Utamaduni huu wa kunywa maji ya chupa nyumbani unanitesa

1.5Lt ni 1000 nchi nzima unless uwende zile 3-5* places. Wameshusha labda wameongeza vyanzo vya upatikanaji wa maji πŸ˜€πŸ˜€
Basi Zenji wanatuuzia bei za kitalii, ilikuwa maji ya Kilimanjaro unayapata baadhi tu ya maduka na pack yake ipo kwenye boxes. Sema siku nyingi sijayanunua. Nakunywa Drop of Zanzibar au Dew drop. Ila nikiwa home zaidi natumia maji ya bomba
 
Maji mazuri ni ya kuchemsha mwenyewe, kunywa maji ya chupa ni arrogance ya elite class wage earners.
Na mimi nilitaka kumwambia hivyo hivyo. Tena haya maji ya chupa ya siku hizi Bongo yanaweza kuwa hatari kuliko kunywa ya bombani bila kuchemsha. Mimi maji nayopenda ni yale ya kuchemsha kwa kuni, halafu yanakuwa na mwonjo wa moshi kwa mbali... ukiweza kuzingatia usafi wakati wa kuchemsha ni mazuri sana.
 
Maji ya kilimanjaro ya ladha mbaya kama magadi, bora Uhai na Dew drop.
Unywaji wa maji ya chupa nyumbani ni dalili ya kuwa na kipato kizuri/kuwa mgonjwa mgonjwa.
Uhai kwangu ndiyo mabaya kuliko maji mengine.
 
Hahahaha nayaonaga tuu mzee πŸ˜‚ me maji ya viwandani ya moto Yana ladha ya hovyo, ya baridii ndo yananipa tonsils

Ko napiga dawasa baridii safi ya asili....
Maji baridi hayasababishi matezi. Naua kuna watu wengi sana huwa wanasema hivyo lakini ukweli ni kwamba matezi yanasababishwa na aidha maabukizi ya virus au bakteria. Japo naweza kusema ukiwa unaumwa matezi na ukinywa maji baridi unaweza kupata maumivu.
 
Mfano Mimi feni wala maji ya baridii situmii iwe ya Bomba au kiwandani vyote hivyo napata homa kwann ?
 
Kweli? Mimi nikila ice cream, juice na maji baridi kesho yake au jioni ya hiyo siku nina tonsils.
 
Si uchemse maji au vipi
 
Mfano Mimi feni wala maji ya baridii situmii iwe ya Bomba au kiwandani vyote hivyo napata homa kwann ?
Inawezakana una underlying condition nyingine tu. Kwa mfano feni inaweza kuwa una allergy ya mavumbi hivyo hufanya uugue. Kuhusu maji ya bomba na viwandani kuwa unapata homa, mh.. hili ni gumu kidogo. Inawezekana kabisa ni hisia zako tu au ilikuwa coincidence iliyotokea. Vinginevyo pengine mwili wako uko sensitive kwa vitu vinavyopatikana kwenye maji japo ni ngumu. BTW unaposema unapata ''homa'' una maana gani? Kwa sababu homa maana yake ni joto la mwili kupanda na kuisikia kuumwa na pia baridi. Nauliza kwa sababu kuna makabila mengine kuumwa kokote huwa wanaita ni homa.
 
Kweli? Mimi nikila ice cream, juice na maji baridi kesho yake au jioni ya hiyo siku nina tonsils.
Hili ni la kisayansi kabisa. Vitu vya baridi havisababishi. Ni maambukizi ya virus au bakteria. Wewe pengine mwili wako uko sensitive sana kwa temperature change hivyo unakuwa na reaction kooni kwa sababu ya ule ubaridi. Nina uhakika unachopata siyo tonsils bali ni reaction ya mwili wako. Ni kama mwili wako unapata ''shock'' na ku-react kwa ule ubaridi. Nikuulize swali: hiyo hali inachukuwa muda gani kuisha na huwa unatumia nini?
 
Haya maji ya Auwsa yaliojaa chumvi ndio tuchemshe tunywe!! [emoji28]
Anafikili wote tunapata ya mto RUVU
huki temeke ya DAWASA ila yana chumvi
ndio nikagundua kunve ya kisima ila yanasambaWa na dawasa hata kwa chai hayanyweki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…