Utajuaje kama huna nafsi au umeuza nafsi

Naomba link mada ya new age religion tafadhali.
 
Mkuu nakubaliana na wewe kuhusu bible...nimetoa tahadhali ya kuwa makini na mafundisho mengine,kwa mfano Mungu wa kwenye Bible na quran ni sawa according to mleta mada,.....kuna upotoshaji mwingi sana unafanyika kupitia Bible sababu imeandikwa ktk namna ya kimafumbo....mwisho wa yote giza haliwezi kuzima NURU...kuna mtu anaitwa Alister Cromwell soma historia wakati anakaribia kufa.
 
Babu kama umeamua 2+2 kuwa ni 9 basi hakuna namna tutaelewana.
 
Pamoja kuongozi ngoja nikamsome huyo jamaa.
 

watu wengi sana hawaelewi hii falsa ya 'nipo, nilikuepo na nitaendelea kuepo'

hii ina ukweli ndani yake
 
Mkuu kwemaa!?
 
Wakati unaelezea kuhusu nafsi, sikuelewa kwakweli na nikapanga nikuulize unaongeleaje maandiko ya kiislam ya kusema "Kila nafsi itaonja mauti" je kwahiyo wasiokuwa na nafsi hawataonja umauti?

Msingi wa swali langu ulikufa baada ya wewe kusema kuwa sio muumini wa theory ya creation, kama hutojali naomba unitag Uzi wako ulio elezea mwanzo au chimbuko la mwanadamu ili nipate kujifunza kitu kipya namie
 
Meditation ni uchawi wa teknolojia ya kisasa! Hauna tofauti na mke mchawi anaetoka na kwenda kuwanga mtaani huku akionekana bado yupo kitandani kalala na mumewe!
 
Baada ya kusoma ishu za meditation huku JamiiForums nikataka na mimi niijaribu.
Sitosahau ile siku, nilihisi kuchanganyikiwa kabisa na Ilinichukua karibu wiki moja kurudi kwenye hali yangu ya kawaida.
Usijaribu jaribu tu yale mambo ni ya kichawi unaweza ukafa ukiwa hai kwa kujigeuza msukule! Wachawi hawana nafsi ndio maana kwao ni simple
 
Watu wote ambao wanaturusha hela zetu hawana nafsi! We kama ulikopa na ukadhamiria kutorudisha hela huna nafsi😅
 
Duh mzee huwa ni kweli hayo unayosema? 😅 Naona watu wamepita kimya kimya kwa kuogopa miadi na wewe!
 
Mimi ninapingana na wewe kabisa. Kwanza Wacha nikuambie tu kuwa huo ni ufunuo wa kuzimu unao .

Mtume Paulo kasema hivi
Ijapokuwa tunaenenda katika mwili hatufanyi vita Kwa jinsi ya mwili lakini silaha zetu Zina nguvu katika Mungu hata kuangusha ngome,(mawazo) na chochote kinachojiinua kinyume na Elimu ya Mungu ili Kila fikra zipate kumtii Kristo.

Mfalme Daudi anasema Mungu huihuisha nafsi yangu na kuiongoza

In short nikuambie tu kuwa hakuna mtu Hana nafsi ila Kuna nafsi zilizokaa vifungoni, zilizochoka, zilizokufa ila zipo ndio maana mtu akihuburiwa injili neno la Mungu linaingia tofauti na siku zingine alikuwa anahubiriwa ghafla anasikia hukumu ndani akiongozwa Sala ya Toba anapata amani ya ajabu kabisa
Hiyo Amani huku Dunia haipatikani inaletwa na Mungu mwenyewe ndani ya mtu

So Kuna watu Kwa sababu wamemkataa Mungu wanataka watufundishe Elimu za mizimu

Ndio maana hapo juu mtume Paulo anasema Chochote kinachojiinua kinyume na Elimu ya Mungu
Kila fikra zimtii Kristo

Sasa hapa umetuletea Elimu nyingine tofauti na ya Kristo
Haikubaliki hiii
Kristo ndie Kweli yote na anatutakasa na Neno lake
Haya mengine ni ya kukataa
Ni mafunuo ya kuzimu
 

Labda kwa kukujibu tu ni kwamba huo mstari ni kwaajili ya kutengenezea watu wenye nafsi hofu. Kufa lazima kila mtu afe lakini sio mauti. Kuna tofauti kati ya kufa na kuonja mauti.

Watu wenye nafsi pindi wakifa wana option ya reincarnation kurekebisha makosa yao na watu ambao hawana nafsi hawawezi kuwa na nafasi ya reincarnation wanapokufa na story yao inaisha.. Nita ku tag
 
Wewe unamuamini Mungu au una mambo mengine?
 
Duhhh nimepata kitu kingine tena hapa cha kutaka kufahamu, tofauti ya kifo na mauti, kama hutojali kwa ufupi tu nipe elimu mkuu juu ya utofauti wa hayo maneno mawili ambayo kwa kawaida yanatumika kwa mfanano katika jamii zetu

Pia usihahau kuni tag Uzi wako Mkuu
 
Wewe unamuamini Mungu au una mambo mengine?

Aliye juu zaidi au Most High ndio ninaye fata sheria zake na haisuhiani na kuamini. Kuamini unaweza kuamininkitu chochote na ukajiona upo sawa lakini ukifata sheria huna haja ya kuamini kwakuwa sheria zipo. Mungu aliyejuu zaidi ni Sheria zinazoongoza na kushikilia ulimwengu wote.
 

Neno mauti limetokana na neno sakratil maut la kiarabu likiashiria uchungu na mateso pale mtu anapokufa. Kiukweli binadamu hana haja ya kuogopa kufa wala kifo hakina uchungu wowote ni malango wa kwenda dimension nyingine au time line nyingine. Neno hilo linatumika kuwapa binadamu hofu juu ya kifo na ili uweze kuwq binadamu uliyekamilika uende mbiguni unatakiwa usiwe na hofu na moyonwako uwe mwepesi kama wa mtoto wala hutakiwi kuogopa kiumbe yoyote kwani unachokiogopa kitakutawala.
 
Okay, pamoja mkuu nimekupata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…