Utata kifo cha Afisa Usalama Kijitonyama

Utata kifo cha Afisa Usalama Kijitonyama

Wakuu, ni bora huyo kaka yake angeeleza ukweli au inawezekana alimweleza ukweli mwandishi ila aliandika kivyake. Angeeleza kuwa kaka yake alikuwa na matatizo ya akili na pengine hilo ndo lilikuwa chanzo cha yeye kutumbukia kisimani. Pia kuna uwezekano mkubwa kuwa mwandishi hakupata story kamili na ndo kaana anajichanganya wakati wa kuandika. Mara anasema kuwa post mortem ilikuwa imefanyika na wakati huo huo anasema kuwa alipowasiliana na kenyela alimwamnia kuwa uchunguzi unaendelea. Ni vyema angejikita kwanza kujua matokeo ya hio post moterm

Kwahiyo unataka kutuambia marehemu alikuwa na ugonjwa wa akili?? sasa kile kisima si nasikia huwa mnakilinda, sikuhiyo mlimpeleka wapi mlinzi?!

Wewe kama sio Rama basi Ighondu..
 
Mkuu, marehemu hakwenda kuteka maji pale bali alitumbukia aidha kwa bahati mbaya kutokana na matatizo yake ya akili au alijitumbukiza. Taarifa kutoka kwa watu wa karibu zinasema kuwa alishafanya majaribio kadhaa ya kujiua lakini aliweza kuokolewa.

Kama ni huyu Peter Tyenyi tunayemfahamu basi ni wazi kuwa kifo chake hakina mkono wa mtu. Wakati mwingine akifika pale simba kapakatwa alikuwa ana tabia ambayo kila mmoja kama ni mgeni basi utaona ni mtu aliyekosa ustaarabu wa hali ya juu. Unamkuta anaagiza chakula na vinywaji na baada ya kumaliza kula hujipangusa kwenye nguo zake bila ya kunawa na huondoka bila ya kulipa. Pale simba kapakatwa, kijitonyama wanamfahamu sana. Na ndipo story ya kuwa peter alikuwa na matatizo ya akili nilipoupata

Wakuu, ni bora huyo kaka yake angeeleza ukweli au inawezekana alimweleza ukweli mwandishi ila aliandika kivyake. Angeeleza kuwa kaka yake alikuwa na matatizo ya akili na pengine hilo ndo lilikuwa chanzo cha yeye kutumbukia kisimani. Pia kuna uwezekano mkubwa kuwa mwandishi hakupata story kamili na ndo kaana anajichanganya wakati wa kuandika. Mara anasema kuwa post mortem ilikuwa imefanyika na wakati huo huo anasema kuwa alipowasiliana na kenyela alimwamnia kuwa uchunguzi unaendelea. Ni vyema angejikita kwanza kujua matokeo ya hio post moterm
Lazima utakuwa unajua mengi sana kuhusu kifo hiki.
 
Mkuu hicho ni kiinglishi cha kiintelijensia..wala hajachapia!
ukisoma hiyo thread kwa makini kuna kluu nyingi....ila naogopa kutolewa makucha miye!

Hivi nyinyi watu kwa nini huwa hamuandiki Kiswahili ili mueleweke vizuri? Kama basi ni lazima muandike kwa Kiingereza basi andikeni kwa kiingereza kinachoeleweka!
 
hata hayo majibu ya uchunguzi waliyoahidiwa 'yatatengenezwa ' , Ushahidi wangu wa kimazingira unaonyesha bila shaka yoyote kwamba 'ameshughulikiwa '! Pole Mama Mjane uliyeachwa .
 
TISS kwishaaaa!hapo ndiyo wamechochea uasi ndani ya TISS ninaamini sasa tutashuhudia mengi! "Vita vya panzi burudani kwa kunguru". Chanzo cha haya yote ni DHURUMA na tamaa ya kutawala kwa lengo la kujinufaisha binafsi.

Ni kweli kamanda, maana sio wote wanaofurahia haya..
 
Ninaamini kuwa humu jf tuna watu wa usalama wanaofanya kazi pale makao makuu kijitonyama. Ni vema wakatueleza ukweli wa hili tukio
 
Nahisi itakua alilewa kupita kiasi hivyo kudumbukia kisimani.

