Utakatishaji Fedha, Biashara inayoendelea kwa Siri kubwa

Utakatishaji Fedha, Biashara inayoendelea kwa Siri kubwa

Na hivi ndivyo nijuavyo kwamba pesa yoyote ambayo inapatikana katika shughuli zilizo nnje ya sheria za nchi na pengine kidunia ndio huwekwa kwenye huo upande wa kuwa pesa haramu ila wahusika mara nyingi huwa wanazitafutia sababu ya kuzitakasa ili zionekane safi.

Sasa kitu ambacho kidogo kimeniyumbisha kwenye hilo bandiko ni kwamba mfano wa watu wa makanisa kwamba kwa mujibu wa andiko kile wanachokifanya sicho kinachowaingizia pesa ila wanatumia hiyo njia ili iwe ya utakaso wa hizo fedha walizo nazo.

Hapa ndio amenichanganya mimi kwa sababu hadi sasa kuna pastor alikua na kanisa lake huko buza na alikua anaombea watu kwa laki tano na watu wanakiri kwamba walikua wanatoa hizo fedha na bado kuna mmoja alijaza ule uwanja wa pale kawe na akauza sana maji na mafuta plus sadaka na mengine yote ambayo yaliyofanyika usiku ule kuhamisha pesa kutoka kwenye mifuko ya watu kwenda kwakwe.

Hapa ndipo nnapohitaji connection ya hilo andiko na utakatishaji.

Yaani anawezaje kuprove kwamba hawa watu hawapati pesa kupitia hizo njia ila zipo njia haram za upatikanaji wa pesa zao hasa ukizingatia uwingi wa wafuasi ambao wamejizolea kwenye hayo maeneo yao ya kazi.
Ni rahisi mbona kufanya money laundering Kwa dini , si Una declare Tu kuwa hata ni mapato yatokanayo na sadaka za waumini ?
Na hiyo pesa ina
Mtu akiwa na njaa anachukia sana matajiri tafuta pesa na wewe utakula tu
Acha ukilaza wako ,haya mambo yapo sana. Wewe ukisikia shell companies na offshore bank accounts kule Switzerland ,Cyprus , seacheylles , Panama nk unadhani ni utani ?
Mpaka kanisa katoliki wanafanya hii kitu miaka mingi .
Makampuni makubwa na watu matajiri nk
Ulimwengu hauko kama unavyoaminishwa
 
Mfano msani A ameenda kufanya shoo. Mtu anataka kumtumia kitakatisha fedha. Huyo mtu atamlipa kiasi cha fedha labda bilioni mbili ambazo kimsingi hazilingani na thamani ya shoo hiyo.
Hiyo bilioni mbili ni fedha chafu. Kwahiyo ataingiza kwenye akaunti ya msani A. So hela itaingia benki( mfumo rasmi wa fedha) hapa tayari fedha chafu imeingia kwenye mfumo Ili iwe safi. Baada ya muda msani yule ataenda kwa mfano kununua apartment, mabasi ya biashara, malori na kadharika kutokana na fedha Ile na ikiwa imetokea benki. Hapa fedha tayari imetakakata na imeingia kwenye mzunguko rasmi. Sasa kwenye kununua vitu hivyo wao msani A na mhusika watajua wanafanyaje.
Dah bora umewasaidia hivi vichwa ni vigumu kuelewa sana .
 
Ni rahisi mbona kufanya money laundering Kwa dini , si Una declare Tu kuwa hata ni mapato yatokanayo na sadaka za waumini ?
Na hiyo pesa ina
Yeah hii nakubaliana na wewe kwamba kufanya hiyo kitu inaweza kufanyika na watu hao ila sio kuundergrade ule ukwasi wanaojikusanyia kupitia hicho wafanyacho... wanapiga sana pesa kupitia upande huo.
 
Show room za magari na maduka kama ya simu maduka ya nguo ndio cover kubwa ya kutakatisha pesa.

Inshort mtu anakuaminisha kwa macho source of income yake ni hii lakini ana issue zake nyuma ya pazia.

Ndio maana kuna watu hawaweki pesa bank wanakaa na cash ndani, Magufuli alidhurumu sana pesa za watu kwa kisingio hicho, na kesi yake ni uhujumu uchumi haina dhamana.
 
Mkuu mbona huu Uzi kama umekugusa sana.
Maana una makasiriko sana.
Mkuu mbona huu Uzi kama umekugusa sana.
Maana una makasiriko sana
Hii biashara ni hatari kuliko madawa ya kulevya. Leo hii mtu anajipost na millions of money na serikali imekaa kimya. Kipindi cha nyerere watu walikuwa wanaogopa hata kununua blue band. Wataulizwa hela wametoa wapi.
 
Utakatishaji fedha ni mchakato wa kufanya fedha au mali zilizopatikana kwa njia haramu kuonekana kama zimepatikana kwa njia halali. Lengo la utakatishaji fedha ni kuficha chanzo cha fedha hizo ili zisiweze kuhusishwa na uhalifu.

Utakatishaji fedha unahusisha michakato mikuu mitatu kuu. Hapa kuna ufafanuzi wa kila mchakato pamoja na mbinu zake:

1. Mchakato wa Kwanza (Placement)

Huu ni hatua ya kwanza ambapo fedha haramu zinaingizwa kwenye mfumo wa kifedha. Lengo ni kutoa fedha hizo kutoka kwenye chanzo chake cha uhalifu.

