Utaratibu wa kulazimisha mtoto wa kwanza kuanza kufunga ndoa kwanza kisha ndio wafuate wadogo zake

Utaratibu wa kulazimisha mtoto wa kwanza kuanza kufunga ndoa kwanza kisha ndio wafuate wadogo zake

Hizo mila na desturi ni ngonjera tu labda kama huyo mdogo mtu ana miaka 24 ila kama dogo yuko 29 nadhani wazee wangeharakisha sana zoezi.

Hio familia nina mashaka watakuwa watu wa Mbeya hao akina nyonyoma [emoji1787][emoji1787][emoji1787] sio kwa misimamo hio ya familia nzima. Kitu akiongea dada hata kama upuuzi wadogo wote mnasikiliza.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Binafsi nitamsubiri dada aolewe
Nitatangulia pale tu atakaponiambia hana mpango wa kuolewa.
Na hapa nilishaanza kumuuliza anaolewa lini ili nichange karata zangu vizuri.
 
Habari zenu wana MMU nawasalimu

Nianze kwa kusema ndoa ni rizki, ndoa ni bahati, ndoa ni baraka sasa kuna mila na desturi za ndoa ambazo ni za kishamba katika jamii zetu ambazo bado tunazikumbatia bila maana yoyote.

Ipo hivi mwanzoni mwa mwaka huu kuna rafiki yangu wa karibu alidhamiria kuaga ukapela hivyo basi akajitoa kimasomaso kuchumbia binti katika familia flani na mchakato ukaanza chapchap Mungu si Athuman barua ya uchumba ikakubaliwa kisha tarehe ya kikao/siku ya kupeleka mahari ikapangwa.

Mungu ni mkubwa siku iliwadia na mara baada ya zoezi la kupokea mahari kuisha basi bana utata ukaanzia pale tulipo wapa tarehe tulio kusudia kuja kuoa ili kama kuna la kujadili tuwekane sawa kabisa maana tulihitaji kuondoka na tarehe rasmi ya siku ya ndoa.

Nakumbuka wanafamilia wa binti walianza kuongea kwa minong'ono kisha babu alianzisha hoja na malumbano ya hoja yakanzia hapo.

Upande wa binti wakadai kuwa haiwezekani mdogo mtu aolewe kabla ya dada yake eti ni dharau, aisee tulijitahidi kuwaelimisha kadri ya uwezo wetu kuwa ndoa ni rizki inayopangwa na Mungu hivyo sisi wanadam hatuwezi kuisitishaa ndoa ya binti yao mdogo eti kisa dada yake bado hajaolewa wakati dada mtu hata kuchumbiwa tu haijulikani atachumbiwa lini lakini wapi familia ya yule bint ilishikilia msimamo wake hadi ikatubidi tuondoke bila jibu la maana na kuahidi kurudi siku nyingine.

Ikapita kama mwezi hivi tukaomba kikao kingine nakumbuka kwenye kikao hicho tulishirikisha na viongozi wa dini lakini wapi familia ya binti ilisimamia msimamo wake na kuweka wazi kuwa hadi mkubwa aolewe ndio mdogo nae ataolewa.

Ila safari hii hatukuondoka mpaka tulipo kubaliana na tukawapa miezi 4 kama bint yao mkubwa atakua hajachumbiwa basi ndoa ya binti yao mdogo itafanyika na kama atakua amechumbiwa basi tutakuwa radhi kusubiria.

Sasa ile miezi imeshatimia na panapo majaaliwa siku ya kesho tunarudi tena huko ukweni ili kufahamu ni ipi hatma ya ndoa hii tarajiwa maana kwa taarifa tulizonazo hadi wakati huu yule binti yao mkubwa bado hajachumbiwa.

Waungwana nakaribisha ushauri wenye kujenga katika hili.

Ahsanteni

Kesho uliyoisema jana si ndo leo?

