PAKASHUME JOHN
JF-Expert Member
- Jan 7, 2017
- 303
- 329
Kazini kuna kazi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa taarifa yako mafuta ya upako yanayotumika muda huu, ndiyo yale yale waliyokuwa wanapakwa wfalme wa zamani kama vile akina Daudi na akina Sauli
Kipindi hicho walikuwa ni makuhani pekee waliokuwa wanaweza kuyatamkia baraka, ila baada ya Yesu kufa msalabani hali imebadilika na kuwafanya watu wote waliookoka kuwa Makuhani
Kwa taarifa yako zaidi ni kuwa watu waliokanayagana kwenye tamasha la la kukanyaga mafuta la Mwamposa na kupelekea wengine kufariki dunia, zilikuwa ni hujuma zilizofanyw na wachawi, lengo ilikuwa ni ili azuiwe kuwa anatengeneza mafuta ya upako
Huelwei chochote, mimi ninapoongea usinibishe, nina ushahidi kutoka pande zote, duniani na Mbinguni
Sasa inawezekanaje mtu wa mungu ahujumiwe na wachawi wakati unaupako zote
Hana jibu, mtu wa mungu anazidiwaje na shetani au wachawi?NI hujuma zilizofanywa na kundi LA wachawi kwa kutumia njia za kawaida. Ni kama watafute wezi na kuwapa hela ili kuja kuiba nyumbani kwako
Ni kweli watu wengi hawana uwezo wa kuchambua mambo na kuhoji. Kwa sababu hiyo sisi tuliojaliwa uwezo wa kuchambua mambo, tusikae kimya, tuwasaidie wenzetu.watu weusi wengi hawana uwezo wa kuchambua mambo na kuhoji. Wanapigwa wengi sana.
Unatoa wapi hizo definition za dini?Dini ni biashara ,ukiona Ukristo umefanywa dini basi Kuna biashara ndani yake
Ukristo ni wokovu wa MUNGU kumtafuta mwanadamu aliyepotea dhambini
Dini ni njia , mishemishe, mbilingembilinge,harakati ,utapeli wa mwanadamu kutafuta pesa na ku manipulate watu kupitia jina la Mungu
asante kunitagPascal Mayalla uje uku
Mkuu Achia Huru, Setfree , haya usemayo ni kweliNyakati hizi za mwisho manabii wengi wa uongo wametokea na kuwadanganya wengi kama Maandiko yanenavyo(Mt24:11). Na watu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Maneno ya Mungu yako wazi lakini kwakuwa watu hawasomi Biblia wanadanganyika kirahisi.
ni kweliNi kweli katika Biblia mafuta na chumvi vimetajwa.
ni kweli sio mafuta na chumvi tu,Kwa mfano katika kitabu cha Yakobo 5:14 imeandikwa:"Mtu wa kwenu anaumwa? Na awaite wazee wa kanisa, nao watamuombea, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana." Andiko hili linaonyesha kuwa upako wa mafuta ni sehemu ya ibada na uponyaji wa kiroho.
ni kweliKatika Marko 6:13 imeandikwa pia hivi – "Wakatoa pepo wengi, wakawapaka mafuta wengi waliokuwa wagonjwa, wakawaponya." Andiko hili linaonyesha pia jinsi Mitume walivyotumia mafuta kwa uponyaji.
true, ni kweli!huo ni utapeli!。LAKINI Maandiko hayo hayatuambii kwamba wagonjwa, wenye shida na wanaohitaji baraka wanapaswa kununua bidhaa hizo ili wapone au wabarikiwe. Kwahiyo wauzaji ni matapeli.
ni kweliKatika Mathayo 10:8, tunasoma kuwa Yesu aliwapa wanafunzi wake mamlaka ya kuponya wagonjwa na kufukuza pepo, lakini aliwaonya wasifanye huduma hiyo kwa kudai malipo.
ni kweli。Mathayo 10:8 – "Ponyeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure."
Andiko hilo linaonyesha wazi kuwa karama za Mungu zinapaswa kutolewa bure.
Kwani hujionei,?Unatoa wapi hizo definition za dini?
Hujaelewa.Hana jibu, mtu wa mungu anazidiwaje na shetani au wachawi?
We Paschal hujamwelewa vizuri aliyeleta uzi huu. Yeye lengo lake ni ku-dscourage watu wasivitumie vitu hivi kwa sabau anajua nguvu iliyomo ndani yake. Kwa hiyo anajitahidi kuwarubuni watu humu ili watakapokuwa wameacha kuvitumia, aweze kupata ahueniasante kunitag
ni kweli
ni kweli
ni kweli sio mafuta na chumvi tu,
bali maji,mafuta,chumvi na mafusho,moto,moshi,ubani, majivu, udongo, etc ni vifaa vya kiroho,vinapokuwa annointed!
Wakristu Wakatoliki,wanatumia maji na mafuta kubatiza na kwenye kutoa sacramenti zote,Yale maji ya baraka,yamekuwa annointed na chumvi,tunatumia mafuta kwenye sacrament ya upako mtakatifu,tunatimia majivu siku ya Jumatano ya majivu,tunatimia udongo kwenye mazishi na tunatumia mafusho ya ubani kwenye ibada za sikukuu zote。
Matumizi ya vitu hivyo vyote ni natural elements,sio utapeli,they have the induction powers kufungulia imani yako,kufunguka na kufanya miujiza ya uponyaji na mafanikio。Kinachoponya sio maji,mafuta na chumvi, ni imani oliyo ndani yako。Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo? na "Will Powers!", "Faith Healing!"-Nguvu za Kufanya Miujiza ya Uponyaji kwa Imani. Kila Mtu Anazo!
ni kweli
true, ni kweli!huo ni utapeli!。
ni kweli
ni kweli。
P
Nasemaga imani ikikuzidi ni utumwa wanabisha.Kabla ya kuufichua huo utapeli, hebu tuwasikilize kwanza hawa manabii feki:
Nabii XXL: Aisee, hizi sadaka tunazopata hazitoshi kununua ndege, na kutufanya tuishi maisha ya kifahari. Naomba tubuni mbinu ya kuongeza mapato.
