Utaratibu wa kuachia vyumba kwenye Hotel, Lodges na Guest House ni wa udhulumaji

Utaratibu wa kuachia vyumba kwenye Hotel, Lodges na Guest House ni wa udhulumaji

Hotel zinazoeleweka unaambiwa check in time ambayo huwa 1000hrs-1200 na check out time 1000hrs-1200hrs. Hapa unakuwa umefsnya booking.
Sasa ukifika saa 1000 utapata 24hrs unayotaka. Kama ukifika baadae sio kosa lao.
Tatizo wengi wanaenda Hotel au Guest house bila booking, mfano unafika saa mbili usiku. Wao muda wao wa check in and out ni ule ule hawawezi kubadili kwasababu yako. Chumba hicho unacholala wewe leo kuna mtu kashafanya booking anaingia kesho saa 1000 au 1200.
Wasiwe wanauza sasa kama hakita kidhi muda, ama wamwambie mteja tu.
 
Hii inakera sana. Niliwahi book showtime wakati najiandaa na game ndom hakuna.
Ikabidi nitoke nje nikatafute zana.
Nafika naambiwa muda umeisha.
Nilijitetea sana, nikaambiwa ona wateja wanasubiria.
Nikataka nilete songombingo. Ndo nikaruhusiwa.
Mchuchu yuko ndani anasubiria.
Nilipiga show kinyonge sana sababu walishanichanganya.
Naam hii starehe yataka utulivu... 👍
 
Ili kuwakomoa we nenda saa 1 asubuhi then unawaambia unalala wala awana shida utalipia ya mpaka kesho 4 asubuhi
 
Masaa 6 yote hayo?

Mbona mie huwa naachia chumba hata ndani ya dakika 45 tu na hakuna lawama

labda lawama za mhudumu kuhusu mashuka yake anayoyakuta uvunguni yana rangi 3 mpya!!
Sasa chumba chote umesha kiharibu na harufu ya kinyesi wwe mwenyewe huwezi kukaa unakikimbia!!
 
Serikalini kuna kitu wanasema fuata sheria, kanuni, na miongozo ya kazi. Taasis imara haihitaji huruma katika kutekeleza majukumu yake. Hata hizo Lodge, hotel etc zinaweza kuwa na mfumo huo.
Lodge ni biashara, na kwenye biashara kanuni ya kwanza kabisa ni kufata matakwa ya mteja.
Serikali haijawai kufanikiwa kwenye biashara kwa sababu wanatumia sana sheria kuliko kumsikiliza mteja.
Picture this, umejenga lodge yako kwa 100 millionns unakuja kukataa mteja wa 25000 tu kwa sababu kafika saa 8 usiku na sheria inataka atoke saa nne asubuhi, mind you hicho chumba hadi kinapatikana kwa usiku huo maana yake jana hukufanya biashara,
Binafsi nikilazimika kuchukua lodge usiku mnene huwa nafanya makubaliano kabisa kwamba sito check out saa nne akikataa naondoka na hela yangu, hadi nipate lodge wanaoelewa logics za biashara
 
Check in: any time
Check out 10:00
 

Attachments

  • IMG_1632.jpeg
    IMG_1632.jpeg
    309 KB · Views: 5
Hio ratiba ya hovyo sana.. kuna siku nilikua nilikua na harakati nyingi mpaka saa10 usiku nikasema nikalale mahala saa6 nisepe zangu mkoa... nikasema niwaambie kabisa mana hio hiyana wanayo! Aisee nilimwelekeza yani tu kulala nipitilize mpaka saa6 yani hayo masaa tu mawili kuyaongeza naambiwa nilipie tena..
Nililala tu kwakua nilikua na shida na nna msala la sivyo nisingelala
 
Kuna hotel niliwahi kulala hadi saa nne na dakika 5, nilipo toka na kuomba radhi kwa kuchelewa for 5 minutes.....
Nilisikia msonyo mrefu ukitoka kwa nyuma yangu na kufuatiwa na maneno "ukitaka raha, safiri na chumba chako"
😂🤣
 
Back
Top Bottom