Utaratibu wa kulazimisha mtoto wa kwanza kuanza kufunga ndoa kwanza kisha ndio wafuate wadogo zake

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Binafsi nitamsubiri dada aolewe
Nitatangulia pale tu atakaponiambia hana mpango wa kuolewa.
Na hapa nilishaanza kumuuliza anaolewa lini ili nichange karata zangu vizuri.
 

Kesho uliyoisema jana si ndo leo?


Hebu tupashe imekuwaje ndio tuchangie tukiwa tunaelewa a to z
 
Yani ambacho ntakifanya nikiisoma akili yako ni kukuvimbisha chini tu na najua una hofu ya mungu huwezi toa hio mimba. Wazazi watajiongeza tu kama watalea mjukuu au watapiga simu nije kukufata.🤣🤣🤣
 
Dada yako hakutakiwa kuongea kauli kama hiyo kwa sababu itakuweka kwenye wakati mgumu kufikia maamuzi inapotokea fursa kama hiyo kwa upande wako!

I don't believe in fate, but your sister should at least know kuna watu wana-believe in fate na kuchukulia hata kama hataolewa kabisa maishani mwake wakati wadogo zake wakiendelea kuolewa, basi yote hayo ni sehemu ya maisha!!

Haya mambo kwamba heshima ya mwanamke ni kuolewa ni lazima yawe dumped in a bin kwa sababu msingi wa yote haya ni kwenye hiyo imani kwamba heshima ya mwanamke ni ndoa!!

I do believe, heshima ya mwanamke is how she behaves in the community!

Hata kama ameolewa lakini bado anaonesha tabia za hovyo hovyo mbele ya jamii bado ndoa yake haiwezi kuwa kigezo cha heshima kwake kwa sababu bado ni jinamizi mbele ya jamii, tena ni jinamizi tisha tisha kuliko mwanamke ambae hajaolewa lakini bado anajiheshimu!!
 
Yani ambacho ntakifanya nikiisoma akili yako ni kukuvimbisha chini tu na najua una hofu ya mungu huwezi toa hio mimba. Wazazi watajiongeza tu kama watalea mjukuu au watapiga simu nije kukufata.[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Sina mpango wa kuzaa na mtu kabla hajanioa
 
Niijaribu kuvaa viatu vyake mkuu

Kauli yako ya heshima ya mwanamke si ndoa ni kweli kabisa ila jaribu kukaa na wadada walio kwenye 30's uwaone jinsi walivyo na uhitaji na hiyo ndoa.

Sometimes hadi natamani nimtafutie mchumba ila ndiyo siwezi..sijui anachagua mno hata sielewi.
 
Sina mpango wa kuzaa na mtu kabla hajanioa
Kwani wote waliozaa walipanga? Mie na cousin alilipiwa mahari na akabaki na mtoto wake to date, japo aliolewa na mtu mwengine akaongeza watoto na maisha yanaendelea.

Hio hutokea na itapokukuta hutakaa huamini. Omba usipitie hilo kama mtihani wa maisha.
 
Ikitokea basi ila sitamani itokee
 
Familia mkiwa wote wanaume haina shida kabisa akitangulia yeyote.
Ila mkiwa wa kike nakwamnbia lazima huruma ikuingie
Sisi kwetu ilikuwa
1.Ke
2.Ke
3.Ke
4.Ke
5.Me
6.Me
7.Ke
Wale wote watatu wa juu waliolewa kwa mtiririko huohuo.
Sasa amebaki #4 na #7 ambaye ni Mimi,
Unampigaje gap hapo mkuu!?!
 
Nafahamu yote hayo Anne, na ndo maana wengine wakifikia 30's wanakuwa tayari kuwa na yeyote yule ili mradi tu nae awe Mrs. fulani!!

Lakini nawe unapojaribu kuvaa viatu vyake, usifunge kamba za viatu kwa nguvu kupindukia hadi unashindwa kuzifungua kwa sababu, wakati upande mmoja unajaribu kuvaa viatu vya dada yako, kwa upande mwingine unatakiwa kuvaa viatu vya nafsi yako!

Katika kupenda mtu, na kwa muktadha huu, katika kumpenda dada yako, unaweza kuwa tayari ku-sacrify your own happines kwa ajili ya "furaha" ya dadako... that's fine!!

Lakini pia usisahau kwamba, wakati utakuwa tayari kuvaa suicide vest na kuifanyia nafsi yako ugaidi wa mapenzi, kwa upande mwingine utakuwa unaifanyia ugaidi nafsi ya mtu mwingine... nafsi ya yule atakayekuwa tayari kukukabidhi moyo wake lakini unaacha kumkabidhi wa kwako kwa sababu ya sister!!

Anyway, nami hivi sasa najisikia nafsi inanisuta kwa kuona ni kama najaribu kumhukumu sister wako, jambo ambalo si sahihi kwa sababu kila kitu kipo mikononi mwako mwenyewe!!
 
Hahaha
Haujamuhukumu mkuu.

Sema Mimi mwenyewe nilikuwa sijafikiria mambo ya kuolewa,ni vile tu alikuwa anajihami[emoji1787]
 
Duh! Huko kwenu Anne, ni kutamu kweli kweli... au labda niseme hapo kale kabla hawajaanza kutawanyika, kulikuwa kutamu kweli kweli!!!

Na kwa mamlaka ya kiroho (hata kama sina upako) niliyonayo, chige mimi nasema kwamba "Dada yako anafunga ndoa mwakani kati ya Septermber to November"! Sema "Ameeeeeen"!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…