Hizi ni hulka za ubaguzi tu zinatusumbua!
Kwa uzoefu wangu Kiswahili kinazungumzwa ukanda wote wa East Africa. Ukiwa Nairobi au Busia kwa mfano; Kiswahili kinatumika sana! Si askari, si kwenye matatu, si boda boda, si vendors, makanisani, misikitini, n.k! Kiswahili kinazungumzwa hasa! Na lahaja zinafuraisha kama midundo ya mzuki mzuri.
Lugha yoyote ile ikizungumzwa na watu wa jamii tofauti tofauti waliotenganishwa na mipaka ya asili lazima matamshi na lahaja ziwe tofauti! Mfano: Kiingereza cha mmarekani, mkanada, muingereza, muaustria, mfaransa, mdachi, mwarabu n.k ni tofauti! Muhimu ni kuwa watu wanawasiliana na deals zinakamilika!
Sasa tunapoteza muda kuanza kujadili wapi wapo vizuri wapi hawako vizuri! waTanzania tunajinasibu kuwa tunakiongea Kiswahili kwa ufasaha sana Lakini walioshikilia fursa za kukifundisha na kukiendeleza kwenye vyuo nje ya nchi ni waKenya.
Tutafute vinavotuunganisha!