Mfano msani A ameenda kufanya shoo. Mtu anataka kumtumia kitakatisha fedha. Huyo mtu atamlipa kiasi cha fedha labda bilioni mbili ambazo kimsingi hazilingani na thamani ya shoo hiyo.
Hiyo bilioni mbili ni fedha chafu. Kwahiyo ataingiza kwenye akaunti ya msani A. So hela itaingia benki( mfumo rasmi wa fedha) hapa tayari fedha chafu imeingia kwenye mfumo Ili iwe safi. Baada ya muda msani yule ataenda kwa mfano kununua apartment, mabasi ya biashara, malori na kadharika kutokana na fedha Ile na ikiwa imetokea benki. Hapa fedha tayari imetakakata na imeingia kwenye mzunguko rasmi. Sasa kwenye kununua vitu hivyo wao msani A na mhusika watajua wanafanyaje.