Hiyo ni ishara kuonesha namna ambavyo siasa nchini kwetu zimefiliska kufikia kiwango hiki.
Style ya uongozi wa Magufuli imefuta ideological identity/positions za vyama vya siasa vyote na kubakiza party legal framework operations similar to an industrial line of product manufacturing.
Hata CCM hali iko hivyo ndio maana tunashuhudia wajasiria siasa wengi (kibao) wanaomba kugombea udiwani au ubunge kupitia chama hicho.
Pengine utakuwa ulimsikia Augustino Lyatonga Mrema jana ndani ya Mkutano Mkuu wa CCM akiomba chama chake kipewe wagombea ubunge/udiwani kutoka miongoni wa watakaokuwa hawakupitishwa na CCM.
Aidha, ukisikiliza nyimbo walizokuwa wakiimba wasanii kwenye mkutano mkuu wa CCM na kisha kushangiliwa na wajumbe hao pasipo nyimbo kuwa na ideological substance inaonesha kiwango kilichofikiwa cha ideological paucity ndani ya CCM.
Ukiona mwenyekiti na mgombea kiti cha urais wa chama anateuliwa, lakini badala ya hotuba yake ya kukubali uteuzi kusheheni mipango kiitikadi au tathmini ya utendaji miaka mitano iliyopita (hapa kikwete alipaweza sana), kwa mfano namna ambavyo chama kinaungwa mkono na wananchi (wanachama wapya), uwezo wa kubuni na kutekeleza miradi yake ya kisiasa, uwezo wa kuhamasisha na kutumia rasmilimali za chama, uwezo wa kuimarika kwa institutuinal machinery ya chama, uwezo wa chama (siyo serikali) kuchagiza (influence) public opinion, na kadhaika - mgombea pekee wa nafasi ya urais na mteule wa Chama Cha Mapinduzi ana-reduce mkutano mkuu wa chama chake kuwa tukio la kupiga kura za kumteua mgombea tu, na ndani ya masaa manne, badala ya kuendelea na ratiba ya siku mbili zilizopangwa, anakatiza na kutangaza kuisha kwa mkutano mkuu, ujue kuwa kwa sasa Tanzania inaelekea shimoni kisiasa, and the first victim is CCM!