Niliwahi kusoma mahala, hii sio Tanzania tu, ni Dunia nzima kwa wanasheria kuitwa au kujiita wasomi au Learned brothers/sisters.
1. Mawakili wanapokua mahakami na wakawa wanabishana kwa hoja, wakili mmoja haweza kumpinga mwenzake kwa kumuita mjinga au mpumbavu, hapana anatakiwa hata kama hoja ya wakili wa upande wa pili ni ya kijinga, anatakiwa kusema wakili msomi mwenzangu hapo napingana na wewe hivi na hivi na sio kutumia maneno mabaya au majina mabaya katika kupinga hoja. Yani hutakiwi kumuonyesha mtu ni mjinga moja kwa moja, unampaka mafuta kwa mgongo wa chupa. Kwamba kama mtu ni mjinga usimwambie wewe ni mjinga, mwambie tu brother uwezo wako wa kukubali mambo unashuka ndugu yangu(your level of appriciating things is diminishing)
2. Mawakili au wanasheria wanafundishwa kumshitaki au kumtetea yoyote kutoka katika taaluma yoyote ile, iwe unatoka uhasibu, sheria, uchumi, uinjinia, sayansi, udaktari, wizi, ujambazi, ulawiti, ubakaji, urubani, fani zote.
Hivyo wanajiona kua wanajua mambo karibu yote kama sio yote kwa ujumla yaliyo chini ya jua. Ndio maana huwezi kupeleka kesi mahakamani ya udaktari hakimu akakuambia kua bwana sisi sio madaktari hivyo hiyo kesi haitasikilizwa, hapana , wataipokea na kuisikiliza hadi mwisho na hukumu itatolewa utafikiri wao wanajua udaktari.
Kwa mantiki hiyo wanasheria toka zamani wamekua wakiona fani nyingine kama fani za kiwango cha chini na kijiona wao ni bora na ni wasomi kuliko wengine.