Mbinu za Kuweka:

  • Biashara za Kivyake: Kutumia biashara kama migahawa, salon, au maduka ya rejareja kuingiza fedha kama mauzo halali.
  • Mauzo ya Pesa za Kigeni: Kununua fedha za kigeni na kisha kuziuza ili kupata fedha halali.
  • Deposit za Kiwango Kidogo: Kuweka fedha kidogo kwenye akaunti za benki ili kuepuka uangalizi wa benki.

2. Mchakato wa Pili (Layering)

Katika hatua hii, lengo ni kuficha uhusiano kati ya fedha na chanzo chake. Hii inafanywa kwa kutoa fedha hizo katika mfumo wa muamala wa kifedha.

Mbinu za Layering:

  • Kutumia Akaunti Nyingi: Kuhamisha fedha kati ya akaunti tofauti za benki, mara nyingi ndani na nje ya nchi.
  • Muamala wa Zana za Fedha: Kutumia bidhaa za kifedha kama hisa, dhamana, au bidhaa za biashara.
  • Kufanya Muamala wa Kigeni: Kupeleka fedha kwenye nchi zenye sheria dhaifu za fedha.

3. Mchakato wa Tatu (Integration)

Huu ni hatua ya mwisho ambapo fedha hizo zinarejeshwa kwenye mfumo wa kifedha kama fedha halali. Mchakato huu unawawezesha wahalifu kutumia fedha hizo bila ya kudhaniwa.

Mbinu za Ujumuishaji/integration:

  • Kuanzisha Biashara Halali na kuingiza fedha za utakatishaji kama mtaji.
  • Kununua mali kama nyumba, magari, au sanaa, ambayo yanaweza kuonekana kama uwekezaji wa halali.
  • Mifumo ya Uhamishaji wa Fedha: Kutumia huduma za uhamishaji fedha za kigeni kuhamasisha fedha hizo.
Utakatishaji fedha ni mchakato wa tata na unatumia mbinu nyingi za uhalifu.
 
Show room za magari na maduka kama ya simu maduka ya nguo ndio cover kubwa ya kutakatisha pesa.

Inshort mtu anakuaminisha kwa macho source of income yake ni hii lakini ana issue zake nyuma ya pazia.

Ndio maana kuna watu hawaweki pesa bank wanakaa na cash ndani, Magufuli alidhurumu sana pesa za watu kwa kisingio hicho, na kesi yake ni uhujumu uchumi haina dhamana.
Maduka ya Cm, nguo, viatu, etc.
Jamani ukijaribu kufuatilia kwa undani unachokaa kabisaa. Lol
 
Hivi unajua vizuri Money laundering? (Utakatishaji wa pesa) uko je au unadhani kila mwenye pesa nyingi ni mtakatishaji fedha.......unajua watanzania tuna pewa misamihati mikubwa wakati elimu yetu na uelewa wetu uko chini, kisa tuna kipaji cha kuongea hata taka taka.
Case closed!!!
Elimu yetu haituruhusu hata kuujadili Muungano wetu.
 
Habari wadau!

Naenda kwenye hoja moja kwa moja kwenye hoja.

Ki ukweli utakatishaji fedha ni biashara ambayo ipo kwa siri sana.

Usione mtu anajipost na rundo la hela na hana kazi yeyote akasema yeye ni free mason ukaamini we ni mjinga hata serikali ina ujinga flani.

Kuna watu wana hela Dunian hapa hela chafu ambayo inahitaji kuwa katika system sehemu sahihi ya kutakatisha ni Africa.

Usione msanii analipwa milioni 300 ya kibongo kwa shoo ya watu 20 uko nje ukasema amepata bingo.

Leo hii kuna companies wanakopesha hela kisa una Nida Number siamini kama kweli wanapata faida.

Wachungaji feki wa kutosha wana hela hatari. Ukiuliza wanauza maji na mafuta au baraka ndo wanapata hizo hela.

Jichanganye ukiamini utatoboa kama hamna source ya hizo hela.

Watakatishaji fedha wakubwa duniani ni

1. Drug dealers.
2. Wanasiasa
3. Wafanyabiashara.
4. Wanamichezo.
5. Wasanii. (wanamuziki na wacheza filamu.)
6. Kamali.

Ongeza yako unayoyajua katika hili!!!!!!
Sina hakika ila kuna mahali ukiona dots haziungiki kabisa, unakuta duka lipo tu visendo na vicover vya simu au nguo za uongo na ukweli kadhaa

kukuta mteja ni kwa kutafuta kwa tochi ila lipo miaka nenda rudi kwenye eneo frame ni ya 500 mpaka 800+ unabaki tu eeh hapa Return of investment inarudije hupati jibu


Hizi utaziona sana Sinza Sinza, Makumbusho na maeneo mengine ya mjini
 
Sina hakika ila kuna mahali ukiona dots haziungiki kabisa, unakuta duka lipo tu visendo na vicover vya simu au nguo za uongo na ukweli kadhaa

kukuta mteja ni kwa kutafuta kwa tochi ila lipo miaka nenda rudi kwenye eneo frame ni ya 500 mpaka 800+ unabaki tu eeh hapa Return of investment inarudije hupati jibu


Hizi utaziona sana Sinza Sinza, Makumbusho na maeneo mengine ya mjini
Hujui biashara inavo oparate maduka mengine ni ofisi ya kukutana mzigo uko store unakua derivered na gari popote, unajua nyie mnakalilishwa, kwasbb hamna pesa mnadhani kila alio nazo alitakatisha tu, nyie akili finyu sanaa
 
Back
Top Bottom