Utaratibu wa kuishi na ndugu baada ya ndoa unafaa uwe vipi?

🀣🀣🀣Ukoo una laana hao
 
Nakupa mbinu moja ya kibaharia

Hao ndugu zake wa kike tongoza wote atakaekubali pita nae na watakaokataa lazima watamwambia mke wako na mkeo akikuuliza maambie tu wanakaaga sebulen kihasarahasara....lazima awapige marufuku kuja kwake


CASE CLOSED
 
Wewe ni tatizo unajifanya unapesa, unatoa nauli kwa watu wazima !! Watu wavivu hawaingii nyumba yenye njaa!! endelea watakuja na begi next time
 
Ndugu zako wao huwa hawaji kwako?,familia zetu za kimaskini ni jau,wengine walikaa kwa watu na kusaidiwa hadi hapo walipofika!,ndugu kutembeleana ndiyo uungwana ila kuweka kambi ndiyo changamoto.
 
Nakuambia tabu sana
 
Wazo zuri sana
 
Kiongozi nikupe tu ushauri ,ndgu hawabebiki na huwa wanamthamini wakati mtu ana kitu ,
Mtakupa historia fupi ya mzee wangu (binafsi nimepata funzo ) kipindi mzee ana uwezo na mali zake ,nyumbani watu hawakauki ,ndgu walijaa kibao mpaka sisi watoto tukawa tunaminyika au kupunjika maswala ya msosi kwa ajili yao ,maana alikuwepo ma mdogo akijipakulia basi alikuwa anajijazia yeye na sisi kutupunja chakula ,hiki kitu huwa sikisahau mapaka utu uzima huu,Baadae mzee alikuja filisika sana na ndgu hawaji hata kusalimia ,jambo ambalo lilikuwa likimuumiza mama na alikuwa akinilalamikia ,wanavyonyanyapaa ndgu zake kisa hana kitu ,kama mtoto ilikuwa inaniumiza sana ,ni kaapa ntatafuta maisha kwa hali na mali ,
Si haba kwa sasa nnakijiuwezo ,kiasi na nimekuwa na msimamo ,familia yangu kwanza (mke watoto baba na mama ) hao wengine wanasubiri ,Habari mtu kaja kwangu kutembea bila taarifa huwa sitoi nauli hata kama ninayo maana ukiwazoesha huwa wanajenga tabia ,Na ukiwaonyesha kwamba ww unazo watakufanya chuma ulete ,siku huna kitu watakukimbia ,
Nimewekeza nguvu na akili katika kujijenga mm kwanza bila kumtanguliza mtu mwingine na hata nnachopata juwa najitahidi kuwaneemeshe familia yangu na wazazi wangu ,Hao wengine nasaidia panapouhitaji ,
Pia nimeweka msimamu kuwa sibebi mzigo wa mtu (kwa kulea mtoto wa mtu) mimi mwenyewe nimejibana niwe nawatoto wachache ili kuwapa malezi bora ,Kila mtu abebe msalaba wake ,
Usiposimama imara na kuwajengea watoto wako msingi imara kesho na kesho kutwa hao hao ndgu watakuja simanga watoto wako na kuwaambia baba ako alikuwa na pesa ila akachezea ,watasahau kwamba ulikuwa unajitoa kwao na wamesababisha kushinda kuwatimizia watoto wako kwa kuwajengea misingi mizuri
 
Nenda kawanywee then Rudi home wape mbovu watasepa wenyewe.
 
Hapo mbinu Ni rahisi tu kila akija ndugu yeyote wa mkeo wewe omba mzigo tu bila kujali jinsia hautaona kiumbe hapo tena kinakuja kuleta mazoea
 
Sidhani! Labda ungesema Wajaluo,Wagogo,Wasambaa ningekuelewa! Lakini changamoto ni kuoa ukoo maskini.
Mbona familia yetu masikin na hatuna tabia yakwenda majumbani Kwa watu tokea wadogo tulilizika na maisha ya home kipatikane chakula kisipatikane hatukuwai kuwaza kwenda kuishi Kwa ndugu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kifupi hata kama unaswali au ni mlokole unatakiwa kufukuza wote ubaki wewe na mke wako tu! Wawe ni ndugu zako au ni ndugu za mkeo fukuza.
Wakikataa nenda kwa mjumbe wa shina ukashitaki!
Mkuu unayoongea unaweza kuyatenda? hisije ikawa maneno Tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu vumilia mbona kawaida au wewe hujawai kupitia hayo Maisha? Tatizo umri husiwachukie wapo kwenye mapito

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hali ilikuwa hivi kwetu wakati tunakaa Singida mjini. Ukoo mzima wa mama wakitoka Iramba, kwetu ndio palikuwa guest house yao.
Ndio maana nilipoamua kujenga Dar, niliamua kujenga nje ya mji ili ndugu wajifukuze wenyewe kutokana na umbali. πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Tatizo hukuweka mkazo mkuu brother alikuwa mbogo sio mchezo
 
Na kwakuongezea kama amepanga atafute nyumba ndogo tuuu yenye chumba seble choo na jiko baaas hao wageni wakose pakulala
 
Pole sana kuna Watu wanapenda kitonga sana, kila kitu kwa kiasi.
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji119][emoji119] family za kiswahili hizo , ndio shida ya kuambatana na watu wasiojua mipaka Yao Ktk Maisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…