Utakapo kufa leo unadhani members wenzako wa jf watajua au ndio ile fulani mbona haonekani hewani?

Utakapo kufa leo unadhani members wenzako wa jf watajua au ndio ile fulani mbona haonekani hewani?

Nianze kwa habari hii, kuna mama mmoja alikuwa pale TRA tawi la Kinondoni,alikuwa mama poa sana,ukienda pale kufanya makadirio huwa anakupa ushirikiano mzur sana na mwisho wa siku mambo yanakuwa sawa.

Kama Miaka miwili au mitatu iliyopita nilimtafuta kwenye call kutaka kumuuliza jambo fulani,nikavuta waya mara paap! Inasikika sauti ya kiume na kunipa taarifa kwamba mama fulani amefariki kwa Kansa ya damu,duh nilihuzunika sana kwakweli.

Sasa je wewe ukivuta chaap! Je kuna mdau wowote wa jf ambaye anaweza sema wadau Ertugrul bey hatupo naye tena!!!

Kwa upande wangu nina best yangu wa kike humu ambaye ndiye pekee nina mawasiliano naye,huwa tunatafutana ingawa sio mara kwa mara lakini ni washikaji,naamini siku akivuta waya kunicheki akiambiwa huyu mwamba ametangulia akhera naamini atawapa habari,lau katangulia yeye siku nikavuta waya ntaambiwa best yako is no more alive,ntaweka ubaoni tangazo,though namtakia umri mrefu zaidi yeye pamoja na mimi

Best yangu mshikaji wangu wa nguvu najua ukisoma post hii utajua nakuzungumzia wewe,nakupenda sana mtu wangu.


Vipi kuhusu wewe?​

Ni hayo tu!​

Ngoja niulize waliokufa ntarudi kuwapa mrejesho
 
Au ndio ile haonekani hewani.. na watu wanamzka hewani hewani.. kumuulizia tu rambirambi tosha..
 
Ikitokea nimekufa leo member pekee atakayejua ni baba mtoto wangu. Nina rafiki mwingine ambae tuna mawasiliano ya ON and OFF kiasi sina uhakika kama atajua kwamba trudie hatunaye tunaweza ghostiana hata miezi 3 bila kujualiana hali.
 
Back
Top Bottom