Utata: Msanii Roma Mkatoliki na wenzake wakamatwa/tekwa nyara

Roma aliimba akasema wamkamate hata wamtupe kwenye daraja la Mkapa so muwe wapole maneno yanaumba unachokiomba ndio unachopewa,hata maandiko yanasema motto akiomba mkate hauwezi kumpa jiwe unampa mkate
unaonekana umetanuka kwelikweli uwo .....wako....
 
Kama kweli simu ya Roma inapatikana kwa nini Serikali isiwatumie TCRA na polisi kuitafuta sehemu inapo patikana?
 
Duh hii comments imeandikwa ki makini sana. Roma hawezi kuwa na wazazi wawili, pili haya maswala ya kupotea kwa watu hapo Tanzania sasa imekuwa kama movie na ni vigumu kujua lipi ni kweli. Mmoja kapotea miezi kadhaa lakini habari za awali zilisema serikali ilihusika baadae malumbano yakaanza kwa wenyewe kwa wenyewe kwa kutumia gazeti lao kuwa si kweli. Pili hua siamini sana watu wanaoandika kwanza matatizo yao katika social media halafu baadae yanatokea watu wengine siyo kama hatuna uchungu na kupotea kwao lakini inakua ni vigumu sana kuamini moja kwa moja. Kwangu mimi hizi naziita ni movie kama zingine za Magufuli, Makonda, UKUTA, KATA FUNUA. Sina imani na hayo yote na naomba niwe Thomaso siamini pia kama wamepotea. Baba ya Saanane sijamsikia tena wala CHADEMA. Ila kama Serikali inahusika basi itakua ni jambo la ajabu sana maana sioni kitu chochote kibaya ambacho Roma kakifanya labda kama Serikali na watendaji wake wana vichwa vya panzi kama wanaoshabikia hii stori kuwa ya kweli.

Wewe kuniita mimi Bashite hainisumbui maana mwenyewe najijua kama ni Bashite ama siyo halafu bora kuwa Bashite kuliko kuwa mtumwa wa kuadanganywa na wanasiasa kila kukicha. Watu ambao mnajifanya mna akili kumshinda Bashite lakini mnashindwa kutumia akili zenu na kuchezewa na wanasiasa kama wendawazimu kila kukicha ni hatari sana.
 
Sasa waulize serikali usiniulize mimi, maana tatizo habari zenyewe zinakingana wengine wanasema kapotea na wengine wanasema kashikwa na polisi, ndiyo maana mimi binafsi siamini naona ni uzushi tu kama wa Ben Saanane.
 
Sizonje babaake Bashite kua na huruma basi..
Kafanyaje, acheni ushakunaku, nyie ndio wahusika wakuu. Mmeona mmepigwa stop propaganda majukwaani sasa mnataka serikali kupakwa matope. Hamtaweza
 
Nimeelewa msingi wa hoja yako, HUAMINI, ni sinema tu zinazoendelea, sina hakika una kiwango gani cha kujua siasa za dunia na tanzania. Kila kinachotekea kwa upeo wako ni sinema. Naomba nikuache hapo ulipo uendelee kuangalia sinema. Ukiona imeisha naomba unijulishe tuanze kuchambua sinema. Kuanzia mtunzi, muongozaji, waigizaji, mgogoro, na hatima ya sinema ilivyokua. Asante. "Some people appear smart until they speak"
 
Tongwe records haiko msituni. Wanakuja watu ambao hawajulikani wanatokea mamlaka gani wanakwambia njoo huku, ingia kwenye gari, anabebwa wa pili, wa tatu, bila kupiga kelele tumevamiwa, afu watu ambao hata hatuna uhakika walikuwepo eneo la tukio wanasema wametekwa. Gari isiyojulikana ni ya nani imepaki inapakia PC, TV, hakuna anaesoma hata plate namba ya gari hilo, hivi ni vituko. Hakuna anaesema walipoingia studio walijitambilisha wao ni akina nani na kwa nini wamekuja hapo? kwa kutumwa na nani? Kama ulikuwa ni uvamizi walipiga, walitishiwa kwa silaha yoyote, walipiga kelele kuujulisha umma unaozunguka studio hiyo. Au walinyweshwa madawa wasijitambue. Kama ndio walijuaje mwenzao katekwa. Maswali haya hayana majibu.Wasitufanye mazuzu, haya ya mwelekeo wa propoaganda za kisiasa kama upoteaji wa Ben ambae anaefanya nae kazi ilimchukua takribani majuma kadhaa hajitokezi hadharani kusema msaidizi wake wake karibu kapotea katika mazingira gani. Wamebaki eti wana mawasiliano yalioyofanyika kati ya Ben na watu fulani kabla ya kupotea, Nahiuliza, simu zote zimesajiliwa, kama kweli wako serious, kwanini hawakwenda TCRA kuomba majina ya watu waliompigia au kumwandikia meseji kabla ya kupotea wauambie umma kuwa kabla Ben hajatoweka aliandikiwa ujumbe fulana na mtu huyu? Propaganda za kipuuzi tu
 