Hebu tupashe imekuwaje ndio tuchangie tukiwa tunaelewa a to z
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Binafsi nitamsubiri dada aolewe
Nitatangulia pale tu atakaponiambia hana mpango wa kuolewa.
Na hapa nilishaanza kumuuliza anaolewa lini ili nichange karata zangu vizuri.
Yani ambacho ntakifanya nikiisoma akili yako ni kukuvimbisha chini tu na najua una hofu ya mungu huwezi toa hio mimba. Wazazi watajiongeza tu kama watalea mjukuu au watapiga simu nije kukufata.🤣🤣🤣
 
Mimi siwezi kumkataza mdogo wangu kufunga ndoa ila yeye mwenyewe anapaswa ajiongeze,avute japo kamuda ili nitoke kwanza (hii ni kama nina dalili za kuolewa)

Nikijizungumzia binafsi,Mimi ni mtoto wa mwisho kwetu.
Juzi tu dada yangu amenitamkia kwamba mdogo wangu ukipata mchumba olewa ila jua utakuwa umenivua nguo Mimi dada yako.Nimepishana naye miaka 9.
Kauli yake hii ilinifanya nitafakari.
Dada yako hakutakiwa kuongea kauli kama hiyo kwa sababu itakuweka kwenye wakati mgumu kufikia maamuzi inapotokea fursa kama hiyo kwa upande wako!

I don't believe in fate, but your sister should at least know kuna watu wana-believe in fate na kuchukulia hata kama hataolewa kabisa maishani mwake wakati wadogo zake wakiendelea kuolewa, basi yote hayo ni sehemu ya maisha!!

Haya mambo kwamba heshima ya mwanamke ni kuolewa ni lazima yawe dumped in a bin kwa sababu msingi wa yote haya ni kwenye hiyo imani kwamba heshima ya mwanamke ni ndoa!!

I do believe, heshima ya mwanamke is how she behaves in the community!

Hata kama ameolewa lakini bado anaonesha tabia za hovyo hovyo mbele ya jamii bado ndoa yake haiwezi kuwa kigezo cha heshima kwake kwa sababu bado ni jinamizi mbele ya jamii, tena ni jinamizi tisha tisha kuliko mwanamke ambae hajaolewa lakini bado anajiheshimu!!
 
Niijaribu kuvaa viatu vyake mkuu

Kauli yako ya heshima ya mwanamke si ndoa ni kweli kabisa ila jaribu kukaa na wadada walio kwenye 30's uwaone jinsi walivyo na uhitaji na hiyo ndoa.

Sometimes hadi natamani nimtafutie mchumba ila ndiyo siwezi..sijui anachagua mno hata sielewi.
 
Sina mpango wa kuzaa na mtu kabla hajanioa
Kwani wote waliozaa walipanga? Mie na cousin alilipiwa mahari na akabaki na mtoto wake to date, japo aliolewa na mtu mwengine akaongeza watoto na maisha yanaendelea.

Hio hutokea na itapokukuta hutakaa huamini. Omba usipitie hilo kama mtihani wa maisha.
 
Ikitokea basi ila sitamani itokee
 
Yaani huwa nikisoma michango ya wana-JF hapa kuhusu familia zao hadi huwa nahisi kwamba sie wengine familia zetu hazina maadili kabisa!

Kwenye familia yetu (ya baba + mama) watoto tupo hivi:-
1. Male (chige)
2. Female
3. Male
4. Male
5. Male.

Hadi sasa, mpangilio wa ndoa upo hivi: 2, 4! Baada ya hapo nani atafuata, only God knows!!

Anyway, inawezekana sie wa mjini "tunaiga" mila za hovyo hovyo, manake pamoja na kwamba mimi ndie mkubwa kuliko wote, lakini sijawahi kuwasikia madingi wakimpangia au kumlazimisha yeyote kuhusu mambo ya ndoa!!! Au labda kwa familia iliyojaa madume kama ya kwetu, hiyo rule huenda hai-apply!

