Utapeli wa “Chumvi na Mafuta ya Upako” Wafichuliwa


Sasa inawezekanaje mtu wa mungu ahujumiwe na wachawi wakati unaupako zote
 
watu weusi wengi hawana uwezo wa kuchambua mambo na kuhoji. Wanapigwa wengi sana.
Ni kweli watu wengi hawana uwezo wa kuchambua mambo na kuhoji. Kwa sababu hiyo sisi tuliojaliwa uwezo wa kuchambua mambo, tusikae kimya, tuwasaidie wenzetu.
 
Unatoa wapi hizo definition za dini?
 
asante kunitag
Nyakati hizi za mwisho manabii wengi wa uongo wametokea na kuwadanganya wengi kama Maandiko yanenavyo(Mt24:11). Na watu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Maneno ya Mungu yako wazi lakini kwakuwa watu hawasomi Biblia wanadanganyika kirahisi.
Mkuu Achia Huru, Setfree , haya usemayo ni kweli
Ni kweli katika Biblia mafuta na chumvi vimetajwa.
ni kweli
Kwa mfano katika kitabu cha Yakobo 5:14 imeandikwa:"Mtu wa kwenu anaumwa? Na awaite wazee wa kanisa, nao watamuombea, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana." Andiko hili linaonyesha kuwa upako wa mafuta ni sehemu ya ibada na uponyaji wa kiroho.
ni kweli sio mafuta na chumvi tu,
bali maji,mafuta,chumvi na mafusho,moto,moshi,ubani, majivu, udongo, etc ni vifaa vya kiroho,vinapokuwa annointed!
Wakristu Wakatoliki,wanatumia maji na mafuta kubatiza na kwenye kutoa sacramenti zote,Yale maji ya baraka,yamekuwa annointed na chumvi,tunatumia mafuta kwenye sacrament ya upako mtakatifu,tunatimia majivu siku ya Jumatano ya majivu,tunatimia udongo kwenye mazishi na tunatumia mafusho ya ubani kwenye ibada za sikukuu zote。

Matumizi ya vitu hivyo vyote ni natural elements,sio utapeli,they have the induction powers kufungulia imani yako,kufunguka na kufanya miujiza ya uponyaji na mafanikio。Kinachoponya sio maji,mafuta na chumvi, ni imani oliyo ndani yako。Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo? na "Will Powers!", "Faith Healing!"-Nguvu za Kufanya Miujiza ya Uponyaji kwa Imani. Kila Mtu Anazo!
Katika Marko 6:13 imeandikwa pia hivi – "Wakatoa pepo wengi, wakawapaka mafuta wengi waliokuwa wagonjwa, wakawaponya." Andiko hili linaonyesha pia jinsi Mitume walivyotumia mafuta kwa uponyaji.
ni kweli
LAKINI Maandiko hayo hayatuambii kwamba wagonjwa, wenye shida na wanaohitaji baraka wanapaswa kununua bidhaa hizo ili wapone au wabarikiwe. Kwahiyo wauzaji ni matapeli.
true, ni kweli!huo ni utapeli!。
Katika Mathayo 10:8, tunasoma kuwa Yesu aliwapa wanafunzi wake mamlaka ya kuponya wagonjwa na kufukuza pepo, lakini aliwaonya wasifanye huduma hiyo kwa kudai malipo.
ni kweli
Mathayo 10:8 – "Ponyeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure."

Andiko hilo linaonyesha wazi kuwa karama za Mungu zinapaswa kutolewa bure.
ni kweli。
Kwa upande wangu, nilipandisha mabandiko haya kujaribu kusaidia
P
 
Unatoa wapi hizo definition za dini?
Kwani hujionei,?

Dini utaambiwa ni njia ya mwanadamu kumtafuta Mungu ,but in reality Wewe ukipotea huwez kumtafuta Mungu bila yeye kwanza kukutafuta

Dini ndio hizo mambo unazoona za kina mwamposa ,kuuza maji, mafuta, vitisho vingi, au kwenye uislamu, dini imejikita kwenye matendo hasa ya mwili



REJEA Yesu na mafarisayo ,ugomvi mkubwa wale walikuwa na dini sana , ndio maana Yesu aliwaambia Watoza ushauru na makahaba wanawatangulia kuingia mbinguni ,

REJEA yule mwizi pale msalabani alifanya jitihada zipi za dini ?