Ivi we mzee wa kuomba BAN na LIZABONI mbona mpo bize sana kuiaminisha jamii kuwa marehemu alikuwa ni mgonjwa wa akili au mlevi sana? Au nanyi ni TISS mnajaribu kuvuruga ushahidi? Kwa mujibu wa maelezo mke wa marehemu alipopiga simu ofisini alijibiwa kuwa marehemu hakuonekana kazini siku hiyo inawezekanaje mtu mwenye matatizo ya akili au mlevi aingie eneo lililojaa maafisa usalama na asionekane na mtu? Kama kuna uzembe kiasi hicho basi waombeni radhi M23 haraka kabla hawajawaingilia kambini na kuwateketeza wote. Naomba mtambue kuwa wana jf wengi wana uwezo mkubwa sana wa kudadavua mambo hivyo msijaribu kuziba mwanga wa jua kwa kutumia ungo, wote tuvute subira matokeo kamili ya uchunguzi yatatolewa.
 
huyu kauawa kutokana umri wake atakua kuna kitu alikua anajiandaa kuwaumbua magamba wakaona wamBARLOW MAPEMA RIP OFISA.
 
Lazima utakuwa unajua mengi sana kuhusu kifo hiki.
Mkuu, bila kufanya utafiti, huwezi kuwa na hoja sahihi. Binafsi nilipoona taarifa hii kwenye gazeti la leo la mwananchi nilianza kudodosa hapa na pale na ndo nikabaini hayo niliyoeleza. Najua kuna wengi humu jf wana akili za kitoto ndo maana wanakimbilia kupost vitu wasivyovijua
 
Mkuu, marehemu hakwenda kuteka maji pale bali alitumbukia aidha kwa bahati mbaya kutokana na matatizo yake ya akili au alijitumbukiza. Taarifa kutoka kwa watu wa karibu zinasema kuwa alishafanya majaribio kadhaa ya kujiua lakini aliweza kuokolewa.
Angalau sasa umenipa mwangaza.
 
huyu kauawa kutokana umri wake atakua kuna kitu alikua anajiandaa kuwaumbua magamba wakaona wamBARLOW MAPEMA RIP OFISA.
Mkuu, kama watu wa umri huo na zaidi ndani ya tiss wapo wengi sana. Kwa nini awe yeye? Shirikisha bongo zako ipasavyo
 
Imetajwa kuwa Mhe Waziri mmoja Wa Serikali ya JK ndio aliyesambaratisha ndoa ya Peter, sasa mkewe tayari ana mimba ya huyo Waziri. Imetajwa pia Peter aliapa kumuweka wazi Mhe huyo hasa baada ya kusababisha mfarakano na yeye kuamua kumuachia nyumba mkewe pamoja na wtt waliozaa. Japo haijajulikana kama Mhe huyo kahusika lakini kama Serikali inataka kufanya uchunguzi lazima wazifanyie kazi taarifa hizi.
 
Ivi we mzee wa kuomba BAN na LIZABONI mbona mpo bize sana kuiaminisha jamii kuwa marehemu alikuwa ni mgonjwa wa akili au mlevi sana? Au nanyi ni TISS mnajaribu kuvuruga ushahidi? Kwa mujibu wa maelezo mke wa marehemu alipopiga simu ofisini alijibiwa kuwa marehemu hakuonekana kazini siku hiyo inawezekanaje mtu mwenye matatizo ya akili au mlevi aingie eneo lililojaa maafisa usalama na asionekane na mtu? Kama kuna uzembe kiasi hicho basi waombeni radhi M23 haraka kabla hawajawaingilia kambini na kuwateketeza wote. Naomba mtambue kuwa wana jf wengi wana uwezo mkubwa sana wa kudadavua mambo hivyo msijaribu kuziba mwanga wa jua kwa kutumia ungo, wote tuvute subira matokeo kamili ya uchunguzi yatatolewa.
Mkuu, akili za kuambiwa changanya na za kwako. Ni bora ungefanya kautafiti japo kidogo ili ujue marehemu alikuwa anakaa wapi na wapi alikuwa anafanyia kazi. Then hapo ndo utajua uhalisia wa jambo hilo
 
Mkuu hicho ni kiinglishi cha kiintelijensia..wala hajachapia!
ukisoma hiyo thread kwa makini kuna kluu nyingi....ila naogopa kutolewa makucha miye!

Acha uoga Mjanga; tupe hizo kluu na sisi tufaham, majanga japo tu.
 
Back
Top Bottom