Utata wa Kifo Cha Hayati Sokoine

Utata wa Kifo Cha Hayati Sokoine

images
images

Hapo ndipo kwenye Mnara wa kumbukumbu ya Moringe Edward Sokoine
Kweli baada ya Kikao cha Bunge kumalizika alikua aondoke na ndege ya Serikali kwenda Dar-es-salaam
Marehemu Sokoine akachagua atatumia Barabara
Heresay: alikuwa kochi la nyuma peke yake na hakufunga mkanda
ajali ilipotokea alirushwa hadi kioo cha mbele na aliummia kifuani sana (km ni headrest ya abiria wa mbele au dreva vilitoboa haya)
Kitu nisichokiamini ni kuwa walimpiga risasi na kumuita Dube eti alipondeponde hilo gari M-Benz mpaka lichakae NO- BIG- NO
Ninachokumbuka nilikuwa Chuoni siku hiyo na tifu ni kuuendeleza msako wake wa WALANGUZI ambao sasa utawavaa viongozi wa juu, wakatihuo alishakatazw kwani alimkamata Waziri Barongo akitaka aswekwe ndani Marehemu Julius Nyerere akamwambia sasa unaifanya kazi visivyo Barongo Mfungulie
Sokoine alikufa kwa ajali ingawa aliuwa na maadui wengi hasa Viongozi wenzake na wale walioupitia Uwaziri mkuu wakiwemo Msuya na Kawawa

sokoine.jpg
 
Another rumour or Conspiracy theory: wkt wa kikao cha Bunge dodoma, Sokoine aliapa akifika far atawachukulia hatua kali Viongozi wa serikali wasiowajibika. Viongozi waliojiona ni waasisi wa tanu na Uhuru, na waliokuwa karibu na nyerere hawakufurahia vitisho hivyo, na tangu awali wala hawakupendezwa na kupanda kwa umaarufu wa sokoine kwa ghafla na kukubalika kwake kwa jamii kutokana na umahili wake wa kushughulikia kwa vitendo kero za wananchi. kwa upande mwingine nyerere pia aliona kupaa na kukubalika kwa sokoine ni tishio kwa Hadhi na umaarufu wake...Kilichoendelea waweza kuunganisha mwenyewe.

Kudhibiti njama zisivuje, mazishi take yalidhibitiwa na serikali, na mwili wake ulizikwa na kufunikwa kwa zege la sement kali na kulindwa na askari kwa miaka mingi.
Hiyo no miongoni mwa mitazamo ya watu kuhusu chanzo cha kifo cha kiongozi Hugo ambaye alitarajiwa kuwa mrithi wa nyerere...
 
La hasha mkuu,

Najaribu kusema tu kwamba hli suala lilikuwa halielezeki si kwa wanafamilia tu bali nchi nzima.

Kuna mambo mengi ambayo hakuna atakaeweka wazi bali ni hadithi tu.

Mkuu hapo nime kuelewa sasa.
 
images
images

Hapo ndipo kwenye Mnara wa kumbukumbu ya Moringe Edward Sokoine
Kweli baada ya Kikao cha Bunge kumalizika alikua aondoke na ndege ya Serikali kwenda Dar-es-salaam
Marehemu Sokoine akachagua atatumia Barabara
Heresay: alikuwa kochi la nyuma peke yake na hakufunga mkanda
ajali ilipotokea alirushwa hadi kioo cha mbele na aliummia kifuani sana (km ni headrest ya abiria wa mbele au dreva vilitoboa haya)
Kitu nisichokiamini ni kuwa walimpiga risasi na kumuita Dube eti alipondeponde hilo gari M-Benz mpaka lichakae NO- BIG- NO
Ninachokumbuka nilikuwa Chuoni siku hiyo na tifu ni kuuendeleza msako wake wa WALANGUZI ambao sasa utawavaa viongozi wa juu, wakatihuo alishakatazw kwani alimkamata Waziri Barongo akitaka aswekwe ndani Marehemu Julius Nyerere akamwambia sasa unaifanya kazi visivyo Barongo Mfungulie
Sokoine alikufa kwa ajali ingawa aliuwa na maadui wengi hasa Viongozi wenzake na wale walioupitia Uwaziri mkuu wakiwemo Msuya na Kawawa

