kanisa katoliki lazima wafiasi wake wangejua na kufanya pia kwani ndio kanisa lenye nguvu ma ndio waliomdika bible.

Nilianza kupata wasiwasi juu ya meditation baada ya kuambiwa ni kitu kizuri ila nilipo jaribu ilikiwa ngumu sana na baada ya kujaribu sana siku moja sijui ndio ilifanikiwa lakini nilipata sleep paralysis kama nimeganda nisijue kusogeza hata mkono nikahisi kuna kiumbe kinataka kuniteka. Ndipo nikagundua siri za meditation.

Nilianza kupata mashaka sana juu ya meditation ndipo nikaanza utafiti wangu. Nigagundua meditation ni agenda za new age religion ambapo ni mafundisho ya secret Cults iliupate kujua usiyo yafahamu kama remote viewing and chameling of spiritis.
Meditation ni uchawi wa teknolojia ya kisasa! Hauna tofauti na mke mchawi anaetoka na kwenda kuwanga mtaani huku akionekana bado yupo kitandani kalala na mumewe!
 
Baada ya kusoma ishu za meditation huku JamiiForums nikataka na mimi niijaribu.
Sitosahau ile siku, nilihisi kuchanganyikiwa kabisa na Ilinichukua karibu wiki moja kurudi kwenye hali yangu ya kawaida.
Usijaribu jaribu tu yale mambo ni ya kichawi unaweza ukafa ukiwa hai kwa kujigeuza msukule! Wachawi hawana nafsi ndio maana kwao ni simple
 
Tuanze na material ambayo yapo relevant kwako mfano kitabu cha biblia Marko 8:36 kinasema For what shall it profit a man, if he shall gain the whole world, and lose his own soul? Hii kwanza inakufundisha mtu anaweza kuishi bila nafsi na akafanikiwa kwemye mambo ya kidunia kwa kupitia kutesa mwengine. Nafsi ni ile sauti inayoishi ndani kwako haisuhiani kabisa na uhai wako. Kuna watu hawana internal dialog sema ni ngumu sana kukubali juu ya hili na wengine kwa kiupitia hii mada wamejua wapo katka kundi gani.

Uhai wa mwanadamu upo kwenye damu tuu ndio mana unapaswa kujua kuwa roho inaishi kwenye damu. Katika maisha ya kibinadamu mambo mengi yamefichwa kwa kigezo cha kutokuamini ukweli kwani truth is stranger than finction.

Sociopaths na psychopaths are soulless being au ni aina fulani ya watu ambao hawana nafsi yani jamii yote ya Narcisist hawana sifa za kuwa na emotion zozote wala hisia au feelings za namna yoyote je hao unawazungumziaje? Ndio mqqna kuongezeka kwa watu hawa ambao hawana nafsi imekuwa chqngqmoto kwenye jamii kuongezeka kwa matukionya kikatili kuvunjika mahusiano kama ndoa kuongezeka ka laana ya zinaa na vitu kama hivyo.

Anyway inabidi utofautishe kati ya roho (spirit) na nafsi (soul) ndio utaelewa material nilizoandika hapa. Hawa watu ambao hawana nafsi wapo sana tuu na wanaitwa empty souls au soulless beings au NPC hili linaweza kuwa jambo jipya kwako chukua muda kujiridhisha. Roho ni uhai nafsi ni utashi wa kumuongoza mtu. Ambaye hana nafsi ndio anayeweza kutumika na mapepo au demons kwa urahisi.

Sio kila binadamu ana maamuzi juu ya nafsi yake. Kuna watu hawana uwezo wa kupenda wala hawana hisia zozote na bado wanaishi kwenye jamii watu hao ndio hawana nafsi.
Watu wote ambao wanaturusha hela zetu hawana nafsi! We kama ulikopa na ukadhamiria kutorudisha hela huna nafsi😅
 
Mpaka sasa ninashindwa kuelewa hiyi Khali hutokana na ni nn kuna muda ninakuwa na uwezo wa kugundua hata mtu anae taka kufa mwezi ujao na hatua ya kwanza huwa napiga nae sana stori na kumuhaid kesho yake ningeweza kuja lakini huwa haiw hvy kila nikijaribu kutaka kukutana nae hujikuta sipat muda baada ya mwezi utasikia jamaa kafa imetokea zaid ya watu 9 had kufikia 2020 mwishon hawa wa mwisho nilikuwa nawachana kimafumbo inawezekana huu ndio ukawa mwanzo na mwisho wa kukutana

Suala lingine huwa nikiwa na hisia za kukutana na viongozi wakubwa usiku nikilala hupiga nao stori na mfano magu Kikwete nk na juz samia ila niligombana nae sana sikuelewa kwann huyu nikiota hujikuta nagombana nae

Mambo ni mengi ila haya ni kwa uchache
Mkuu hili lina uhusiano gani kwenye haya mambo
Duh mzee huwa ni kweli hayo unayosema? 😅 Naona watu wamepita kimya kimya kwa kuogopa miadi na wewe!
 
