GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Msukuma ana helikopta?Wako kibao tu Askofu .Gwajima ana Helikopta Yake,mbunge Msukuma pia anayo helikopta yake,Askofu Mwingira wa Kanisa la Efatha ana ndege yake nk
Ni kweli mfano kuna mashirika ya dini za kikiristo yana ndege zao ndogo.ambazo hutua popote kuliko.na makanisa yao au wanakohudumia huduma kama za afya nk vijijini maporini kusiko hata na barabara za uhakika hutumia ndege zao ndogo au helikopta kutua na kuruka hukoInawezekana mleta mada anataka kuepuka usumbufu kukodi ndege n.k.
Inaelekea ana shughuli au anatarajia kuwa na shughuli zitakazomfanya awe anatumia ndege kila siku Asubuhi na Jioni. Akiwa na yake itampa uhuru wa kupangilia ratiba yake kulingana na uhitaji wa siku husika.
Na pengine, inaweza ikamsaidia kupunguza na gharama zingine, ila sina uhakika.
AnayoMsukuma ana helikopta?
Kweli, aliyesema "don't judge a book by its cover" alikuwa sahihi.
Ninamaanisha dege ndogo ya kawaida (aeroplane) yenye uwezo wa kubeba abiria watatu na helikopta yenye uwezo wa kubeba abiria watatu.
Naomba kufahamishwa:
A. Bei yake ikijumuisha gharama za ununuzi, usafirishaji na usajili
B. Makadirio ya gharama za kuihudumuia kwa mwezi. Wastani wa safari zake kwa mwezi ni kutoka Mwanza kwenda Dar Es Salaam Asubuhi na kurudi Mwanza Jioni
C. Kuna ulazima (Kisheria) wa kuwa na "pilot" zaidi ya mmoja?
D. Kuna unafuu wa gharama (tozo za Serikali) ikiwa itamilikiwa na taasisi ambayo ni non-profiti organization?
E. Utaratibu ukoje kuhusu parking?
F. Sheria inaruhsu kupaki helikopta nyumbani au kwenye uwanja wa ofisi ya taasisi?
Ikiwa kuna taarifa zingine zozote ninazopaswa kufahamu naomba nisaidiwe.
Asante.
Mkuu, nashukuru kwa kunitoa matongo tongo.Ni kweli mfano kuna mashirika ya dini za kikiristo yana ndege zao ndogo.ambazo hutua popote kuliko.na makanisa yao au wanakohudumia huduma kama za afya nk vijijini maporini kusiko hata na barabara za uhakika hutumia ndege zao ndogo kutua na kuruka huko
Kila la heriMkuu, nashukuru kwa kunitoa matongo tongo.
Acha nithubutu kuamini, one day itakuwa "yes".
Sikujui ila Nina uhakika huna hata hela ya wiper ya ndege ,, Kama uko serious nitumie 20k nikwambie Kila kitu ,, najua huwezi kosa hio pesa Kama kweli unanunua degeNinamaanisha dege ndogo ya kawaida (aeroplane) yenye uwezo wa kubeba abiria watatu na helikopta yenye uwezo wa kubeba abiria watatu.
Naomba kufahamishwa:
A. Bei yake ikijumuisha gharama za ununuzi, usafirishaji na usajili
B. Makadirio ya gharama za kuihudumuia kwa mwezi. Wastani wa safari zake kwa mwezi ni kutoka Mwanza kwenda Dar Es Salaam Asubuhi na kurudi Mwanza Jioni
C. Kuna ulazima (Kisheria) wa kuwa na "pilot" zaidi ya mmoja?
D. Kuna unafuu wa gharama (tozo za Serikali) ikiwa itamilikiwa na taasisi ambayo ni non-profiti organization?
E. Utaratibu ukoje kuhusu parking?
F. Sheria inaruhsu kupaki helikopta nyumbani au kwenye uwanja wa ofisi ya taasisi?
Ikiwa kuna taarifa zingine zozote ninazopaswa kufahamu naomba nisaidiwe.
Asante.
Sijabisha mkuu, ni kwamba nimeshangaa!Anayo
Aisee! Umenifanya nicheke hadharani! Umetisha!!!Sikujui ila Nina uhakika huna hata hela ya wiper ya ndege ,, Kama uko serious nitumie 20k nikwambie Kila kitu ,, najua huwezi kosa hio pesa Kama kweli unanunua dege
🙏🙏🙏Kila la heri
Yeap na wanaziita crop dusterMwingine anaweza asiamini. Atakuambia mkulima hana hela ya kumiliki ndege wakati nasikia wengine hata mashamba yao hunyunyizia dawa kwa kutumia ndege.
Kuna mzee mmoja namjuwa anaitwa mwamasika anaiuza mln 250 ya kibongo...Hongera sana kwa kuwaza hilo.
Zipo used ambazo utapata kuanzia 200m.
Ikiwa nje sasa mengine piga hesabu zako.
Au kusanya ununue mpya tu na ukihitaji pilot naweza kuchukua license nikawa naendesha [emoji1]
Inaonekana kuna Watanzania wengi wanaomiliki ndege ingawa wengi hatukuwa tunalijua hilo.Kuna mzee mmoja namjuwa anaitwa mwamasika anaiuza mln 250 ya kibongo...
Ipo tu kaipaki Airport ya zamani huko
Aina ya ndege ni cesna...
