Utata wa imani - jirani yangu kaponea tundu la sindano. Ilikua ni kwaheri buriani

Ukishapeleka jina tu, ushajiondoa kwenye uchawi.

Huelewi wapi?
 
Yaani stori nzima kutuaminisha kwamba uchawi na waganga wapo. Nchi imeharibika. Sasa bila shaka utasubiri kuulizwa mganga gani huko iringa ili uanze kupiga hela za udalali. Fanyeni kazi jamani fursa zipo sio kutafuta kudhulumu wenzenu.
 
Ebu Tuma majina ya Mafisadi wa Tanzania na Rais ili wazimwe chap chap..maana majina yao yanajulikana kabisa
 
Afrika hizo mambo kawaida mi nilishangaa kuna kijana alifanyiwa ulozi na mama yake mzazi ikafikia hatua akamtelekeza baba mtu kahangaika akaponea kigoma, baada ya kupona ndo mama anamtaka mwanae, hivi hawa watu akili zao huwa zipo matakoni eti!
No, mama hawezi kumdhuru mwanawe kwa namna yoyote . Japo siamini uchawi.
 
Uchawi upo na una nguvu dhidi ya wale walio katika usawa wa mawimbi yake.

Uchawi ni mawimbi, nishati, nguvu ambayo inaenda kugandamana na mwili wako au ngao ya mwili yako (Auric field) na inatengeneza giza au aina fulani ya NISHATI CHAFU juu yako.

Au, mapepo yanakuganda kwenye mwili wako na kwenye ngao ya mwili wako pale tu ambapo umeweza kushuka kabisa chini katika usawa wa mawimbi ya mapepo.

Mapepo yanafanya kazi kwenye mawimbi ya chini au nguvu ya chini kabisa, kwahiyo ili yakupate lazima ushuke chini katika usawa wao. Ushuke kinishati.

Mimi silogeki, nimejengwa kweli kweli ndani na nje, na pembeni yangu kuna viumbe wenye nguvu ajabu, UKITHUBUTU UTADATA.

Cc: DR Mambo Jambo min -me NAMBA MOJA AJAYE NCHINI Rabbon Pascal Mayalla
 
As per usual story zote za ushirikina ni hearsay tu. Wewe unasimulia kitu ambacho umesimuliwa. Either wewe au aliyekusimulia ni muongo.

Ukitoa story za kijinga za hearsay hakuna ushirikina zaidi ya story story tu mara jana nimekabwa, sijui mtu katokea ukutani, mtu kapaa na ungo mtu kafufuka ndo story za kichawi zinavyoishi hivyo. Ukiulizwa wewe kama wewe nini umewahi kushuhudia na kuthibitisha huu ni ushirikina huna.

Kuamini story za namna hii inabidi na wewe dishi liwe limeyumba maana mtu timamu hawezi kubali kudanganywa kijinga.
 
Ni yule alikuwa mwanamama flan au?cz naskia kuna huyo aliamkia mlimani asubuhi baada ya kuchezewa kichawi ..ila Simiyu ni habar nyingine aysee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…