PreGE2025 Utapeli wa haki mahakamani: Askari kuvaa mask ni ujambazi wa kisheria!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Prof_Adventure_guide

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2023
Posts
533
Reaction score
1,499
Katika historia ya mihimili ya dola, mahakama ndiyo taasisi ya mwisho ya utoaji wa haki—lakini leo tunaishuhudia ikigeuzwa jukwaa la uonevu na maigizo ya kisiasa. Ni jambo la kusikitisha na la kuaibisha kuona askari wa serikali wakivamia mahakama wakiwa wamevalia mask kana kwamba wanakwenda kupambana na magaidi, si kuhifadhi amani.

Kitendo cha askari kuvaa mask ndani ya mahakama si tu ni utovu wa nidhamu, bali pia ni ukiukwaji wa wazi wa Kanuni ya 36 ya The Advocates (Professional Conduct and Etiquette) Regulations, GN No. 118 of 2018, pamoja na miongozo ya Jeshi la Polisi kupitia Police General Orders (PGO). Sheria hizi zinamtaka kila mhudhuriaji wa mahakama, hasa maofisa wa dola, kuonesha heshima kwa mavazi rasmi, kuacha vitisho, na kuonesha uso wao hadharani – ishara ya uwazi mbele ya chombo cha haki.

Lakini leo, haki inatapeliwa mchana kweupe! Serikali hii haijifichi tena – imeamua dhahiri kugeuza vyombo vya sheria kuwa vinywaji vya kisasi kisiasa. Askari waliovaa mask si walinzi wa usalama, bali ni watendaji wa hofu na vitisho. Huu ni ujambazi wa kisheria.

Kinachoendelea dhidi ya Tundu Lissu si kesi, bali ni maigizo ya dhuluma yaliyoandaliwa na mfumo kandamizi. Mtu aliyejaribu kuikosoa serikali, kutetea Katiba na kutafuta haki kwa Watanzania sasa anaandamwa na mifumo ya uonevu kana kwamba ni adui wa taifa.

Haki haipatikani kwa bunduki wala kwa mask mahakamani – inapatikana kwa kuheshimu Katiba, sheria na utu wa binadamu. Serikali hii inaitesa haki, inalipaka tope jina la demokrasia, na kuifanya mahakama kuwa chombo cha utapeli wa kisheria.

Tutazame vizuri: hiki si kioo cha haki. Ni kivuli cha udhalimu.
 
Kwa Her Excellence Rais wetu hili analisemeaje?
 
Hello!

Yaani nimeamua niende kusikiliza shauri la rafiki YANGU Mahakamani,rafiki YANGU kabambikwa kesi ya uhaini.

Nikaamua kuvaa mask usoni Ili kuepuka macho ya wabaya wangu wasinione,

Je nitaruhusiwa kuingia na mask usoni Mahakamani?

Karibuni 🙏
 
Back
Top Bottom