sokoine.jpg

Mkuu one day nitatembelea hapo kwenye mnara wa kumbukumbu,ila sasa braza Ukwaju hivi inawezekana kweli mtu alie funga mkanda kwenye gari tena kakaa siti ya nyuma then arushwe mpaka mbele...!? basi hakuna umuhimu wa kufunga mkanda uwapo kwenye gari.
 
Last edited by a moderator:
Chinga one mimi nakumegea yale ambayo ninayafahamu. Sokoine alikuwa anatokea Dodoma kurejea Dar baada ya kumalizika kwa kikao cha Bunge. Msafara wake ulipofika eneo la Wami Sokoine mkoani Morogoro, jirani na palipojengwa makao makuu ya sasa ya Wilaya ya Mvomero, gari yake ilipata ajali kwa kugongwa na gari L/cruiser iliyokuwa inaendeshwa na Mkimbizi raia wa Afrika ya kusini anaitwa Dumisani Dube aliyekuwa anaishi kwenye Kambi ya wanachama wa ANC hapo Dakawa. Dumisani alishitakiwa mahakamani lakini ninadhani kwa sababu za kisiasa zaidi, mahakama ilimwachia na alirudishwa kwao Afrika ya Kusini. Ajali hiyo ilitokea mchana na Sokoine alipofikishwa Hospitali ya mkoa wa Morogoro, madaktari walithibitisha kifo chake. Miaka kumi baada ya kifo chache, Daktari aliyeufanyia uchunguzi mwili wa Sokoine baada ya kifo, aliweka wazi taarifa ya chanzo cha kifo chake. Sehemu ya taarifa hiyo ilisema kuwa baada ya ajali, Sokoine alivunjika shingo ambayo ilisababisha kubana mshipa wa fahamu (spinal cord) ambayo ilikata mawasiliano kati ya ubongo na sehemu nyingine za mwili. Kumbuka Nyerere na Karume walikuwa maraisi wa nchi, Jamuhuri ya muungano wa Tanzania na raisi wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar, pia waasisi wa mataifa haya, hivyo tunawaenzi kwa sababu hizo kuu tofauti na Sokoine aliyekuwa Waziri mkuu. Mahali alipopatia ajali Sokoine pamejengwa mnara wa kumbukumbu. NINAWASILISHA.

Mkuu Karume baba alipigwa risasi na shemejie mwaka 1977 na mwaka huo 1984 rais alikuwa mzee Jumbe
 
Hakukuwa na utata wowote kwenye ajali ya Sokoine. Wakati ule tulikuwa na vyombo vizuri sana vya DOLA. Ile ilikuwa ni ajali. Sema tu ajali haikustahili kumpata Sokoine wetu ambaye kwa kweli alikuwa ni MJAMAA zaidi hata ya Mwalimu.
Mkuu kubali hii kitu wenziyo wanasema Tazama gari iligongwa upande hupi na Waziri mkuu alikaa wapi!kwa impact hii hwaziri mkuu isingemkuta hii ajali pili kuna gari la kusafisha njia na kukinga (sweeper car guard)Ungesema waziri mkuu alikuwa anaendesha sawa au angekuwa anaendeshewa rwanda sawa maana huko ni keep right!.
 
Cha ajabu humu JF kulikuwa na uzi kama huu lakini sababu isiyoeleweka umetoweka na wasiwasi hata hu utatoweka.