Ova
Ndege watu binafsi wanazo wengi tuHadi unanunua ndege
Kumbe alikuwa akiitwa Bob Sambeke, Mimi nilifikiri ni Babu Sambeke!Ndege watu binafsi wanazo wengi tu
Mfano mmoja kuna tajiri Sambeke alikuwa ana ndege yake binafsi akiendesha mwenyewe.Sio ajabu.Akinunua
Alifariki miaka michache iliyopita taarifa yake ilitolewa wakati huo hii hapa
'Kwa mara nyingine, Mikoa ya Kilimanjaro na Arusha imetikiswa, kutokana na kifo cha mfanyabiashara maarufu katika mikoa hiyo, Joseph Sambeke (49) maarufu kama Bob Sambeke.
Bob Sambeke alifariki dunia juzi jioni baada ya kuanguka na ndege ndogo aliyokuwa akiiendesha, kilomita moja kutoka Uwanja wa Ndege wa Arusha wakati akitokea mkoani Kilimanjaro.
Huu ni msiba wa tatu katika muda wa mwezi mmoja kwani mwishoni mwa mwezi jana, Wakili na Mfanyabiashara maarufu mkoani Arusha, Nyaga Mawalla alifariki dunia, ikiwa ni siku moja tagu kufariki ghafla kwa mfanyabiashara mwingine wa madini wa mkoani humo, Henry Nyiti.
Ndege ya Sambeke aina ya MT 7- namba 5H-QTT ilianguka saa 12.34 jioni baada ya bawa lake kugonga mti katika eneo la Magereza linalopakana na uwanja huo.
Alijeruhiwa na baadaye alifariki akiwa njiani wakati akiwahishwa hospitalini na askari wa Magereza ambao wanaishi katika kambi alipoanguka. Mazishi yake yamepangwa kufanyika Alhamisi eneo la Karanga, Moshi.
Meneja wa Uwanja wa Ndege Arusha, Ester Dede alithibitisha jana kutokea kwa ajali hiyo, na kueleza kuwa taarifa za awali zinaonyesha ndege hiyo ni mali ya marehemu Mawalla ambaye alikuwa mbia wa biashara na Bob Sambeki na imesajiliwa kupitia Kampuni ya Quality Tours & Travellers.
Hata hivyo, Wakili Alex Msando, ambaye pia alikuwa mshirika wa Mawalla, aliliambia gazeti hili kuwa Sambeke alikuwa ameinunua ndege hiyo kutoka kwa marehemu.Dede alisema ndege hiyo, ilianguka mita 200 kutoka njia namba 8 ya kuruka ndege katika uwanja huo ikitokea Kilimanjaro, katika dakika 15 za muda wa nyongeza wa matumizi ya uwanja huo.
Alisema ndege hiyo ikiongozwa na rubani Bob Sambeki ina uwezo wa kubeba watu wanne akiwamo rubani. Baadhi ya walioshuhudia tukio hilo, walisema kabla ya kuanguka ndege hiyo, ilikuwa ikiyumba na iligonga mti mkubwa katika moja ya mabawa yake na kupoteza mwelekeo.
Mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo, Julias Laizer alisema kwamba aliona ndege hiyo ikigonga mti na kuyumba, kisha kudondoka chini na ndipo askari wa magereza walipojitokeza kutoa msaada. Laizer alisema Sambeki alikuwa peke yake na alijeruhiwa kichwani."
Ni Bob sambeke sio babuNawafamu Watanzania wawili waliokuwa wakimiliki ndege, japo wote kwa sasa ni marehemu.
Advocate MAWALLA, alikuwa akiishi Arusha, na mtu mmoja aliyekuwa akiitwa Babu Sambeke, nafikiri alikuwa mfanyabiashara. Naye alikuwa na makazi yake Arusha.
Bob Sambeke alikufa Arusha kwa ajali ya ndege aliyokuwa akiirusha.
Naamini kuna na Watanzania wengine wanaomiliki ndege. Hawafahamiki tu kwa vile, pengine, si watu maarufu kwenye vyombo vya habari.
Kipindi fulani nilisikia Askofu Gwajima naye alinunua chopa.
Nashukuru mkuu. Nitarekebisha.Ni Bob sambeke sio babu
Matatizo ya ajira yanafanya watu wanadata.
Maana wenye vimilion 15 vya kununuwa IST tu unajuwa bei za magari utapata kwenye websites za used car kama Be forward, SBT Japan and likes, isitoshe google haijawahi kushindwa jambo ambalo lipo online.
Jikaze walau ununue hata kabaiskeli kakuchaji.Ninamaanisha dege ndogo ya kawaida (aeroplane) yenye uwezo wa kubeba abiria watatu na helikopta yenye uwezo wa kubeba abiria watatu.
Naomba kufahamishwa:
A. Bei yake ikijumuisha gharama za ununuzi, usafirishaji na usajili
B. Makadirio ya gharama za kuihudumuia kwa mwezi. Wastani wa safari zake kwa mwezi ni kutoka Mwanza kwenda Dar Es Salaam Asubuhi na kurudi Mwanza Jioni
C. Kuna ulazima (Kisheria) wa kuwa na "pilot" zaidi ya mmoja?
D. Kuna unafuu wa gharama (tozo za Serikali) ikiwa itamilikiwa na taasisi ambayo ni non-profiti organization?
E. Utaratibu ukoje kuhusu parking?
F. Sheria inaruhsu kupaki helikopta nyumbani au kwenye uwanja wa ofisi ya taasisi?
Ikiwa kuna taarifa zingine zozote ninazopaswa kufahamu naomba nisaidiwe.
Asante.