Utambulisho wa "Wakili Msomi" kwa Mawakili au wanaSheria

Hili neno wakili msomi hata mim nilikua nataka kulijua kinaga ubaga maana hasa mtangazaj maulid kitenge hulitumia
 
Teh naona Jf wameamua kutuumbua tunaotumia tecno halafu kwenye uzi wa tecno tunapondea kinyama..... Hiyo ndio tofauti ya usomi sijui umenielewa

"Sent from Tecno whatever "
Eeeh ndo mambo yanavyokwenda kumbe

Sent from my SM-J100H using JamiiForums mobile app
 
Kwa maana hiyo kama kuna watu wa taaluma nyingine kama watangazaji, wahasibu n.k. wanaofanya kazi hizo kutokana tu na uzoefu wao bila kusomea hao waitwe watangazaji na wahasibu. Wale waliosomea waitwe watangazaji wasomi na wahasibu wasomi?
 

Ni sawa na katika Wanaume sisi ambapo kiuhalisia Wanaume wote ni ' Wabanduaji ' ila kuna Wanaume ' Wabanduaji ' wa ' Kutukuka '. Ni matumaini yangu kwa mfano huu ' Kuntu ' kabisa nitakuwa nimeshakidhi haja yako ya Uelewa juu ya ulichokiuliza Mkuu.
 
Kwa maana hiyo kama kuna watu wa taaluma nyingine kama watangazaji, wahasibu n.k. wanaofanya kazi hizo kutokana tu na uzoefu wao bila kusomea hao waitwe watangazaji na wahasibu. Wale waliosomea waitwe watangazaji wasomi na wahasibu wasomi?
HAPANA NA WALA SIDHANI HIZO ZAMA WALIFANYA HIVYO.
kama watu wa fani mbali mbali wangeitwa kama ulivyoandika hapo juu enzi hizo...basi na sisi wa leo tungerithi.

Sent from my HTC Desire 820G PLUS dual sim using JamiiForums mobile app
 
Wakili msomi ni neno/kauli isiyo rasmi inayotumiwa na watu kwa utashi binafsi.

Ndio maana kuna watu uhususani wapinzani wanamuona Tundu Lisu ni wakili msomi lakini ukimwambia Olesendeka Lisu ni wakili msomi hawawezi kukuelewa kabisa.
 
Kwahiyo wasomi wapo kwenye sheria tu? Hakuna wahasibu wasomi? Wanauchumi wasomi? Mainjinia wasomi? kwani msomi si mtu aliyesoma? kwanini wakili ndio wawe wasomi? ina maada kada nyingine sio wasomi(hawajasoma)?
Kwa upande wa mainjinia "wasomi" wao upenda kutambulishwa kwa kuanza na neno "Engineer" na kama ni kuandikwa jina upendelea iandikwe kwa kuanza na Eng. kisha jina lake linafuatia Japo kuna baadhi hawapendi sifa hizo.
 
Wakili msomi ni neno/kauli isiyo rasmi inayotumiwa na watu kwa utashi binafsi.

Ndio maana kuna watu uhususani wapinzani wanamuona Tundu Lisu ni wakili msomi lakini ukimwambia Olesendeka Lisu ni wakili msomi hawawezi kukuelewa kabisa.
Isijekuwa waasisi wa matumizi ya maneno hayo ya "wakili msomi" wakawa ni wafuasi au mashabiki wa wabunge wanasheria au mawakili hasa wale wanaokuwa wanatetea kwenye kesi zinazohusu vyama vya upinzani wa kisiasa kutokana na uzito wa hoja zao bungeni au mahakamani?
 
wanasemaga eti ni mawakili ambao huwa wanakua hawapo upande wa serikali wakati utetezi mahakamani.
 
aseeh kumbe
 
Kwa upande wa mainjinia "wasomi" wao upenda kutambulishwa kwa kuanza na neno "Engineer" na kama ni kuandikwa jina upendelea iandikwe kwa kuanza na Eng. kisha jina lake linafuatia Japo kuna baadhi hawapendi sifa hizo.
Kwa upande huo,lazima uende intern kwa miaka mitatu na upeleke ripoti Bodi ndipo usajiliwe kama Mhandisi Mahiri/Mjuzi(Professional Engineer)! Hata kama una PhD,Masters Degree lazima ujisalimishe Bodi kwa andiko fulani la ubobez katika Uhandisi ndipo Bodi ya Wahandisi(ERB) ikupe usajili na kukuandikia barua kuwa kwa usajili huu utaanza jina lako kwa kuanzi kifupisho Eng. CHAZA au CHAZA(PEng-ERB)!
Kipekee ni utaratibu mzuri na makini. Ukiona mtu anaanza na jina au kuandika hivyo nilivyotoa mfano,jua Bodi imebariki atumie jina hivyo. Siyo jambo jepesi hata kidogo. Wapo watu wengi hawajapata hiyo sifa ya kuanza na kifupisho Eng....... badala yake wanajulikana kama Grad Eng,ambapo kisheria haruhusiwi kuanza mwanzon,bali ni mwishoni kwamba bado ni Mhandisi Mwanafunzi,haijalishi una level gani ya Elimu,ikiwa Bodi haijaona ripoti yako kuonyesha umeiva,hutaruhusiwa kuanza na acronomy Eng.

Sent from my G630-U10 using JamiiForums mobile app
 
Ni maneno ya heshima tu(courtesy) kati ya pande mbili za watu ambao kadhia(kesi) inawafanya kuwa kama maadui(adversaries).
Kesi katika mfumo wa 'common law' zinazalisha povu jingi ambalo namna moja ya kulizuia ni matumizi ya lugha ya kiungwana kama mheshimiwa hakimu, wakili msomi(learned brother, learned attorney) n.k
Common law inatumiwa na nchi za Uingereza na yaliyokuwa makoloni yake na kote huko kuna huo msemo. Hivyo maneno hayo hayana uhusiano na attitude za mawakili wa Tanzania pekee au kuwa wao ndio wasomi pekee hapa nchini.
Ila ni kweli pia kuwa mawakili kwenye sheria(attorneys at law)
wana sifa maalum za kisomi zinazowatofafautisha na wadau wengine kwenye daawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…