Mimi ninapingana na wewe kabisa. Kwanza Wacha nikuambie tu kuwa huo ni ufunuo wa kuzimu unao .

Mtume Paulo kasema hivi
Ijapokuwa tunaenenda katika mwili hatufanyi vita Kwa jinsi ya mwili lakini silaha zetu Zina nguvu katika Mungu hata kuangusha ngome,(mawazo) na chochote kinachojiinua kinyume na Elimu ya Mungu ili Kila fikra zipate kumtii Kristo.

Mfalme Daudi anasema Mungu huihuisha nafsi yangu na kuiongoza

In short nikuambie tu kuwa hakuna mtu Hana nafsi ila Kuna nafsi zilizokaa vifungoni, zilizochoka, zilizokufa ila zipo ndio maana mtu akihuburiwa injili neno la Mungu linaingia tofauti na siku zingine alikuwa anahubiriwa ghafla anasikia hukumu ndani akiongozwa Sala ya Toba anapata amani ya ajabu kabisa
Hiyo Amani huku Dunia haipatikani inaletwa na Mungu mwenyewe ndani ya mtu

So Kuna watu Kwa sababu wamemkataa Mungu wanataka watufundishe Elimu za mizimu

Ndio maana hapo juu mtume Paulo anasema Chochote kinachojiinua kinyume na Elimu ya Mungu
Kila fikra zimtii Kristo

Sasa hapa umetuletea Elimu nyingine tofauti na ya Kristo
Haikubaliki hiii
Kristo ndie Kweli yote na anatutakasa na Neno lake
Haya mengine ni ya kukataa
Ni mafunuo ya kuzimu
 
Wakati unaelezea kuhusu nafsi, sikuelewa kwakweli na nikapanga nikuulize unaongeleaje maandiko ya kiislam ya kusema "Kila nafsi itaonja mauti" je kwahiyo wasiokuwa na nafsi hawataonja umauti?

Msingi wa swali langu ulikufa baada ya wewe kusema kuwa sio muumini wa theory ya creation, kama hutojali naomba unitag Uzi wako ulio elezea mwanzo au chimbuko la mwanadamu ili nipate kujifunza kitu kipya namie

Labda kwa kukujibu tu ni kwamba huo mstari ni kwaajili ya kutengenezea watu wenye nafsi hofu. Kufa lazima kila mtu afe lakini sio mauti. Kuna tofauti kati ya kufa na kuonja mauti.

Watu wenye nafsi pindi wakifa wana option ya reincarnation kurekebisha makosa yao na watu ambao hawana nafsi hawawezi kuwa na nafasi ya reincarnation wanapokufa na story yao inaisha.. Nita ku tag
 
Wewe unamuamini Mungu au una mambo mengine?
 
Duhhh nimepata kitu kingine tena hapa cha kutaka kufahamu, tofauti ya kifo na mauti, kama hutojali kwa ufupi tu nipe elimu mkuu juu ya utofauti wa hayo maneno mawili ambayo kwa kawaida yanatumika kwa mfanano katika jamii zetu

Pia usihahau kuni tag Uzi wako Mkuu
 
Wewe unamuamini Mungu au una mambo mengine?

Aliye juu zaidi au Most High ndio ninaye fata sheria zake na haisuhiani na kuamini. Kuamini unaweza kuamininkitu chochote na ukajiona upo sawa lakini ukifata sheria huna haja ya kuamini kwakuwa sheria zipo. Mungu aliyejuu zaidi ni Sheria zinazoongoza na kushikilia ulimwengu wote.
 
Duhhh nimepata kitu kingine tena hapa cha kutaka kufahamu, tofauti ya kifo na mauti, kama hutojali kwa ufupi tu nipe elimu mkuu juu ya utofauti wa hayo maneno mawili ambayo kwa kawaida yanatumika kwa mfanano katika jamii zetu

Pia usihahau kuni tag Uzi wako Mkuu

Neno mauti limetokana na neno sakratil maut la kiarabu likiashiria uchungu na mateso pale mtu anapokufa. Kiukweli binadamu hana haja ya kuogopa kufa wala kifo hakina uchungu wowote ni malango wa kwenda dimension nyingine au time line nyingine. Neno hilo linatumika kuwapa binadamu hofu juu ya kifo na ili uweze kuwq binadamu uliyekamilika uende mbiguni unatakiwa usiwe na hofu na moyonwako uwe mwepesi kama wa mtoto wala hutakiwi kuogopa kiumbe yoyote kwani unachokiogopa kitakutawala.
 
Okay, pamoja mkuu nimekupata
 
Back
Top Bottom