Nabii X: Mi nafikiri wakati wa maombezi, tuwe tunawauzia watu chumvi, mafuta, maji na vitambaa, lakini tuwaambie kwamba vitu hivyo vina upako. Watanunua tu.
Nabii XXL: Mh, tukifanya hivyo kabla ya kuwaombea, watatugundua. Katika Biblia Yesu si alisema huduma za kuponya na kutenda miujiza hazipaswi kutolewa kwa malipo?
Nabii X: Mkuu, watu hawana muda wa kusoma Biblia, hawajui hilo Andiko. Nakwambia watanunua tu. Tena tukiwaambia mafuta na chumvi vimetoka Israeli, ndio kabisa, hata tukiwauzia kwa dola watanunua.
Nabii XXL: Hahaa, aisee we una akili. Hebu tuanze haraka kuifanyia kazi hiyo mbinu. Ndani ya mwaka mmoja tu, tutakuwa mabilionea.
================
Nyakati hizi za mwisho manabii wengi wa uongo wametokea na kuwadanganya wengi kama Maandiko yanenavyo(Mt24:11). Na watu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Maneno ya Mungu yako wazi lakini kwakuwa watu hawasomi Biblia wanadanganyika kirahisi.
Ni kweli katika Biblia mafuta na chumvi vimetajwa. Kwa mfano katika kitabu cha Yakobo 5:14 imeandikwa:"Mtu wa kwenu anaumwa? Na awaite wazee wa kanisa, nao watamuombea, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana." Andiko hili linaonyesha kuwa upako wa mafuta ni sehemu ya ibada na uponyaji wa kiroho.
Katika Marko 6:13 imeandikwa pia hivi – "Wakatoa pepo wengi, wakawapaka mafuta wengi waliokuwa wagonjwa, wakawaponya." Andiko hili linaonyesha pia jinsi Mitume walivyotumia mafuta kwa uponyaji.
LAKINI Maandiko hayo hayatuambii kwamba wagonjwa, wenye shida na wanaohitaji baraka wanapaswa kununua bidhaa hizo ili wapone au wabarikiwe. Kwahiyo wauzaji ni matapeli.
Katika Mathayo 10:8, tunasoma kuwa Yesu aliwapa wanafunzi wake mamlaka ya kuponya wagonjwa na kufukuza pepo, lakini aliwaonya wasifanye huduma hiyo kwa kudai malipo.
Mathayo 10:8 – "Ponyeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure."
Andiko hilo linaonyesha wazi kuwa karama za Mungu zinapaswa kutolewa bure.
Enyi mnaolifanya Jina la Mungu litukanwe kwa sababu mmewalaghai watu kuwa chumvi na mafuta mnayouza yana upako, kumbe uongo, nawasihi, popote pale mlipo ulimwenguni, badilikeni. La sivyo unabii huu utatimia kwenu:
Mathayo 7:22-23 – "Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu."
View attachment 3261034View attachment 3261076
Wamefanya kina Gwajima, Mwingira, Kakobe na T.B. Joshua nishindwe mimi kwa lipi?Ohoo, na wewe tena!
Sio manabii wa Uongo huo ni mchezo pandikizi la Wanasiasa fulani fulani wa Chama fulani kuwaweka watu km hao ili kuwapumbaza watu wasiamke na kudai haki zao, wote unaowaona wanafanya vile kwa kupitia mkono wa Wanasiasa kuanzia Kimara Temboni mpaka Kawe kote ni pandikizi la WanasiasaMathayo 7:22-23 – "Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu."
Kuna Jamaa Yeye anasema ni Vifaa vya Kiroho pale Morogoro Road.Hahaa, umenivunja mbavu: "kama hajachezea bakora..."
Hata Yesu alipindua meza za waliokuwa wakifanya biashara hekaluni. Ni wakati mwafaka sasa wa kupindua meza za hao wauza viambata vya upako.
Leta ushahidi, mkuuSio manabii wa Uongo huo ni mchezo pandikizi la Wanasiasa fulani fulani wa Chama fulani kuwaweka watu km hao ili kuwapumbaza watu wasiamke na kudai haki zao, wote unaowaona wanafanya vile kwa kupitia mkono wa Wanasiasa kuanzia Kimara Temboni mpaka Kawe kote ni pandikizi la Wanasiasa
Mwamposa pandikizi la CCMLeta ushahidi, mkuu
Mkuu, Pascal Mayalla , wewe ni Great Thinker na Biblia unaijua. Kwakuwa Biblia ndio mwongozo wa maisha ya Wakristu(Zaburi 119:105; 2 Timotheo 3:16-17), naomba unitajie mistari ya Biblia inayoagiza hayo uliyoyasema yafanyike. In other words, wanaofanya hayo, wanafanya kwa kuegemea Maandiko yapi ya Biblia.Wakristu Wakatoliki wanatumia maji na mafuta kubatiza... tunatumia majivu siku ya Jumatano ya majivu... Matumizi ya vitu hivyo vyote ni natural elements,sio utapeli,they have the induction powers kufungulia imani yako
Ushauri wako ni upi maana utapeli umeenea hata kwa makanisa yasiyouza hivyo vitu sadaka zimekuwa nyingi mno mtu unakamuliwa mpaka Senti ya mwisho uliyo nayo je tukasali wapi sasa maana tunampenda MunguPoleni. Ila sasa mmeijua kweli, iwaweke huru.