Lakini nikja kwenye familia ya mama mkubwa, mpangilio upo hivi:-
1. Female
2. Female
3. Female.

Ndoa: #3

Hao huwezi kusema wanaiga mambo ya hovyo kwa sababu ukitoa #1, wengine wote in the family ikiwa ni pamoja na wazazi wao, wanaishi Bush!!

Ni kutokana na hayo, ndo maana huwa nahisi labda sie wengine mafamilia yetu yapo yapo tu!!!
Familia mkiwa wote wanaume haina shida kabisa akitangulia yeyote.
Ila mkiwa wa kike nakwamnbia lazima huruma ikuingie
Sisi kwetu ilikuwa
1.Ke
2.Ke
3.Ke
4.Ke
5.Me
6.Me
7.Ke
Wale wote watatu wa juu waliolewa kwa mtiririko huohuo.
Sasa amebaki #4 na #7 ambaye ni Mimi,
Unampigaje gap hapo mkuu!?!
 
Niijaribu kuvaa viatu vyake mkuu

Kauli yako ya heshima ya mwanamke si ndoa ni kweli kabisa ila jaribu kukaa na wadada walio kwenye 30's uwaone jinsi walivyo na uhitaji na hiyo ndoa.

Sometimes hadi natamani nimtafutie mchumba ila ndiyo siwezi..sijui anachagua mno hata sielewi.
Nafahamu yote hayo Anne, na ndo maana wengine wakifikia 30's wanakuwa tayari kuwa na yeyote yule ili mradi tu nae awe Mrs. fulani!!

Lakini nawe unapojaribu kuvaa viatu vyake, usifunge kamba za viatu kwa nguvu kupindukia hadi unashindwa kuzifungua kwa sababu, wakati upande mmoja unajaribu kuvaa viatu vya dada yako, kwa upande mwingine unatakiwa kuvaa viatu vya nafsi yako!

Katika kupenda mtu, na kwa muktadha huu, katika kumpenda dada yako, unaweza kuwa tayari ku-sacrify your own happines kwa ajili ya "furaha" ya dadako... that's fine!!

Lakini pia usisahau kwamba, wakati utakuwa tayari kuvaa suicide vest na kuifanyia nafsi yako ugaidi wa mapenzi, kwa upande mwingine utakuwa unaifanyia ugaidi nafsi ya mtu mwingine... nafsi ya yule atakayekuwa tayari kukukabidhi moyo wake lakini unaacha kumkabidhi wa kwako kwa sababu ya sister!!

Anyway, nami hivi sasa najisikia nafsi inanisuta kwa kuona ni kama najaribu kumhukumu sister wako, jambo ambalo si sahihi kwa sababu kila kitu kipo mikononi mwako mwenyewe!!
 
Hahaha
Haujamuhukumu mkuu.

Sema Mimi mwenyewe nilikuwa sijafikiria mambo ya kuolewa,ni vile tu alikuwa anajihami[emoji1787]
 
Familia mkiwa wote wanaume haina shida kabisa akitangulia yeyote.
Ila mkiwa wa kike nakwamnbia lazima huruma ikuingie
Sisi kwetu ilikuwa
1.Ke
2.Ke
3.Ke
4.Ke
5.Me
6.Me
7.Ke
Wale wote watatu wa juu waliolewa kwa mtiririko huohuo.
Sasa amebaki #4 na #7 ambaye ni Mimi,
Unampigaje gap hapo mkuu!?!
Duh! Huko kwenu Anne, ni kutamu kweli kweli... au labda niseme hapo kale kabla hawajaanza kutawanyika, kulikuwa kutamu kweli kweli!!!

Na kwa mamlaka ya kiroho (hata kama sina upako) niliyonayo, chige mimi nasema kwamba "Dada yako anafunga ndoa mwakani kati ya Septermber to November"! Sema "Ameeeeeen"!
 
Back
Top Bottom