Wanasiasa na wanasahau kuwa jamii isiyopata jibu kwenye jambo fulani haitakata tamaa kudadisi kadri muda unavyokwenda.Mfano mzuri ni kifo cha Yasar Arafata wa palestina mwisho wa siku mwili wake ililazimika uchunguzwe upya na wasiwasi hata hili ya Sokoine iko siku litapata jawabu

Kwa wenzetu nako kulikuwa hivyo lakini a least to some point the story get in rest.

Mkuu mbona mnazidi kuleta majibu yenye utata. kwanza unasema gari iliyosababisha ajali ndio hii apo juu (Toyota Land Cruser) alafu ushaidi mwingine huu hapa chini unaonyesha gari ingine iliyosababisha ajali.

Pichani ni gari lililosababisha kifo cha aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania Mhe:Edward Moringe Sokoine mnamo Tar 12 Mwezi 04 Mwaka 1984 wakati akitokea kwenye kikao cha Bunge mjini Dodoma kwenda jijini Dar – Es – Salaam

sokoine.jpg

Juu ni gari lililosababisha ajari then chini ni gari lililosababisha kifo!
 
kidonto 00:35 Today
By ofisa :
Mkuu Karume baba alipigwa risasi
na shemejie mwaka 1977 na mwaka
huo 1984 rais alikuwa mzee Jumbe
Mimi nafahamu ilikua 1972 na sio
1977

Which is which?
 
Ndugu yangu Ofisa ninajua fika kuwa Karume alipigwa risasi. Mleta uzi hapa ndani alitaka kujua kwa nini tuna siku ya mapumziko KARUME DAY na nyingine NYERERE DAY. Hilo lilikuwa jibu la uzi wake wala sina maana kuwa Karume alikuwepo wakati huo.
 
Ha ha ha!
Unanikumbusha nafikiri mwaka 1972/3 wakati waandshi wa habari wawili, Carl Bernstein na Bob Woodward walipokuwa wanachunguza kashfa ya Rais Nixon, walipewa kavu kavu walipoenda ofisi moja nyeti.

Wao walienda kwa sheria ya uhuru wa magazeti, na wakasema"we want to know the truth about the Watergate scandal"
Huko walimkuta ofisa mmoja mkali kweli kweli akawajibu, " can you HANDLE the truth?"

Jamaa walipoelewa wakaishia.

Katika hili la Sokoine, the truth can be explosive, let bygones be bygones.
Mkuu mimi nikiona mtu anatumia phrase za namna hii napenda sana tena sana yaani namuona ni linguistic na anajua kiingereza, by the way please nipe namna ya kupata hizi misemo maana nazipenda sana zinatia nakshi kwenye kiingereza
 
wewe Unataka kujifunza kiingereza au unakijua kiingereza?
 
Pichani ni gari lililosababisha kifo cha aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania Mhe:Edward Moringe Sokoine mnamo Tar 12 Mwezi 04 Mwaka 1984 wakati akitokea kwenye kikao cha Bunge mjini Dodoma kwenda jijini Dar – Es – Salaam

sokoine.jpg

Picha hapo chini ikimuonyesha Baba wa Taifa ambaye naye ni marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akilia kwa uchungu baada ya kuona mwili wa aliyekuwa rafiki yake kipenzi Waziri Edward Sokoine ukiwa umelala milele.

soko.jpg

Sokoine alifariki kwa ajali ya gari Jumatano ya Aprili 12, 1984 saa 11:30 jioni wakati akitoka kwenye kikao cha bunge Dodoma kuelekea Dar es Salaam
Mwili wa Edward Moringe Sokoine ulizikwa nyumbani kwao Monduli, mkoani Arusha!
Hayo mengine ni maswali ya hisia tu ambayo kila mwenye hisia zake moyoni hana budi kujiuliza bt all in all apumzike kwa amani milele!

leo nimepata darasa lingine, kumbe hisia ziko moyoni, daah moyo una kazi nyingi!
 
state car - Mercedes benz, gari alilopata nalo ajali SOKO liliitajiwa na wenyewe kwa ajili ya uchunguzi, mwl aligoma kulitoa!
 
Back
Top Bottom