Aliokolewa kiulaini


Kwahiyo hakikisha unatafuta Wokovu ambao unapatikana kwa njia ya kumuamini Yesu kristo, dini zimejaa utapeli mwingi sana ,humo utatishwa Hadi uliwe nauli utembee km 10,
 
Hana jibu, mtu wa mungu anazidiwaje na shetani au wachawi?
Hujaelewa.

Kilichotumika siyo uchawi, zilitumika hujuma kwa njia ya kawaida ila walioandaa mpango huo walikuwa ni wachawi.

Kwani tuseme wewe hapo ulipo ukichukua kisu halafu ukaenda ukamvizia mtumishi wa Mungu na kumburuza nacho, hakiwezi kumkata kisa ni mtumishi wa Mungu?
 
We Paschal hujamwelewa vizuri aliyeleta uzi huu. Yeye lengo lake ni ku-dscourage watu wasivitumie vitu hivi kwa sabau anajua nguvu iliyomo ndani yake. Kwa hiyo anajitahidi kuwarubuni watu humu ili watakapokuwa wameacha kuvitumia, aweze kupata ahueni

Yesu alsiema kuwa wanaomwamini watafanya yote aliyowahi kuyafanya, na pia zaidi ya hayo kwa maana kuwa Yesu aliwapatia waumini uwezo wa kufanya hata yale ambayo yeye hakuwahi kuyafanya

Chukulia kwa mfano, muumini anayeweza kuomba halafu mtu aliyekufa akafufuka, anashindwaje kubariki maji au chumvi kwa ajli ya matumizi ya mtu mwingine ambaye imani yake ni ndogo?

Hii nchi sasa hvi tumeshavamiwa na mtandao wa wachawi inabidi tuwe makini sana, ila mbele ya Mungu watanyoosha mikono tu muda siyo mrefu; ni hakika KWA JINA LA YESU!
 
Nasemaga imani ikikuzidi ni utumwa wanabisha.
 
Sio manabii wa Uongo huo ni mchezo pandikizi la Wanasiasa fulani fulani wa Chama fulani kuwaweka watu km hao ili kuwapumbaza watu wasiamke na kudai haki zao, wote unaowaona wanafanya vile kwa kupitia mkono wa Wanasiasa kuanzia Kimara Temboni mpaka Kawe kote ni pandikizi la Wanasiasa
 
Hahaa, umenivunja mbavu: "kama hajachezea bakora..."

Hata Yesu alipindua meza za waliokuwa wakifanya biashara hekaluni. Ni wakati mwafaka sasa wa kupindua meza za hao wauza viambata vya upako.
Kuna Jamaa Yeye anasema ni Vifaa vya Kiroho pale Morogoro Road.
Mungu atusamehe sana
 
Leta ushahidi, mkuu
 
Wakristu Wakatoliki wanatumia maji na mafuta kubatiza... tunatumia majivu siku ya Jumatano ya majivu... Matumizi ya vitu hivyo vyote ni natural elements,sio utapeli,they have the induction powers kufungulia imani yako
Mkuu, Pascal Mayalla , wewe ni Great Thinker na Biblia unaijua. Kwakuwa Biblia ndio mwongozo wa maisha ya Wakristu(Zaburi 119:105; 2 Timotheo 3:16-17), naomba unitajie mistari ya Biblia inayoagiza hayo uliyoyasema yafanyike. In other words, wanaofanya hayo, wanafanya kwa kuegemea Maandiko yapi ya Biblia.

Nimekuuliza hivyo kwa sababu Yesu alisema tukiwa na chembe ndogo tu ya imani tunaweza kuuambia mkuyu huu ng'oka ukaote baharini(Luka 17:6). So, kwanini tuhangaike tena kutafuta majivu na kuharibu mazingira?

Vile vile Biblia inasema imani huja kwa kusikia ujumbe unaotokana na Neno la Kristo(Rum 10:17), sio kwa kutumia natural elements.
 
Poleni. Ila sasa mmeijua kweli, iwaweke huru.
Ushauri wako ni upi maana utapeli umeenea hata kwa makanisa yasiyouza hivyo vitu sadaka zimekuwa nyingi mno mtu unakamuliwa mpaka Senti ya mwisho uliyo nayo je tukasali wapi sasa maana tunampenda Mungu
 
Mitume na manabii feki wameua soko la wazee wa tiba mbadala waliotuuzia juice za michicha na matembele kwa hela ndefu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…