Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
🤣🤣🤣🤣🤣 wanazunguka zunguka tu ukute na wao hawajui kama mimi🙆♀️Sasa mnaojua si ndio mtoe shule hapa watu tujifunze
Hii ndo jf aisee,,mtu anasema kitu sio,haya badala ya kutufahamisha anapiga kimya,hatar sana🤣🤣🤣🤣🤣 wanazunguka zunguka tu ukute na wao hawajui kama mimi🙆♀️
Wewe umeshawahi kutakatisha?Habari wadau!
Naenda kwenye hoja moja kwa moja kwenye hoja.
Ki ukweli utakatishaji fedha ni biashara ambayo ipo kwa siri sana.
Usione mtu anajipost na rundo la hela na hana kazi yeyote akasema yeye ni free mason ukaamini we ni mjinga hata serikali ina ujinga flani.
Kuna watu wana hela Dunian hapa hela chafu ambayo inahitaji kuwa katika system sehemu sahihi ya kutakatisha ni Africa.
Usione msanii analipwa milioni 300 ya kibongo kwa shoo ya watu 20 uko nje ukasema amepata bingo.
Leo hii kuna companies wanakopesha hela kisa una Nida Number siamini kama kweli wanapata faida.
Wachungaji feki wa kutosha wana hela hatari. Ukiuliza wanauza maji na mafuta au baraka ndo wanapata hizo hela.
Jichanganye ukiamini utatoboa kama hamna source ya hizo hela.
Watakatishaji fedha wakubwa duniani ni
1. Drug dealers.
2. Wanasiasa
3. Wafanyabiashara.
4. Wanamichezo.
5. Wasanii. (wanamuziki na wacheza filamu.)
6. Kamali.
Ongeza yako unayoyajua katika hili!!!!!!
Wewe umethibitisha ulichoongea maana pia umeandika taka taka na jinsi gani kichwa chako kilivyo na akili mbovu kuwahi kutokea.Hivi unajua vizuri Money laundering? (Utakatishaji wa pesa) uko je au unadhani kila mwenye pesa nyingi ni mtakatishaji fedha.......unajua watanzania tuna pewa misamihati mikubwa wakati elimu yetu na uelewa wetu uko chini, kisa tuna kipaji cha kuongea hata taka taka.
Umesema vyema ila kuna watu leo hii nchini wanatumika kutakatisha fedha na serikali ipo kimya. Mtu anaonyesha hela kwenye mtandao akidanganya watu yeye ni free madonMtoa post unaonekana hujui maana ya Utakatishaji fenda ni Kuitoa pesa chafu ambayo ilipatikana visivyo halali eg wizi uwe wa serikalini au ujambazi au hela uliyoipata visivyo halali na kwa vile ni nyingi unataka isikae mkononi mwako iwe kwenye mzunguko ili ufaidike baada ukiwa nayo watu wajue uliipata kwa biashara isionekane kuwa uliipata kwa njia isiyo halali serikali ijue kuws chanzo cha mapato yako ni ile biashara na sio vinginevyo.
NdioKwahiyo fisadi moja serikalini akinunua ma basi ya abiria kutokana na pesa ya rushwa au hongo huo ni utakatishaji wa pesa??
Yah casino ni biashara halali kisheriaMbona hayana uwiano hayo, na utakatishaji pesa.......
Sasa unahitaji taaluma ya ujasusi kweli hapo kubaini kuwa kuna mianya ya kutakatisha pesa za watu wengine? Au hata zake alizotengeneza kwenye Illegal business zake nyingine?Na hivi ndivyo nijuavyo kwamba pesa yoyote ambayo inapatikana katika shughuli zilizo nnje ya sheria za nchi na pengine kidunia ndio huwekwa kwenye huo upande wa kuwa pesa haramu ila wahusika mara nyingi huwa wanazitafutia sababu ya kuzitakasa ili zionekane safi.
Sasa kitu ambacho kidogo kimeniyumbisha kwenye hilo bandiko ni kwamba mfano wa watu wa makanisa kwamba kwa mujibu wa andiko kile wanachokifanya sicho kinachowaingizia pesa ila wanatumia hiyo njia ili iwe ya utakaso wa hizo fedha walizo nazo.
Hapa ndio amenichanganya mimi kwa sababu hadi sasa kuna pastor alikua na kanisa lake huko buza na alikua anaombea watu kwa laki tano na watu wanakiri kwamba walikua wanatoa hizo fedha na bado kuna mmoja alijaza ule uwanja wa pale kawe na akauza sana maji na mafuta plus sadaka na mengine yote ambayo yaliyofanyika usiku ule kuhamisha pesa kutoka kwenye mifuko ya watu kwenda kwakwe.
Hapa ndipo nnapohitaji connection ya hilo andiko na utakatishaji.
Yaani anawezaje kuprove kwamba hawa watu hawapati pesa kupitia hizo njia ila zipo njia haram za upatikanaji wa pesa zao hasa ukizingatia uwingi wa wafuasi ambao wamejizolea kwenye hayo maeneo yao ya kazi.
Bank moja ulaya Hongkong and Shanghai Banking Corporation Limited walipigwa fain ya 1.9 b usd kwa kusindwa kuwazuia CARTEL WAKUBWA WA COLOMBIA NA MEXICO ku launder hela kupitia hiyo benk, KIMSING WAUZA MADAWA WANAONGOZA KWA SHUGHULI YA KUTAKATISHA FEDHA, mleta mada hajakosea wakuu, Top ten money laundering scheme in histori ina Wauza Ngada wengi kuliko watu wengine wowote.Drug dealer hatakiwi kuwepo hapa
Watu wengi hawajui money laundering ni nini, wanaropoka tu, mtoa mada hajakosea hata kama hajasema exaclty jinsi gani watu wanatakatisha fedhaWatu wengi wana criticise hali ya kuwa mtoa post yuko sahihi
Umepata hela chafu unaenda kuinunua nyumba alafu unakaa after sometime unaiuza tena ile nyumba then hii hela inakuwa justifiable hata ukiulizwa umepata wapi pesa unasema uliuza nyumba ilokuwa yako, kuna stail nyingi za kutakatisha fedha. Nakumbuka kuna jamaa alikujaga hapa jukwaani kuuliza namba ya kuvusha dolla laki 9 kama sio M1 kuja tanzania kutoka marekan sababu hawez weka hiyo hela benk na hawez kusafiri nayo akawa anataka apewe mawazo ya namna gani hiyo fedha ataifikisha bongo land kwa namna yeyote, ukisoma ule uzi ndio utajua watu wanavyosafisha fedha aiseeKutakatisha pesa ni kitendo cha kuchukua pesa iliyopatikana kwa njia haramu(madawa, wizi,utapeli etc)kisha kuiingiza kwenye mfumo,biashara halali inayotambulika kisheria.
Mfano labda tuseme mimi ninafanya biashara ya madawa ya kulevya, pesa nitakayoipata baada ya kufanya biashara ya madawa ya kulevya niende nikafungue showroom ya kuuza magari, so kila ninapouza madawa nachukua pesa naenda kuongeza magari huo ndio utakatishaji. Wengine ongezeeni
Babe!!!🤣🤣🤣🤣🤣 wanazunguka zunguka tu ukute na wao hawajui kama mimi🙆♀️