Homeboy, Mwigulu, hapa ndo tunajua tai na skafu za bendera za taifa siyo uzalendo......actions...power....authority KAMA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI....SEEMS U LACK OF ALL OF THEM. JE, WE NI WAZIRI KIVULI FROM OPPOSITION AS MR. LEMA DOES? ...UNA KOMAND KWELI KWA JESHI LA POLISI?...NINA WASIWASI!
 
Na Bosston George

HABARI

Wanachama wa CCM washangilia kutekwa na kupotea kwa Msanii Roma na wenzake,
Mitaa yote mjini na vijijini CCM wameomekana wakifurahia ukatili wanao tendewa n watanzania wenzetu bila hata chembe ya aibu .
Nimejaribu kupitia page mbalimbali Instagram na Fb za CCM zote zinafurahia kutekwa kwao na uku wakiongezea kuwa Ikiwezekana wauwawe na Kuzikwa Baharini, ( Roho mbaya Jamani)

Nimesoma page ya [HASHTAG]#TanzaMwanga[/HASHTAG] ya CCM
[HASHTAG]#Uvccm[/HASHTAG] tawi la Mitabdaoni
[HASHTAG]#Friends[/HASHTAG] of CCM fb na Instagram page zote zimepost kwamba Roma Afe tu na Wanampongeza Bashite kwa kufanya Kazi yake nzuri sana na wakiongezea kwamba Ikiwezekana apandishwe cheo.
Sasa najiuliza Ivi CCM wafuasi wake ni watanzania kweli?
Au ni wakimbizi kutoka Kongo na Burundi,
Mbona wamejaa roho mbaya za Kishetani?
Ivi kuna Mtanzania anae waunga mkono katika hili?
Wanadai eti Roma Kajiteka,
Huu ni upuuzi uliopitiliza asee,

[HASHTAG]#StukaMtanzania[/HASHTAG]
[HASHTAG]#UkomboziUnakaribia[/HASHTAG]
[HASHTAG]#FreeRoma[/HASHTAG]
 
Uwezo wao wa kufikiri umefika mwisho.

"Asiefunzwa na UKAWA,hufunzwa na CCM"

Zamu yao yaja.
 
Saga linazi kuwa tamu nadhani kuna kitu watanzania tunahitaji kufahamishwa
 
Imebuma
 

Mkuu ongezea na hii, ili dot zigonge vizuri, nimekupa haki miliki [emoji38] [emoji38] [emoji38]
 
Kwa mnaofuatilia muziki wa hiphop nadhani Kalapina sio jina geni. Alisifika sana mwanzoni mwa mwaka 2000 kwa ubabe wake na umahiri wa kupigana kunyanyua vitu vizito n.k.

Wana kundi lao linaitwa kikosi cha mizinga lipo Kinondoni block jamaa walikuwa wanafanya sana mazoezi ya kupigana. Mmoja wao alipata dili la kuwafumdisha askari wetu karate. Kalapina alisifika sana kwa ubabe ambapo aliwahi kuwateka wasaani kadhaa wa bongo fleva akiwemo Solo Thang ambaye mwenyewe alikiri katika wimbo wake fulani.

Nadhani zilikuwa hatua za ukuaji kwani mwaka 2010 aligombea udiwani kwa tiketi ya CUF ila kura zake hazikutosha na mwaka 2015 aligombea ubunge jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya ACT wazalendo. Mara ya mwisho nilikuwa namuona kwenye kipindi cha clouds TV cha hatakati ya kupambana na madawa ya kulevya najaribu kuwaza hao watekajo waliomteka ROMA wangekuja na style gani kama huyu jamaa angekuwa anaendelea na zile harakati za kuimba hiphop ngumu.
 
Hehehe, unachezea chuma cha moto wewe, pale tembo anaangushwa na mtoto mdogo iwe Kalapina? Angedeka ka mtoto mdogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…